Friday, December 18, 2015

WATATU WAFA AJALINI PWANI

Na John Gagarini,Kibaha

WATU watatu wamefariki dunia leo katika matukio mawili ya ajali yaliyotokea mkoani Pwani.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Boniventura Mushongi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo, ambapo amesema katika tukio la kwanza watu wawili walifariki dunia kwenye ajali iyotokea huko Mbala Kijiweni wilaya ya Kipolisi Chalinze .

Amesema katika tukio hilo gari lenye namba za usajili T.743 BTV aina ya scania Lori likiendeshwa na Hashim Sadick(30) mkazi wa Gairo ikitokea Dar es salam kuelekea chalinze iligongana uso kwa uso na gari yenye namba za usajiliT.846 BXU aina ya Fuso ikiendeshwa na Cosmas Mwaifule.

Kamanda Mushongi amesema,madereva wa magari hayo walikufa baada ya ajali hiyo kutokea.
Amesema ajali nyingine imetokea  baada ya gari lenye namba za usajili T.290 DFS aina ya Isuzu mali ya kampuni ya magazeti ya Mwananchi ikiendeshwa na Elisha Mmari ikitokea Dar es salaam kwenda Mbeya ilimgonga mwendesha pikipiki na kumsababishia kifo.
Kamanda Mushongi amesema jina la dereva huyo wa pikipiki halikufahamika  na ajali imetokea eneo la Visiga  wilaya ya Kibaha.

Chanzo cha ajali hizo kinadaiwa kuwa ni kupishana bila tahadhari(overtaking) pasipo uangalifu.

Miili ya marehemu wote watatu imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Tumbi ikisubiri uchunguzi wa daktari.

Mwisho

No comments:

Post a Comment