Na John Gagarini, Kibaha
MAMIA ya wananchi wa wilaya ya Kibaha na mkoa wa Pwani wamelilia
mkuu wa mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo awasidie kupata ajira wazuia msafara
wake kwa mabango kwenye kituo cha ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kilichopo
kwenye Kijiji cha Soga inayojengwa na kampuni ya Yapi Merkezi ya nchini
Uturuki.
Wananchi hao walifikia hatua hiyo wakati mkuu wa mkoa wa Pwani
akiwa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ilipotembelea kujionea ujenzi huo
ambao tayari umeanza na kusema kuwa watu wa mkoa huo wamekuwa wakibaguliwa na
kuajiriwa watu kutoka Jijini Dar es Salaam zaidi wananchi hao.
Kwa upande wa
Rukia Ally amesema kuwa wametumia gharama kubwa kujenga mabanda wanayofanyia
biashara hiyo ya chakula na wamekopa mikopo kwenye taasisia za kifedha hali
ambayo inawapa wasiwasi huenda wakauziwa mali zao.
Ally amesema
kuwa wanahofu kuuziwa mali zao kwani watashindwa kurudisha fedha walizokopa kwa
ajili ya kujenga mabanda na kunuanua bidhaa kwa ajili ya biashara hiyo hivyo
kumwomba mkuu wa mkoa kuwasaidia ili kampuni hiyo iruhusu waendelee kupata
huduma ya chakula nje na si ndani kwa mzabuni.
Kwa upande wake meneja mradi kutoka kampuni Hodhi ya Rasilimali za
Reli (RAHCO) Mhandisi Maizo Mgedzi amesema kuwa wao wanaajiri kutokana na sifa
za waombaji ambao wengi ni madereva na waendeshaji wa mitambo.
Kutokana na malalamiko hayo mkuu huyo wa mkoa wa Pwani ametoa siku
saba kwa vyombo vya dola kufutailia suala la rushwa kama lipo na kutaka
wahusika waliotajwa na wananchi hao kusimama kupisha uchunguzi.
Aidha ametaka kupelekewa majina ya watu waliajiriwa kama wanatoka
mkoa wa Pwani au la kwani serikali imekuwa ikitaka wanufaika wa kwanza wawe
wanaoishi kwenye eneo la mradi.
Pia ametaka utaratibu wa chakula nao uangaliwe ili akina baba na
mama lishe walioko nje ya eneo hilo la mradi huo waruhusiwe kuendelea
kufanyabishara badala ya kuwazuia wafanyakazi wasitoke nje baada ya kupewa
mazabuni kwa ajili ya kuwapa chakula.
Naye mwakilishi
wa mkandarasi wa kampuni hiyo Merz Oz alisema kuwa waliamua kuacha utaratibu wa
wafanyakazi wao kula chakula nje kwa madai kuwa wanatumia muda mwingi na
kufanya shughuli kushindwa kufanyika kwa wakati.
Oz alisema
kuwa sababu nyingine ni kuhakikisha wafanyakazi wanapata chakula chenye ubora
hasa ikizingatiwa kampuni yao ni ya kimataifa hivyo haiwezi kuwaacha
wafanyakazi wao wanakula bila ya utaratibu na huwapatia bure chakula hicho
jambo ambalo lilipingwa na wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment