JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kujiunga na Jeshi kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne hadi shahada ya uzamili ambao wamemaliza mkataba wa miaka miwili wa mafunzo ya kujitolea katika Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na kurudishwa majumbani.
Thursday, March 9, 2023
JWTZ WATANGAZA NAFASI KUJIUNGA NA JESHI
KIKWETE AOMBA USHIRIKIANO KUTIMIZA LENGO LA RAIS KUWA NA MUUNDO WA UTUMISHI KWA USTAWI WA TAIFA
MHE. RIDHIWANI KIKWETE AOMBA USHIRIKIANO KUTIMIZA LENGO LA MHE. RAIS LA KUWA NA SERA ZA KIUTUMISHI NA MIUNDO YENYE TIJA KWA USTAWI WA TAIFA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Uendelezaji Taasisi kumpa ushirikiano wa kutosha kwenye eneo la kusimamia uendelezaji wa sera katika Utumishi wa Umma na miundo ya Taasisi za Umma.
Mhe. Kikwete ametoa rai hiyo Jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Usimamizi wa Taasisi kwa nyakati tofauti kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na Idara hizo pamoja na kuhimiza uwajibikaji.
Amesema kuwa ili aweze kumsaidia vema Waziri mwenye dhamana kufikia lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwa na sera za utumishi wa umma zenye tija na miundo inayotekelezeka kiutendaji kwa ustawi wa taifa.
Mhe. Kikwete amesema ameteuliwa na Mhe. Rais kumsaidia Waziri mwenye dhamana ya kusimamia utumishi wa umma na utawala bora, hivyo hana budi kufahamu kwa kina majukumu yanayotekelezwa na idara hizo ili aweze kuyazungumzia pale yanapohitaji ufafanuzi na uelewa kwa umma.
“Malengo ya kukutana nanyi leo ni kufahamiana na kujua majukumu yenu kwa kina kwa kuwa mimi nina jukumu la kumsaidia Mhe. Waziri kujibu maswali ya kiutumishi na utawala bora yanayoulizwa Bungeni,” Mhe. Kikwete amesisitiza.
Ameongeza kuwa, anatamani kujua kila kitu kinachofanyika katika idara hizo pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji kwani kwa kufanya hivyo atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza kwa ufanisi lengo la Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha Kikwete ameitaka Idara ya Undelezaji Sera kuhuisha sera za kiutumishi ili ziendane na wakati na ziweke mazingira rafiki ya kuzihusisha sekta binafsi kutoa mchango katika kuboresha utumishi wa umma kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza.
Wednesday, March 8, 2023
KIKWETE ATAKA USHIRIKIANO KUTIMIZA LENGO LA RAIS DK SAMOA SULUHU HASSAN KUWA NA SERA KWA USTAWI WA TAIFA
MHE. RIDHIWANI KIKWETE AOMBA USHIRIKIANO KUTIMIZA LENGO LA MHE. RAIS LA KUWA NA SERA ZA KIUTUMISHI NA MIUNDO YENYE TIJA KWA USTAWI WA TAIFA
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Uendelezaji Taasisi kumpa ushirikiano wa kutosha kwenye eneo la kusimamia uendelezaji wa sera katika Utumishi wa Umma na miundo ya Taasisi za Umma.
Mhe. Kikwete ametoa rai hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa Idara ya Uendelezaji Sera na Idara ya Usimamizi wa Taasisi kwa nyakati tofauti kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na Idara hizo pamoja na kuhimiza uwajibikaji.
Amesema kuwa ili aweze kumsaidia vema Waziri mwenye dhamana kufikia lengo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwa na sera za utumishi wa umma zenye tija na miundo inayotekelezeka kiutendaji kwa ustawi wa taifa.
Mhe. Kikwete amesema ameteuliwa na Mhe. Rais kumsaidia Waziri mwenye dhamana ya kusimamia utumishi wa umma na utawala bora, hivyo hana budi kufahamu kwa kina majukumu yanayotekelezwa na idara hizo ili aweze kuyazungumzia pale yanapohitaji ufafanuzi na uelewa kwa umma.
“Malengo ya kukutana nanyi leo ni kufahamiana na kujua majukumu yenu kwa kina kwa kuwa mimi nina jukumu la kumsaidia Mhe. Waziri kujibu maswali ya kiutumishi na utawala bora yanayoulizwa Bungeni,” Mhe. Kikwete amesisitiza.
Ameongeza kuwa, anatamani kujua kila kitu kinachofanyika katika idara hizo pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo kiutendaji kwani kwa kufanya hivyo atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutekeleza kwa ufanisi lengo la Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kutoa huduma bora kwa wananchi.
Aidha, Mhe. Kikwete ameitaka Idara ya Undelezaji Sera kuhuisha sera za kiutumishi ili ziendane na wakati na ziweke mazingira rafiki ya kuzihusisha sekta binafsi kutoa mchango katika kuboresha utumishi wa umma kama Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alivyoelekeza.
TASAC YATOA FURSA SEKTA USAFIRISHAJI MAJINI
SHIRIKA la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) linatoa fursa katika sekta ya usafiri majini kwa kuazisha utaratibu kwa kusajili meli kwa masharti nafuu ukarabati wa ujenzi wa meli na kuazisha maegesho ya boti ndogo katika ukanda wa Pwani, viwanda vya utengenezaji wa maligafi za ujenzi wa boti za plastiki pamoja na kujenga bandari rasmi za uvuvi.
Tuesday, March 7, 2023
OSHA YAPATA MAFANIKIO
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Monday, March 6, 2023
WANAWAKE WATUMIE MITANDAO KUFIKIA USAWA WA KIJINSIA
Na Mwandishi Wetu Dodoma
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Doroth Gwajima amewataka wanawake wahakikishe wanatumia huduma za mitandao ili kufikia usawa wa kijinsia kwenye maendeleo kwa kupata taarifa mbalimbali za kijamii kama Afya, Elimu, Kilimo, biashara na zinginezo.
Gwajima ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika March 8 mwaka huu.
Amesema kuwa pengo la wanawake kumiliki simu na kutumia Mtandao linaongezeka zaidi kwa wanawake wenye umri mkubwa ( wazee) , wanawake wanaoishi vijinini, pamoja na wanawake wenye ulemavu Mwaka 2022 takwimu zinaonesha asilimia 63 ya wanawake duniani walitumia Mtandao ukilinganisha na asilimia 69 ya wanaume.
Aidha amesema kuwa kwa kushirikiana na jamii yenyewe serikali itaendelea kuelimisha na kufanyia kazi kuondoka vikwazo vyote vinavyozuia mwanamke kutumia Teknolojia ya kidigitali.
Pia ametoa wito kwa wanawake na jamii kwa ujumla kujitokeza kuadhimisha sikukuu ya wanawake duniani chini ya uongozi wa waheshimiwa Wakuu wa Mikoa na ameimiza wanawake kujiunga na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yaliyo ngazi zote Hadi vijinini Ili kunufaika na uwezeshaji wa serikali na wadau wake.
Sunday, March 5, 2023
WATATU WAFA AJALINI WAMO ASKARI POLISI WAWILI
WATU watatu wakiwemo askari wawili wa Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa Pwani wamefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo alisema kuwa watu hao walifariki papo hapo.
Lutumo alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo Machi 5 mwaka huu majira ya saa 11:45 alfajiri huko maeneo ya Mavi ya Ng'ombe Kijiji cha Mboga Kata ya Msoga Tarafa ya Chalinze katika Barabara ya Chalinze/Segera.
"Gari lenye namba za usajili T 323 BAL aina ya Toyota Cresta likiendeshwa na mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28) askari wa kituo cha Polisi Chalinze akitokea Chalinze kuelekea Lugoba liliacha njia kutoka upande wa kushoto wa barabara na kwenda upande wa kulia na kugonga kalavati kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu watatu na mmoja kujeruhiwa,"alisema Lutumo.
Aliwataja askari waliokufa kuwa ni Mkaguzi msaidizi wa Polisi Ndwanga Dastani (28) aliyekuwa dereva wa gari hilo, Konstebo Emmiliana Charles (26) wote askari wa kituo cha Polisi Chalinze na Karimu Simba (27) ambaye ni karani wa Mahakama ya Wilaya Lugoba.
"Majeruhi huyo ambaye naye ni askari wa Kituo cha Polisi Chalinze Konstebo Mwanaidi Shabani (25) ameumia maeneo mbalimbali ya mwili wake na amepelekwa katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi,"alisema Lutumo.
Aidha alisema kuwa uchunguzi wa awali umeweza kubaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi na dereva kushindwa kulimudu gari na kupinduka.
"Miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Lugoba kwa ajili ya kusubiri taratibu za mazishi,"alisema Lutumo.