Na John Gagarini, Kibaha
WATU waliokuwa wakijihusisha na ukwepaji kodi hapa nchini wametakiwa kutubu mbele za Mungu na kurejesha kile walicho kila ikiwa ni sehemu ya kuonyesha utii kwa mamlaka iliyopo madarakani kwani imewekwa na Mungu.
Hayo yalisemwa jana mjini Kibaha na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Maili Moja Kibaha Isai Ntele kwenye Ibaada ya Krismasi na kusema kuwa kurejesha kile walichokwepa ni kumwogopa Mungu ambaye anataka kila mtu awajibike kwa kiongozi aliye madarakani.
Mch Ntele alisema kuwa Mungu alisikiliza kilio cha watanzania kwa kuwapa kiongozi ambaye ana uchungu na wananchi wake kwani ameonyesha dhahiri kuwa hataki haki za wanyonge zipotee kwa kudhulumiwa na wachache.
“Hata Biblia ina sema kila mtu aitii mamlaka iliyo kuu kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo nimeaminiwa na Mungu hivyo aisye na mamlaka asipotii anashindana na agizo la Mungu hivyo watapata hukumu,” alisema Mch Ntele.
Alisema wakwepa kodi wanapingana na agizo la Mungu hivyo kwa wale waliofranya hivyo wanapaswa kulipa kodi au ushuru ili kuonyesha utii kwa mamlaka iliyopo sasa na watakuwa wamemweshimu Mungu.
“Waliokuwa wakikwepa wasirfanye hivyo tena na watubu na watasamehewa dhambi hiyo waliyoifanya na Mungu atatuelekeza kwenda kwenye njia sahihi kwani tutapata mema ya nchi yetu kama Mungu alivyo agiza,” alisema Mch Ntele.
Aliwataka wakristo kutumia kumbukumbu ya kuzaliwa kristo kwa kutenda mema na kuachana na matendo maovu ambayo hupelekea uvunjifu wa amani ili kuenzi upendo wa Yesu ambao ndiyo unaobeba sherehe hizi za Krismasi.
Naye mwinjilisti wa mtaa wa Luguruni Huruma Foya alisema kuwa watu wanapaswa kumwombea Rais akae kwenye mkono wa Mungu atatekeleza yale ambayo Mungu atamuelekeza katika kuiongoza nchi.
Foya alisema kuwa wakimwombea atakuwa ni msafi na hatatoa maamuzi ya kukurupuka ambayo yatawaumiza wananchi bali ataongozwa na Mungu katika shughuli mbalimbali za kuwatumikia wananchi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment