Thursday, January 23, 2014

MWINJILISTI AU AJINYONGA

Na John Gagarini, Kibaha
MWINJILISTI wa Kanisa Anglikana Eliakia Daniel (35) amekufa kwa kujinyonga baada ya kumuua mkewe Bi Mboni Patrick (28) kutokana na wivu wa kimapenzi.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei alisema kuwa marehemu walikuwa ni wakulima wa Kijiji cha Gama - Makaani wilayani Bagamoyo.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 20 mwaka huu majira ya saa 10 jioni kijijini hapo ambako walikuwa wakifanya shughuli ya kuchoma mkaa.
“Mwinjilisti huyo alimwua mkewe baada ya kutokea wivu wa kimapenzi ndipo alipochukua panga na kumkata kichwani upande wa kulia na kumsababishia majeraha makubwa yaliyosababisha kifo chake,” alisema Kamanda Matei.
Alisema baada ya kumwua mkewe alimfunika kwa magogo sehemu waliyokuwa wakifanyia shughuli zao hizo za kuchoma mkaa kwa ajili ya biashara.
“Baada ya kumwua mkewe alijinyonga umbali wa mita 300 kutoka eneo la tukio,” alisema Kamanda Matei.
Alibainisha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni kutokana na wivu wa kimapenzi na kupelekea tukio hilo kutokea ambalo limewasikitisha wananchi wa kijiji hicho.
Mwisho.

MBUNGE KUZIKWA MIONO

Na John Gagarini, Pwani
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Bw Said Bwanamdogo ambaye alifariki dunia asubuhi Januari 22 mwaka huu katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya tatizo la ugonjwa wa tumbo kwa miaka mitatu anatarjiwa kuzikwa Januari 24 Kijijini kwao Miono wilayani humo.
Akitoa tarifa juu ya msiba huo huko Makondeko msemaji wa familia ambaye ni baba mdogo wa marehemu Bw Omary Nguya alisema kuwa msiba huo utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi.
Bw Nguya alisema mazishi hayo yalikuwa yafanyike Januari 23 lakini yalisogezwa mbele ili kumsubiri Rais ambaye baada ya kupata taarifa aliomba mazishi yahairishwe hadi siku ya Ijumaa ambapo mwili wa marehemu utasafirishwa Ijumaa asubuhi kwenda Kijijini kwake Miono.
 “Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kuanzishiwa matibabu nchini India ambapo mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari hazikuweza kufanikiwa ambapo marehemu alfariki dunia asubuhi Januari 22 akiwa hospitali ya Muhimbili kwa matibabu na marehemu ameacha watoto sita,” alisema Bw Nguya.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoani Pwani Bi Sauda Mpambalioto alisema wamepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kukiri kubadilishwa kwa siku ya mazishi.
“Mbali ya msiba huo pia jana Januari 21 tumemzika mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) kupitia wilaya ya Mkuranga Bi Rukia Msumi ambaye alipata ajali ya pikipiki ambayo ilisababisha kifo chake,” alisema Mpambalioto.
Naye mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Bw Silvestry Koka alisema msiba huo ni pigo kwake kwani walikuwa karibu na marehemu kwa kushirikiana kikazi na kupeana mawazo ya kiutendaji.
Alisema Bwanamdogo alikuwa ni mtu mcheshi ,msikivu ,asiye na majivuno ,alipenda kuzungumza na kila rika pasipo kuwa na majivuno hali inayomfanya awe na kitu cha kuiga kwake.
Kwa upande wake mbunge wa zamani wa Jimbo la Kibaha ambaye kwasasa ni katibu mwenezi mkoani Pwani Dkt Zainab Gama alisema sifa za mbunge wa Chalinze ni nyingi, lakini cha kujivunia kwake ni uadilifu na ucheshi aliokuwa nao.
Dkt Gama alisema enzi za uhai wake atakumbukwa kwa utendaji kazi na kutokuwa mbaguzi kwa wengine.
Mwisho
 

MAENEO YANAUZWA



Maeneo yanauzwa hekari  2,000 liko Mikese kilomita 2 barabara kuu lina hati linauzwa m 400, hekari 1,000 liko Chalinze, liko barabarani  lina hati bei m 500, hekari 900 liko Soga Kibaha lina hati b 3.15, hekari 200 zinauzwa ziko Zogowale km 8 toka barabara kuu ya Moro halina hati linauzwa m 60, hekari 11 na hosteli liko Miembe Saba umbali wa km 1 kutoka barabara kuu ya Moro lina hati m 400, hekari 4 na nyumba zinauzwa liko Kibamba barabarani hati zipo m 400, hekari 100 liko Kwala km 25 kutoka barabara kuu halina hati m 40, hekari 100 liko Mbwawa km 10 toka barabara kuu,  hekari 38 liko Mpiji  lina hati m 133, hekari tano liko Misugusugu barabarani lina hati m 600, hekari 30 liko Misugusugu km 8 toka barabara kuu lina hati m 375, hekari 6 liko Miembe Saba km 2.5 toka barabara kuu halina hati m 100, hekari 6 liko Miembe Saba liko barabarani lina hati m 400, hekari 40 liko Mlandizi km 8 toka barabara kuu lina hati m 400, hekari 9 liko Chalinze liko barabarani lina hati m 400, hekari 11 liko Miembe Saba  km 4 toka barabara kuu lina hati m 35, hekari 20 liko Viziwaziwa/ Kibaha Kwa Mfipa halina hati m 40, hekari 30 liko Kumba Kwa Mfipa km 7 toka barabara kuu halina hati lianuzwa m 60. Kwa mawasiliano piga simu namba 0783 989168, 0754 393118 au 0656 046424.

Saturday, December 14, 2013

JOURNALISM

Other journalism grants

An overview of other organisations, institutions and funds that hand out research grants for investigative journalism.

Arab Reporters for Investigative Journalism – Jordan
In-depth journalism projects for the benefit of the Arab public.
For all journalists who are passionate about telling a story but cannot go ahead with their projects because of budget problems. Funded by Denmark.


The Milena Jesenská Fellowship program offers European journalists time off from their professional duties in order to pursue in-depth research on a topic of their choice. Journalists from Armenia, Azerbaijan, Georgia, and Turkey are also eligible to apply.
The call is directed towards cultural journalists, with the term “cultural” being interpreted in a broad sense to encompass a wide variety of intellectual and artistic fields. However, applicants’ work may also deal with societal issues of European relevance.
 

Thursday, December 12, 2013

WADAKWA NA GONGO LITA 140



Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na Pombe ya Moshi lita 140 katika matukio mawili tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao na ameeleza kuwa  katika tukio la kwanza Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watu saba majira ya saa 10:30 jioni Kijiji cha Oyoyo wilayaya ya Mkuranga.

Kamanda Matei aliwataja watuhumiwa hao kuwa Jubely Lokowano (45), Abdallah Ramadhani (36), Tiago Msuya (35), Halima Khamisi (28), Suzan Moses (25), Zaina Abdallah (40), pamoja na Ramadhani Kinjenge (48) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Oyoyo Wilaya ya Mkuranga ambapo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na lita 40 za Pombe hiyo.

Aliongeza kuwa katika tukio la pili Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukama lita 100 za Pombe ya Moshi pamoja na mtambo mmoja wa kutengenezea Pombe hiyo huko Kijiji cha Kisemvule Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga majira ya saa 10:00 alasiri. 


Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shabani Thomas (22), Francis Felician (21), Mwanjaa Amil (35), pamoja na Lucy Samwel (45).

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

Mwisho.


11 WADAKWA NA GONGO LITA 140



Na John Gagarini, Kibaha

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na Pombe ya Moshi lita 140 katika matukio mawili tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao na ameeleza kuwa  katika tukio la kwanza Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuwakamata watu saba majira ya saa 10:30 jioni Kijiji cha Oyoyo wilayaya ya Mkuranga.

Kamanda Matei aliwataja watuhumiwa hao kuwa Jubely Lokowano (45), Abdallah Ramadhani (36), Tiago Msuya (35), Halima Khamisi (28), Suzan Moses (25), Zaina Abdallah (40), pamoja na Ramadhani Kinjenge (48) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Oyoyo Wilaya ya Mkuranga ambapo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na lita 40 za Pombe hiyo.

Aliongeza kuwa katika tukio la pili Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukama lita 100 za Pombe ya Moshi pamoja na mtambo mmoja wa kutengenezea Pombe hiyo huko Kijiji cha Kisemvule Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga majira ya saa 10:00 alasiri. 


Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shabani Thomas (22), Francis Felician (21), Mwanjaa Amil (35), pamoja na Lucy Samwel (45).

Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao mara baada ya uchunguzi wa awali kukamilika.

Mwisho.


Thursday, December 5, 2013

WAOMBA KUCHOTA MAJI KWENYE MSITU

Na John Gagarini, Kibaha

WANANCHI WA Kitongoji cha Mpiji wilayani Kibaha mkoani Pwani wameuomba uongozi wa Wakala wa Misitu (TFS) Kanda ya Mashariki kuwaruhusu kupita kwenye eneo la msituo huo ili waweze kupata huduma ya maji ya kisima.

Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Mradi wa Mama Misitu moja ya wananchi wa Kitongoji hicho Bw Shaban Nyoka alisema kuwa wamekuwa wakichapwa bakora na walinzi wa msitu huo mara wanedapo kuchota maji.

Bw Nyoka alisema kuwa kutokana na ukosefu wa maji kwenye Kitongoji hicho huwapasa kwenda kuchota maji kwenye visima vilivyopo kwenye hifadhi ya msitu huo.

“Tumekuwa tukichapwa bakora mara tunapokwenda kuchota maji kwenye visima hivyo vya maji lakini cha kushangaza mifugo ya moja ya wawekezaji kijijini hapo imekuwa haichukuliwi hatua yoyote, tunaomba waturuhusu tuwe tunachota maji huko,” alisema Bw Nyoka.
Alisema kuwa watu wamekuwa wakienda kuchota maji huko lakini wanapokutwa huko na walinzi wa msitu wamekuwa wakiadhibiwa kama vile wahalifu jambo limekuwa likiwafadhaisha.
“Sisi tunaomba hifadhi ituruhusu tuchote maji kwani hatufanyi uharibifu wowote kwani lengo letu ni kwa ajili ya kupata maji tu na si kingine hivyo ni vema wanegeturuhusu tupite huko kwa ajili ya kupata maji tu na si vingenevyo,” alisema Bw Nyoka.
Kwa upande wake mratibu wa mradi huo Bw Yahaya Mtonda alisema kuwa tatizo kubwa linatokana na uharibifu ambao umekuwa ukifanywa ndani ya msitu ambapo sheria hairuhusu kufanyika kwa shghuli yoyote.
Bw Mtonda alisema kuwa mipaka iliyowekwa imevikuta visima hivyo vikiwa ndani ya hifadhi hiyo hivyo kama wanataka kutumia visima hivyo ni vema wakaandika barua kwa meneja ili waweze kuruhusiwa kuchota maji kwenye msitu huo.
“Kama mnataka kufanya hivyo ni vema mkaandika barua rasmi kwenye wakala wa misitu wao ndiyo wenye uwezo wa kuruhusu nyie kupata huduma hiyo ya maji lakini lengo si kuwasumbua wananchi,” alisema Bw Mtonda.
Aliwataka wananchi kutumi kamati za misitu kudhibiti waharibifu wa misitu kwani uharibifu umekuwa mkubwa hali ambayo ina hatarisha misitu hiyo ya hifadhi ambayo ni chanzo kikuu cha utunzaji wa mazingira.

Mwisho.