Thursday, December 5, 2013

HABARI ZA PWANI

Na John Gagarini, Kibaha
HUKU kiwango cha maambukizi  ya ugonjwa wa UKIWMI wilayani Kibaha Mkoani Pwani kikiwa kimepanda kutoka
asilimia 7 mwaka jana hadi hadi kufikia asilimia 9.7 mwaka huu  wakazi wa kata ya Kikongo imetakiwa kuepukana unyanyapaa ili kupunguza maambukizi mapya.
Taarifa zinaonyesha kuwa idadi ya waliopata ushauri na kupima kwa kipindi
cha mwezi Januari hadi Desemaba mwaka huku waliopima ni
6,850 kati yao waliokutwa na maambukizi ya VVU ni 665 wanaume 214 na
wanawake 451.
Akizungumza na wananchi wa kata hiyo wakati wa mafunzo ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo iliyoandaliwa na asasi ya kuwaletea maendeleo vijana ya Mlandizi Kibaha (YEN), diwani wa kata hiyo Bi Fatuma Ngozi alisema kuwa moja ya vitu vinavyochangia maambukizi mapya kuendelea ni kutokana na unyanyapaa ambao unaendelea ndani ya jamii.
Bi Ngozi alisema kuwa unyanyanyapaa unasababisha watu walioathirika kushindwa kujibainisha hivyo kuendelea kueneza ugonjwa huo kutokana na kuwa wasiri.
“Jamii inapaswa kuepukana na unyanayapaa ili kuondoa usiri uliopo kwani endapo wangeweka wazi hali zao ili jamii itambue na kuwasaidia,” alisema Bi Ngozi.
Alisema kuwa takwimu zinaonyesha maambukizi kuongezeka licha ya elimu kutolewa kila wakati lakini bado tatizo hilo linaendelea kuwa sugu.
“Kuna sababu nyingi ambazo zimekuwa chanzo cha maambukizi mapya ya ugonjwa huo lakini mojawapo ni unyanyapaa unaoendelea ndani ya jmii,” alisema Bi Ngozi.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Naye mkurugenzi wa mtandao wa kuwapatia uwezo vijana (YEN) wa Mlandizi wilyani Kibaha ambao ndiyo walioandaa tamasha hilo Bw Issa Lukolo alisema kuwa lengo mafunzo hayo ni kuwakumbusha watu kujikinga na UKIMWI na kuepukana na njia zinazochangia maambukizi mapya.
Lukolo alisema kuwa jamii inapaswa kuepukana na vitendo ambavyo vimekuwa chanzo cha maambukizi ya ugonjwa huo ambao umekuwa ukimaliza nguvu kubwa na kusababisha jamii kutumia muda mwingi kuuguza wagonjwa.
Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WAZAZI nchini wameaswa kuhakikisha wanashirikiana na kusimamia malezi ya watoto wao badala ya kuwaachi wasichana wa kazi hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa mmmonyoko wa maadili.
Hayo yalisemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishina Msaidizi Mwandamizi Ulrich Matei katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Pwani Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SSP) Atumani Mwambalaswa wakati wa mahafali ya sita katika shule ya awali ya Memory Day Care Centre iliyopo Kibaha Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, Kamanda Mwambalasa alieleza kuwa ni jukumu la kila familia kuhakikisha kuwa, inajiwekea malengo na mikakati ya kuhakikisha haizalishi wahalifu bali inazalisha watu wema na waadilifu.

“Kila mmoja katika familia yake kukataa kuwa na mhalifu na hivyo iwapo sote tukiunganisha nguvu katika mradi mpya wa Jeshi la Polisi uliozinduliwa hivi karibu na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema wa Familia yetu haina Mhalifu basi uhalifu utapungua na jamii yetu kuwa salama,”. Alisema Kamanda Matei

Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsi na watoto Mkoa wa Pwani Mrakibu wa Polisi Yusta Milinga, (SP) aliwaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwenye madawati yaliyopo kwenye Mkoa na kuwafichua wale wote ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivyo ili sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na amewataka wazazi na walezi kutokubali kuyamaliza matukio ya ukatili wa jinsi majumbani mwao.

Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho Bi Margareth Njimba alisema kuwa kutokana na kutambua umuhimu wa malezi ya mtoto na usalama wao katika makuzi, shule yao wameamua kuanzisha tawi la kupambana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika shule hiyo kwa kushirikiana na wazazi wa wanafunzi hao pamoja na dawati linalohusika na maswala ya kupambana na vitendo vya ukatili ndani ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani.
Mahafali hayo ya sita katika shule hiyo yalienda sambamba na uzinduzi wa tawi hilo uliofanywa na Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Pwani ambapo tawi hilo litakalokuwa na jukumu la ulinzi na usalama wa Mtoto ili kumfanya awe na makuzi yaliyona maadili jamii.


Mwisho

No comments:

Post a Comment