Na John Gagarin, Kibaha
MKE wa Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete amesema kuwa kuna haja ya kuondoa
mila na desturi zinazomkwamisha mtoto wa kike kukosa elimu.
Ambapo jamii nzima
inapaswa kumlinda mtoto wa kike ili aweze kufikia malengo yake kwa ukimsomesha
umeisomesha jamii nzima na nchi itapata maendeleo.
Aidha alisema
kuwa mkoa wa Pwani uko ndani ya mikoa 10 yenye matatizo ya mimba za utotoni
ikiwa na asilimia 30 huku mkoa wa Katavi ukiwa ni wa kwanza kwa kuwa na
asilimia 45 jambo ambalo halikubaliki kwa jamii kupinga masuala haya.
Ameyasema wakati wa sherehe za siku ya mtoto kike Duniani
zilizoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Room To Read ambapo kimkoa
zilifanyika Kibaha na kusema kuwa Pwani inapaswa kuongoza kwenye mambo ya
maendeleo na si kuongoza kwa mambo mabaya.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Kibaha Asumter Mshama ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa
wa Pwani amesema kuwa licha ya sheria kali kuwekwa lakini baadhi ya changamoto
zimekuwa zikimkwamisha mtoto wakike kupata elimu.
Naye
mkurugenzi wa Room To Read amesema kuwa wameanzisha mradi wa mtoto wa kike wa
stadi za maisha ili aweze kujitambua na kuwa na maamuzi sahihi na kujiepusha na
vishawishi ambavyo ni vikwazo vya kushindwa kupata elimu.
Kwa upande
wake Ofisa elimu Mkoa wa Pwani Germana Sondoka amesema kuwa changamoto
zinazochangia mtoto wa kike kupata elimu ni nyingi lakini wamekuwa wakijatihidi
kushirikiana na wadau kuzikabili.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment