Na John
Gagarini, Kibaha
MWANAMKE
mmoja ambaye ni mfanyabiashara Mariamu Omary (31) mkazi wa Mtaa wa Muharakani
wilayani Kibaha mkoani Pwani ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari mjini Kibaha na Blasius
Chatanda kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoani Pwani alisema kuwa marehemu
aliuwawa na watu wasiofahamika.
Kamanda
Chatanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Kwa Mathias majira ya saa 7
usiku umbali wa mita 40 toka kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.
“Marehemu
alikutwa asubuhi huku akiwa amevuja damu nyingi sehemu za usoni na kichwani na
alikutwa na jeraha kubwa kichwani upande wa kushoto,” alisema Chatanda.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Muharakani Hamis Mwarizo alisema kuwa marehemu
alipigiwa simu usiku na mtu ambaye jina lake linaonekana kwenye simu ya
marehemu.
Mwarizo
alisema kuwa waliingia kwenye chumba cha marehemu na kuzikuta simu zake mbili
na moja inaonyesha ilipigwa usiku huo na inaonekana baada ya kupigiwa ndipo
alipotoka ndipo alipokutwa na umauti.
Naye
mama mwenyenyumba Miriamu John alisema kuwa marehemu alikuwa ni mgeni kwenye
nyumba yake akiwa na miezi akiwa na miezi miwili tu na siku ya tukio hawakuweza
kusikia kitu chochote.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment