Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi Mkoani
Pwani linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kukutwa na Pombe ya Moshi lita 140
katika matukio mawili tofauti.
Akizungumza na waandishi
wa habari mjini Kibaha , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi
Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei amethibitisha kushikiliwa kwa watu hao na
ameeleza kuwa katika tukio la kwanza Jeshi la Polisi lilifanikiwa
kuwakamata watu saba majira ya saa 10:30 jioni Kijiji cha Oyoyo wilayaya ya Mkuranga.
Kamanda Matei aliwataja
watuhumiwa hao kuwa Jubely Lokowano (45), Abdallah Ramadhani (36), Tiago Msuya (35),
Halima Khamisi (28), Suzan Moses (25), Zaina Abdallah (40), pamoja na Ramadhani
Kinjenge (48) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Oyoyo Wilaya ya Mkuranga
ambapo watuhumiwa hao walikutwa wakiwa na lita 40 za Pombe hiyo.
Aliongeza kuwa katika
tukio la pili Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukama lita 100 za Pombe ya Moshi
pamoja na mtambo mmoja wa kutengenezea Pombe hiyo huko Kijiji cha Kisemvule
Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga majira ya saa 10:00 alasiri.
Waliokamatwa katika
tukio hilo ni Shabani Thomas (22), Francis Felician (21), Mwanjaa Amil (35),
pamoja na Lucy Samwel (45).
Watuhumiwa wote wanatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao mara baada ya uchunguzi wa awali
kukamilika.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment