Sunday, May 17, 2026

MBUNGE SUBIRA MGALU ATOA MSAADA KWA VITONGOJI VILIVYOKUMBWA NA MAFURIKO BAGAMOYO


MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Subira Mgalu ametoa kiasi cha shilingi milioni 2 kwa Vitongoji vya kata ya Nianjema vilivyokumbwa na mafuriko.

Mgalu amesema vitongoji hivyo vilivyokumbwa na mafuriko yaliyosababisha kuharibika kwa Miundombinu ya barabara na maji kuzingira makazi na taasisi za Umma. 

Nimewapa pole , na nimewaahidi ntaendelea kuwasemea kero hii Bungeni na kwenye Mamlaka mbalimbali .

 Tangu 2018 mafuriko yalipoanza nimekuwa Kiongozi wa kwanza kuwafikia na kuwafariji # Mbunge wa Jimbo Kazini

No comments:

Post a Comment