Na John Gagarini,
Kibaha
MBUNGE wa
Jimbo la Kibaha mkoani Pwani Silvestry Koka ametoa vyerehani vinnne kwa
Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wilaya ya Kibaha kwa
ajili ya kuendeleza shughuli zao za ujasiriamali.
Akikabidhi
vyerehani hivyo kwa uongozi wa shirikisho hilo Katibbu wa Mbunge huyo Method
Mselewa alisema kuwa mbunge huyo katoa vyerehani hivyo kufuatia ombi lao.
Mselewa
alisema kuwa watu wenye ulemavu nao wanapaswa kusaidiwa kama wanavyosaidiwa
watu wa makundi mengine yanavyosaidiwa ili kujiendeleza kiuchumi.
“Kuwa na
ulemavu siyo mwisho wa maisha kwani nguvu mnazo na mnauwezo kama watu wasiokuwa
na ulemavu na tutaendelea kuwasaidia ili nanyi mjikwamue kwa kujiongezea kipato
chenu na cha familia zenu,” alisema Mselewa.
Alisema kuwa
kutokana na kuungana kwao kutasaidia kuwafikia kwa urahisi kuliko kila mtu
angekuwa anaomba peke yake ingekuwa ngumu lakini kwa kuwa pamoja imekuwa
rahisi.
“Hizi mashine
mnapaswa kuzitunza kwani mbali ya kuwapatia ujuzi kia zitawapatia kipato
ambacho kitaweza kuwafanya muwe na mapato kuliko kuomba jambo ambalo
halifurahishi,” alisema Mselewa.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa SHIVYAWATA Ally Mlanga alisema kuwa wanshukuru msaada huo
kwani kwao huo ni kama mtaji ambao watahakikisha wnaauendeleza.
Mlanga
alisema kuwa wao hawataki fedha ila wanachotaka ni kupewa vitu ambavyo
vitawasaidia kuliko fedha ambazo zinaweza kupotea kwa urahisi.
Naye ofisa
Maendeleo wa Kata ya Kibaha Regina Lazaro alisema kuwa kupatiwa vyerehani hivyo
vitawasaidia kujiongezea kipato kwani moja ya shughuli zake ni kuhamasisha
ujasiriamali.
Lazaro
alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na shirikisho hilo ikiwa ni njia mojawapo
ya kuwasaidia kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali au wadau toka
sekta binafsi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment