Na John
Gagarini, Kibaha
CHAMA Cha
Netiboli mkoa wa Pwani (CHANEPWA) kinatarajia kufanya uchaguzi wake Agosti 5
mwaka huu.
Hayo yalisemwa
mjini Kibaha na ofisa michezo mkoa wa Pwani Grace Bureta na kusema kuwa
uchaguzi huo utafanyika Tanita mjini Kibaha.
Bureta
alisema kuwa mchakato wa uchaguzi huo unaendelea ambapo usaili unatarajiwa
kufanyika wiki hii ili kuwapitisha wadau watakaogombea nafasi mbalimbali.
“Mchakato unaendelea
na tunasubiri taarifa kutoka kwenye wilaya za mkoa wetu ili watuletee majina ya
wagombea na baadaye tufanye usaili wiki hii ili kuwapata wale wenye sifa,”
alisema Bureta.
Alisema kuwa
fomu zilianza kutolewa tangu Aprili lakini baadye uchaguzi huo uliahirishwa
kutokana na sababu mbalimbali ambapo sasa unafanyika kesho endapo taratibu
zitakuwa ziko sawa.
“Fomu zote
zinatakiwa zirejeshwe kwa maofisa michezo wa wilaya ambao nao wataziwasilisha
mkoani kwa ajili ya taratibu za uchaguzi huo ambao utawaweka madarakani
viongozi wapya kwa kipindi cha miaka minne,” alisema Bureta.
Aidha alisema
kuwa uchaguzi huo unatarajiwa kusimamiwa na kamati ya michezo ya mkoa na
kuwataka wagombea hao kutimiza taratibu ili wawanie nafasi hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment