Na John Gagarini, Pwani
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani Bw Said
Bwanamdogo ambaye alifariki dunia asubuhi Januari 22 mwaka huu katika hospitali
ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya tatizo la
ugonjwa wa tumbo kwa miaka mitatu anatarjiwa kuzikwa Januari 24 Kijijini kwao
Miono wilayani humo.
Akitoa tarifa juu ya msiba huo huko Makondeko msemaji wa familia
ambaye ni baba mdogo wa marehemu Bw Omary Nguya alisema kuwa msiba huo
utahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete
ambaye yuko ziarani nchini Uholanzi.
Bw Nguya alisema mazishi hayo yalikuwa yafanyike Januari 23 lakini
yalisogezwa mbele ili kumsubiri Rais ambaye baada ya kupata taarifa aliomba mazishi
yahairishwe hadi siku ya Ijumaa ambapo mwili wa marehemu utasafirishwa Ijumaa
asubuhi kwenda Kijijini kwake Miono.
“Marehemu alikuwa
akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo kwa muda mrefu hali iliyosababisha kuanzishiwa
matibabu nchini India ambapo mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari hazikuweza
kufanikiwa ambapo marehemu alfariki dunia asubuhi Januari 22 akiwa hospitali ya
Muhimbili kwa matibabu na marehemu ameacha watoto sita,” alisema Bw Nguya.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoani Pwani Bi Sauda Mpambalioto
alisema wamepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kukiri kubadilishwa kwa siku
ya mazishi.
“Mbali ya msiba huo pia jana Januari 21 tumemzika mjumbe wa
halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) kupitia wilaya ya Mkuranga Bi Rukia Msumi ambaye
alipata ajali ya pikipiki ambayo ilisababisha kifo chake,” alisema Mpambalioto.
Naye mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Bw Silvestry Koka alisema
msiba huo ni pigo kwake kwani walikuwa karibu na marehemu kwa kushirikiana
kikazi na kupeana mawazo ya kiutendaji.
Alisema Bwanamdogo alikuwa ni mtu mcheshi ,msikivu ,asiye na
majivuno ,alipenda kuzungumza na kila rika pasipo kuwa na majivuno hali
inayomfanya awe na kitu cha kuiga kwake.
Kwa upande wake mbunge wa zamani wa Jimbo la Kibaha ambaye kwasasa
ni katibu mwenezi mkoani Pwani Dkt Zainab Gama alisema sifa za mbunge wa Chalinze
ni nyingi, lakini cha kujivunia kwake ni uadilifu na ucheshi aliokuwa nao.
Dkt Gama alisema enzi za uhai wake atakumbukwa kwa utendaji kazi
na kutokuwa mbaguzi kwa wengine.
Mwisho
No comments:
Post a Comment