WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho ya wakulima nane nane Kanda ya Mashariki Mkoani Morogoro Agosti Mosi mwaka huu.
Saturday, July 29, 2023
PINDA KUZINDUA MAONYESHO NANE NANE KANDA YA MASHARIKI
Friday, July 28, 2023
WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA MGENI RASMI NANE NANE KANDA YA MASHARIKI
TASAC KUNUNUA BOTI ZA UOKOZI ZIWA VICTORIA
SHIRIKA la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema limejipanga kununua boti tatu za uokozi katika Ziwa Victoria ambazo zitakwenda kusaidia kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza pindi ajali zinapotokea
Hayo yamesemwa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Bw.Kaimu Abdi Mkenyenge wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka wa fedha 2023/2024 .
Amesema katika boti hizo tatu zitakazonunuliwa mbili zitakuwa ni za mwendonkasi kwaajili ya ukokozi na Moja itakuwa kwaajili ya kubebea majeruhi na wagonjwa (Ambulance) .
“Boti hizi tatu zitatumika kufanya uokozi katika ajali ambazo zimekuwa zikitokea katika Ziwa Victoria ambapo mbili zitakuwa ni za meendo kasi na Moja itatumika kama ambulance kwa ajili ya majeruhi”amesema
Aidha amesema TASAC imeendelea kuimarisha udhibiti huduma za usafiri majini, na kuhakikisha kuna ushindani sawia miongoni mwa watoa huduma.
Amesema kuwa linafanya ufuatiliaji, tathmini na kutoa maelekezo kuhusu utekelezaji wa vigezo na viwango vya ubora wa huduma (performance standards and Benchmarks) kwa watoa huduma za bandari na usafiri majini.
“Tunaendelea kuratibu maombi ya tozo za usafiri wa meli katika Maziwa (Victoria na Nyasa) na kuhakikisha viwango vya tozo vinavyotumika haviathiri ushindani wa kibiashara;
“Lakini pia zoezi la urasimishaji wa bandari bubu Tanzania bara ambapo bandari bubu kumi na tatu (13) zilizowasilishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa ajili ya urasimishaji zilikaguliwa na kufanyiwa tathmini ya kina kwa kushirikiana na TPA, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)”amesema Mkeyenge
Kadhalika amesema bandari bubu kumi zilionekana kukidhi vigezo hivyo na kupendekezwa kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) (WUU-U) kwa ajili ya kurasimishwa kwa mujibu wa sheria
“waendeshaji wa zilizokuwa bandari bubu binafsi tano (05) za Mwanza ambazo ni miongoni mwa zilizokuwa bandari bubu ishirini (20) zilizorasimishwa kupitia Tangazo la Serikali (GN) namba 293/2022 wamepewa leseni za uendeshaji huku TPA wakielekezwa kusimamia kwa karibu bandari kumi na tano (15) zilizobakia.
Akizungumzia kuhusu Kuboresha usalama, ulinzi kwa usafiri majini na kudhibiti uchafuzi wa mazingira baharini utokanao na meli amesema Shirika limetimiza lengo hilo la kimkakati kwa kuendelea kusimamia usalama wa vyombo vya usafiri majini kwa kufanya ukaguzi wa meli kubwa na vyombo vidogo vya majini.
“Shirika lilifanya kaguzi za usalama kwa meli kubwa zibebazo tani 50 au zaidi ili kuhakikisha kuwa ni salama na zinaendeshwa na mabaharia wenye sifa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kagera, Kigoma na Mbeya ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni, 2023, Shirika lilifanya jumla ya kaguzi za meli kubwa 288 ambapo kaguzi 165 zilikuwa za meli za kigeni na kaguzi 123 zilikuwa meli za ndani.”amesema
Kuhusu uratibu Shughuli za Utafutaji na Uokoaji Majini amesema Kituo cha Utafutaji na Uokoaji Majini kilichopo Dar es Salaam kinachoratibiwa na TASAC kiliendelea kufanya shughuli zake katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Juni, 2023 ambapo kituo kilipokea taarifa 4 za ajali zilizohusisha vyombo vya majini ambazo zilitokea katika eneo la maji ya Tanzania.
Katika ajali hizo jumla ya watu 61 walihusika ambapo watu 58 sawa na 95% waliokolewa na watu 3 sawa na 5% walipoteza maisha.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa amesema Serikali inataka kushirikiana na sekta binafsi kuendesha Bandari, mikataba nwatakaoendesha bado haijasainiwa.
“Sasa hivi ndio wataalamu wako mezani kuzungumza kuhusu mikataba, muda na gharama lakini hakuna bandari iliyouzwa, wataalamu watakapokamilisha majadiliano tutaangalia maslahi yetu yako wapi na maoni yanayotolewa na Watanzania yatazingatia Serikali iko macho wakati wote kuhakikisha maslahi ya Watanzania yanalindwa”amesema Msigwa.
Thursday, July 27, 2023
MRADI MKUBWA WA KILIMO CHA VANNILA WAZINDULIWA DODOMA UNAKWENDA KUGHARIMU ZAIDI YA BIL 30 ZA KITANZANIA.
Uzinduzi huo umeambatana na utoaji Elimu kwa wananchi wa eneo hilo kuhusu kilimo cha Vanilla ambao umefanyika Julai 22 2023 katika shamba la kitalu (green House)kubwa ya kilimo hicho inayotumia njia za kisasa.
Mkurugenzi Mtendaji na muasisi wa makampuni ya Vanilla international Limited ,Simon Mkondya amesema shamba kitalu lipo kilomita 40 kutoka katikati ya JIJI la Dodoma barabara kuu ya kwenda Arusha lenye ukubwa wa hekta 125.
Mkondya amesema uwekezaji huo unakuja baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia kilimo hicho katika kisiwa cha Zanzibar.
JWT YAVUTIWA UTALII UWEKEZAJI YAWATAKA WAFANYABIASHARA WAKAWEKEZE
KATIKA kuunga mkono jitihihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani imetembelea vivutio vya utalii na kutambua fursa za uwekezaji zilizopo Wilayani Bagamoyo.
JWT WAVUTIWA NA VIVUTIO VYA UTALII NA UWEKEZAJI BAGAMOYO
KATIKA kuunga mkono jitihihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani imetembelea vivutio vya utalii na kutambua fursa za uwekezaji zilizopo Wilayani Bagamoyo.
Wednesday, July 26, 2023
KATIKA kuhakikisha wafanyabiashara wanaondokana na changamoto mbalimbali Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) imejipanga kuhakikisha inakabili kero na kuzifikisha sehemu husika.