Na John
Gagarini,Kibaha
KATA ya Picha
ya Ndege imepata eneo lenye ukubwa wa hekari 11 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya
sekondari ya Kata ambapo kwa sasa wanafunzi wanaotoka kata hiyo wanasoma shule
ya sekondari ya kata kwenye mtaa wa Mkuza.
Hayo
yalisemwa na Diwani wa Kata hiyo Robert Machumbe wakati wa mkutano wa kata
uliofanyika kwenye shule ya Msingi ya Lulanzi na kusema kuwa eneo hilo
limepatikana kutokana na jitihada zake na wananchi.
Machumbe
alisema kuwa licha wanafunzi wanaotoka kwenye kata yake wanasoma kwenye
mazingira magumu kwani darasa moja linawanafunzi 450 hali ambayo inafanya
usomaji kuwa mgumu.
“Watoto wetu
wanapata shida kwanza kule ni mbali na pia madarasa yao yamejaa wanafunzi hivyo
hupunguza ari ya usomaji na ufaulu kuwa mdogo,” alisema Machumbe.
Naye Thomas
Raymond alisema kuwa ujenzi wa shule hiyo itakuwa mkombozi kwa wanafunzi
wanaotoka kwenye kata hiyo ambayo ni mpya ikiwa haina shule yake ya sekondari.
Raymond
alisema kuwa wao wako tayari kuchangia ujenzi wa shule hiyo mara wakati
utakapofika ili kuhakikisha shule hiyo inajengwa haraka kwenye kata yao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment