Wednesday, August 21, 2024
DC KIBAHA ATAKA MADIWANI KUKAGUA NA SI KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO
Sunday, August 18, 2024
TAKUKURU PWANI KUTOA ELIMU KUELEKEA UCHAGUZI
waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha wanatarajia kuyafikia makundi yote yanayohusika na masuala ya uchaguzi.
Haji alisema kuwa baadhi ya makundi ni pamoja nan a vyama vya siasa, wasimamizi wa uchaguzi,
waandishi wa habari wananachi na jamii kwa ujumla.
"Kwa kipindi hichi cha mchakato wa uchaguzi tumeshaanza kufanya ufuatiliaji wa vitendo vya rushwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji utakaofanyika mwaka huu na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani,"alisema Haji.
Alisema kuwa wanatoa elimu ya madhara ya rushwa ambapo ni kosa kisheria endapo ikitumika
itasababisha kupatikana víongozi ambao siyo wazuri na hawataweza kuongoza wananchi kwa
weledi ambapo kauli mbiu inasema Kuzuia Rushwani Jukumu lako na langu Tutimize wajibu wetu.
Friday, August 16, 2024
MUHARAKANI/MKUZA WAITAKA TARURA KUBORESHA BARABARA YA MTAA HUO
Wednesday, August 14, 2024
SERIKALI YATAKIWA KUWA NA VITUO VYA KULEA VIPAJI VYA WACHEZAJI WA UMISSETA NA UMITASHUMTA ILI KUINUA MICHEZO NCHINI

WANANCHI PWANI WATAKIWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KWENYE DAFTARI LA MPIGAPICHA
WANANCHI Mkoani Pwani wametakiwa kujitokeza kwenye hatua za awali za kujiandikisha au kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) Kibaha Israel Ilunde alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha.Ilunde alisema kuwa Ypc imepeta mradi wa michakato ya uchaguzi (K-VOTE) ambao unawahamasisha uwepo wa vijana kwenye masuala ya umma, elimu ya mpiga kura, uraia, kuwapatia elimu vijana wanaotaka kuwania nafasi za uongozi."Usipojiandikisha hutaruhusiwa kupiga kura na viongozi wabaya huwekwa madarakani na raia wema wasiojitokeza kupiga kura hivyo kuna haja ya wananchi kutumia fursa hiyo ya kujiandikisha au kuboresha taarifa zao mara zoezi hilo litakapofanyika Mkoani Pwani,"alisema Ilunde.Alisema kuwa vijana milioni tano wataandikishwa kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ambapo Tume Huru ya ya Uchaguzi iko kwenye uandikishaji na uboreshaji wa daftari la wapiga kura kwa ajili ya wapiga kura."Tutakuwa tukitoa elimu juu ya elimu ya mpiga kura kwa kushirikiana na mitandao mbalimbali lengo ni kuwahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwani ni haki yao ya msingi ya kuchagua au kuchaguliwa,"alisema Ilunde.Aidha alisema pia elimu hiyo wataitoa ndani na nje ya shule na vyuo ambapo watawahamasisha hata wale ambao walijiandikisha lakini hawapigi kura kwani wasipopiga kura watachaguliwa viongozi ambao watawaamulia na watu wengine."Ushiriki wa vijana kwa mwaka 2004 uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2005 vijana walikuwa ni asilimia nane na uchaguzi wa 2015 waliongezeka na kufikia asilimia 50 na tunatarajia mwaka huu na mwakani wataongezeka,"alisema Ilunde.Aliongeza kuwa vijana hao waligombea nafasi mbalimbali kuanzia serikali za mitaa, udiwani na ubunge na baadhi walichaguliwa kuwa Manaibu Mawaziri wakiwemo Dk Zainab Katimba, Salome Makamba ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum."Vijana wapambane kugombea nafasi husika lakini wasinunue kura kwani zinavunja heshima ya nchi na zinaliaibisha taifa kwani wakiingia kwa njia hiyo uongozi wao utakuwa wa kulipa madeni hivyo wafanye siasa safi za heshima na siyo za matusi,"alisema Ilunde.Aliwataka watoe hoja kwa kuweka utu mbele kwa kuijali jamii na wajue kuwa kuna kushinda na kushindwa na wakubali matokeo kwa kutokufanya fujo ambapo TAMISEMI na Tume Huru ya Uchaguzi watasimamia vyema vyema uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.
Tuesday, August 13, 2024
WIZARA YA MAJI IMEJIPANGA MABWAWA YA MAJI NA TOPE SUMU YANAKIDHI VIGEZO.
Na Wellu Mtaki, Dodoma
Wizara ya Maji kupitia Idara ya Rasilimali za Maji ina jukumu la kuhakikisha mabwawa ya maji na tope sumu yanakidhi vigezo vya usalama wa mabwawa kwa mujibu wa Sheria ya Rasilimali za Maji ili kuepusha madhara yatakayojitokeza katika jamii.
Hayo yamesemwa leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Maji uliopo Mtumba Jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri, amesema Wizara ya Maji imeandaa mafunzo ya siku mbili katika kuhakikisha usalama wa mabwawa ya maji na tope sumu unaimarishwa.
Aidha Mhandisi Waziri amesema kuwa mafunzo yatahusisha watalaam kutoka wamiliki wa migodi kwa ajili ya usalama wa mabwawa ya tope sumu, wamiliki wa mabwawa makubwa ya maji, wataalam wa mabwawa waliosajiliwa na wataalam kutoka Serikalini.
Sambamba na hayo Mhandisi Waziri ameongeza kuwa mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na Tanzania Chamber of Mines na yatafanyika mkoani Mwanza .
TAKUKURU PWANI YAOKOA BILIONI 1.6
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 1.6 kutoka vyanzo mbalimbali vya Halmashauri ya Mji Kibaha.
Hayo yamesemwa na Naibu Kamanda wa Takukuru Mkoa huo Ally Haji wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha juu ya kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu.
Haji amesema kuwa walibaini hayo wakati wa ufuatiliaji wa ukusanyaji wa ushuru wa huduma kama mbalimbali kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili kwa kushindwa kuwajibika.
"Katika ufuatiliaji tuligundua kuwa baadhi ya watumishi wa Halmashauri kwenye kitengo cha ukusanyaji wa mapato watumishi kushindwa kufuata sheria, kanuni, na taratibu za ukusanyaji na kufanikiwa kukusanya shilingi bilioni 1.6 zilizokuwa zinapotea,"amesema Haji.