Thursday, December 19, 2024

KAMPUNI YA PPM GROUP YAHAMASISHA NISHATI SAFI NA UTUNZAJI MAZINGIRA

KAMPUNI ya PPM Group inahamasisha wananchi kuwa na matumizi ya nishati safi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni ili kunusuru misitu ambayo inaathiriwa na matumizi kama hayo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Uwekezaji na Biashara Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya PMM Group Dk Judith Spendi amesema matumizi yanayopaswa kutumika kwa kupikia ni ya nishati safi.

Dk Spendi amesema kuwa Dar es Salaam na Pwani inatumia mkaa tani milioni 2.4 kwa mwaka hali ambayo ni hatari kwa misitu.

"Tunahamasisha matumizi ya majiko sanifu ambapo tutaanza uzalishaji wa majiko sanifu na upandaji miti ili kuepuka mabadiliko ya tabianchi,"amesema Dk Spendi.

Waziri wa Viwanda na Biashara Suleiman Jaffo aliipongeza kampuni ya PPM Group kwa jitihada zake za kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia. 

STAMICO YATAKA WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA NISHATI SAFI NA SALAMA YA MKAA WA RAFIKI BRIQUETTES


KATIKA kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limewataka Watanzania kutumia Mkaa wa Rafiki Briquettes.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na ofisa masoko wa (Stamico) Hope Mahokola wakati wa maonyesho ya Uwekezaji na Biashara ya Mkoa wa Pwani.

Mahokola amesema kuwa mkaa huo ni nishati safi na salama na una uwezo wa kuwaka kwa zaidi ya saa tatu baada ya kuwashwa.

"Tunamuunga mkono Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ili kulinda mazingira ili kutoharibu uoto wa asili ili usisababishe mabadiliko tabianchi hivyo Watanzania watumie mkaa wa Rafiki Briquettes ili kulinda mazingira,"amesema Mahokola.

Amesema kuwa mkaa huo unatolana na mabaki ya makaa ya mawe hauna moshi na ni safi na salama katika kupikia na unachangia kupunguza mabadiliko ya Tabianchi.

"Mkaa huu unaweza kutumika nyumbani, vyuoni, mashuleni na sehemu nyingine zenye uhitaji wa nishati ya kupikia,"amesema Mahokola.

Aidha amesema kuwa mkaa huo ni rafiki kwa matimizi, mazingira na gharama na mkaa huo unatokana na makaa ya mawe yanayochimbwa kwenye mgodibwa Kiwira-Kabulo Mkoani Songwe.

TAASISI YA ANJITA YATAKA USHIRIKIANO KUKABILIANA NA UKATILI WA KIJINSIA










TAASISI ya Anjita Child Development Foundation iliyopo Halmashauri ya Mji Kibaha imeomba wadau wa kupinga ukatili kushirikiana ili kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Anjita Janeth Malela amesema kuwa ili kufikia hatua ya kupunguza matukio hayo lazima watu, taasisi na mashirika waungane kukabili vitendo hivyo.

Malela amesema kuwa kabla ya kufikia hitimisho la siku hizo 16 za kupinga ukatili walitoa elimu kwa jamii juu ya kukabiliana na vitendo hivyo ambapo jamii imepata uelewa kwani wamejengewa uwezo.

"Tumetoa elimu hiyo na imeonyesha kuwa ndani ya jamii bado matukio kama hayo yanajitokeza hivyo tumewapatia uelewa na namna ya kuripoti mara waonapo matukio kama hayo ili hatua stahiki zichukuliwe,"amesema Malela.

Amesema kuwa ili kupunguza au kutokomeza vitendo hivyo lazima wadau waungane kwa pamoja kwa kutoa elimu kwa jamii ili kukabili vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Taasisi ya Anjita inashughulisha zinazohusiana na watoto na vijana pia kundi la watu wazima kupitia elimu ya malezi changamshi  kwa wazazi na walezi kupitia mradi wa Mtoto Kwanza.

Katika kuhitimisha kilele hicho cha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili Taasisi ya Anjita ilipewa cheti cha pongezi na ófisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani cha kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia maeneo mbalimbali ya Mji wa Kibaha.

Wednesday, December 18, 2024

KINGLION KUTOA AJIRA



KIWANDA cha kuzalisha malighafi zitumikazo kwenye uzalishaji vyuma na mabati na usambazaji wa pikipiki cha Kinglion kinatarajia kutoa ajira kwa watu 1,500 ajira za kudumu na ajira za muda zaidi ya 5,000.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa wiki ya maonyesho  ya Biashara na Viwanda ya Mkoa wa Pwani meneja wa kiwanda hicho Anold Lyimo amesema kuwa kiwanda hicho kitafunguliwa muda siyo mrefu.

Lyimo amesema kuwa mara kiwanda hicho kitakapoanza uzalishaji vijana wengi watapata ajira na kuongeza pato la Taifa kwani kitakuwa kiwanda kikubwa na kitauza bidhaa zake hadi nje ya Tanzania yaani nchi jirani.

"Kiwanda kilikuwa kianze uzalishaji mwaka huu lakini kuna changamoto kidogo ikiwa ni pamoja na barabara na gesi ambavyo serikali inavifanyia kazi ili kukabili changamoto hizo,"amesema Lyimo.

Aidha alisema kuwa wanatarajia kiwansa kitakapoanza kazi kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 35,000 kwa mwaka.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amesema kuwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) wataijenga barabara ya kuelekea kiwandani huko yenye urefu wa kilometa 2.5.

Kunenge amesema kuwa pia wanatarajia kusambaziwa gesi kwenye eneo la viwanda la Zegereni ikiwemo kwenye kiwanda hicho cha Kinglion.

MLEZI WA KAMATI YA USALAMA BARABARANI ACP MORCASE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI


Mlezi wa Kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi wa Polisi Salim Morcase Disemba 17 amekiongoza kikao cha kamati ya usalama barabarani ambacho kimejadili maswala mbalimbali ikiwemo kuondoa msongamano wa foleni kwenye barabara kuu za Mkoa wa Pwani na kuweka mikakati ya pamoja ya kumaliza foleni hizo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kali kwa madereva watakaobainika kupandisha nauli za mabasi kwenye kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka pamoja na madereva wanaokaidi kutii Sheria za usalama barabarani kwa watumiaji wengine wa barabara.

Saturday, December 14, 2024

VITENDO VYA UKATILI PWANI VYAPUNGUA










HUKU Tanzania ikiwa imehitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili matukio kwa Mkoani wa Pwani yamepungu kutoka matukio 8,573 mwaka 2023 na kufikia matukio 6,916 mwaka huu sawa na asilimia 19.3.

Hayo yamesemwa na Edna Kataraiya kutoka Ofisi ya Mipango na Uratibu Mkoa wa Pwani wakati wa kuhitimisha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili kimkoa zilifanyika Kwa Mbonde Wilayani Kibaha.

Kataraiya amesema kuwa ofisi yake inashughulikia matukio yanayohusiana na matukio hayo kwa asilimia 40 huku matukio mengine asilimia 60 yanashughulikiwa na idara ya afya.

Kwa upande wake Polisi Kata ya ya Picha ya Ndege Ibrahim Makaruti amesema kuwa moja ya changamoto inayojitokeza ni baadhi ya wazazi kumalizana nyumbani pasipo kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu Wenye Ulamavu Tanzania (SHIVYAWATA) Kibaha Mjni Jabir Makasala alisema kuwa kutungwe sera ya kuwakopesha wazazi wenye watoto wenye ulemavu ili wafanye shughuli za ujasiriamali kwani wazazi hao hawana kipato chochote.

Naye Mkurugenzi wa African Talent Forum (ATF) Rosemery Bujash amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa vijana wa makundi mbalimbali kupitia sanaa na michezo.

Akitoa salamu za taasisi ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mariam Mnengwah amesema kuwa wao walitoa elimu iliyosaidia kuibua vitendo vya ukatili na kutoa msaada wa kisheria na msaada wa matibabu.





  

CATHERINE MWENYEKITI MTAA WA SOFU NA MKAKATI WA KUJENGA OFISI SERIKALI YA MTAA.


**Catherine baada ya kumshinda Mwenyekiti mwanaume aliyeongoza kwa miaka 10 na kuambiwa Mtaa hauwezi kuongozwa na Mwanamke aondoa mawazo hayo, lengo lake ni kujenga ofisi ya Serikali ya Mtaa**

MWENYEKITI wa Mtaa wa Sofu kata ya Sofu wilaya ya Kibaha Catherine Lyimo ameweka mikakati ya kuhakikisha mtaa huo unakuwa na ofisi yake badala ya kupanga.

Lyimo akizungumza na mwandishi wa habari hizi amesema kuwa hilo ndiyo jambo ambalo ni kipaumbele chake mara baada ya kuchguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mita uliofanyika hivi karibuni na yeye kushinda nafasi hiyo.

Amesema kuwa eneo tayari wanalo wanachofanya ni kuwaandikia wadau wa maendeleo kwenye mtaa huo kwa kushirikiana na wananchi kufanya ujenzi huo ambao ni ndoto yake kuhakikisha mkakati wa kuwa na ofisi unafanikiwa.

“Mpango mkakati wa mtaa kwa sasa ni kuwa na ofisi yake badala ya kutumia ofisi za watu wengine tunataka tuwe na ofisi yetu wenyewe ili tufanye kazi kwa uhuru badala ya kutegemea wengine kwani kutumia ofisi za watu wengine kuna changamoto zake,”amesema Lyimo.

Aidha amesema kuwa anamatumaini ofisi itajengwa kutokana na ushirikiano anaoupata kutoka kwa wananchi na wadau wa maendeleo kwani anaamini ushirikiano huo utafanikisha kupatikana kwa ofisi ya mtaa huo.

“Nataka kwa kushirikiana wananchi na wadau kuhakikisha tunaacha alama ya uongozi kwa kujenga ofisi yetu kwani tukiwa na ofisi yetu tutakuwa na uhuru na tutajenga kutokana na mahitaji ya mtaa wetu ambapo itakuwa na vyumba kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi,”amesema Lyimo.

Amebainisha kuwa jambo lingine ambalo atahakikisha linafanyika ni kuwagawia wananchi eneo la kufanyiabiashara kwa ananchi wa mtaa huo ili waweze kupata huduma ya soko karibu kwani wanataka liwe soko dogo ili kuwaongezea wananchi kipato na kutoa huduma.

“Tunahitaji tuwe na eneo ambalo litakuwa kama soko ambapo wananchi watauza bidhaa zao badala ya kwenda mbali kufuata mahitaji yao nyumbani tunataka wapate hapa jirani na pia itakuwa ni sehemu ya kujiongezea kipato,”amesema Lyimo.

Lyimo alifanikiwa kushinda nafasi hiyo baada ya kumshinda aliyekuwa mwenyekiti wa Mtaa huo Lazaro Joseph ambaye aliongoza kwa vipindi viwili vya miaka 10 huku yeye akiwa ni mjumbe wa serikali ya mtaa huo ambapo alishindwa kwenye nasafi hiyo na mtangulizi wake mwaka 2019 na alikuwa ni mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Kata ya Sofu na Mjumbe wa mtaa.