Na John
Gagarini,Kibaha
MTU mmoja anayedhaniwa kuwa ni jambazi mmoja ameuwawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa kisha kuchomwa moto kwa tuhuma za kupora pikipiki.
Kamanda
wa Polisi mkoani Pwani Jonathan Shana alisema kuwa kuwa tukio hilo lilitokea
Julai 23 majira ya saa 1:45 usiku kitongoji cha Amani kata ya Kerege tarafa ya
Yombo wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda
Shana alisema kuwa marehemu akiwa na wenzake watatu wakiwa na silaha
inayodhaniwa kuwa ni bastola walimvamia mwendesha pikpiki aitwaye Mbaraka Joel
(25) mkazi wa Amani walimpora pikipiki yake yenye namba za usajili T 852 BRA
aina ya Sanlg.
“Watu
hyao kabla ya kufanya uporaji walimsimamisha wakijifanya kuwa ni abiria lakini
ghafla walimbadilikia kwa kufayatua risasi mbili hewani na kumtaka awape
pikipiki ambayo aliiachia na kutoweka nayo kusikojulikana,” alisema Shana.
Alisema
baada ya taarifa kulifikia jeshi la polisi wilaya ya Bagamoyo waliendesha msako
mkali kwa kushirikiana na wananchi kupitia vikundi vyao vya ulinzi shirikishi
kwenye maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Mtambani.
“Wananchi
hao waliweza kuwakurupusha watu hao wakiwa wanapanga mipango ya kwenda kufanya
uhalifu sehemu nyingine na kutokana na idadi ya wananchi kuwa kubwa watu hao
walikimbia na kutelekeza pikipiki mbili moja walioipora kwa Joel na nyingine
yenye namba za usajili T MC 972 AJM aina ya Boxer,” alisema Shana.
Aidha
alisema kuwa wananchi hao waliendelea kuwakimbiza na kufanikiwa kumkamata
marehemu ambapo walimpiga kwa mawe na marungu kisha kumchoma moto na kupoteza
maisha papo hapo.
“Wananchi
hawapaswi kujichukulia sheria mikononi kwa kuwaua wahalifu wanapaswa
kuwakabidhi polisi kwa ajili ya hatua za kisheria pia wataweza kubaini mtandao
wa wizi kuliko kuwaua,” alisema Shana.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment