WAZIRI wa Nchi Ofisi Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Seleman Jafo amefika ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kwenda kumsalimia Mkuu mpya wa Wilaya hiyo Petro Magoti.
Waziri Jafo alikwenda kumtembelea mkuu huyo mpya wa Wilaya ikiwa imepita siku moja tu baada ya kuapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge.
Waziri Jafo amesema kwamba ameamua kwenda kumtembelea mkuu huyo kwa lengo la kuweza kumpongeza kwa dhati baada ya kuteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenda kuwaongoza wananchi wa Kisarawe.
Jafo amesema kwamba ana mfahamu Magoti kwa muda mrefu kutoka na kuwa mchapakazi hodari na anatekeleza majukumu yake ipasavyo kwa maslahi ya wananchi.
"Kitu kikubwa nimekuja katika ofisi za Mkuu wa Wilaya lakini lengo kubwa ni kubadilisha mawazo katika Wilaya yetu ya Kisarawe na mimi nampongeza sana Magoti kwa kuletwa hapa,"amesema Waziri Jafo.
Pia Waziri Jafo alimshukuru kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Magoti nakumleta Kisarawe kwa lengo la kuwatumikia wananchi.
Sambamba na hilo Jaffo hakusita kumpa pongezi mkuu huyo wa Wilaya kwa kuchapa kazi kwa bidii zaidi kwani wanafahamiana tangu alipokuwa Waziri wa TAMISEMI waliweza i kufanya kazi kwa ushirikiano wa hali na mali.
Kwa upande wake Mkuu huyo wa Wilaya Petro Magoti amemwahidi waziri Jafo kumpa ushirikiano wa karibu zaidi lengo ikiwa ni kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.
No comments:
Post a Comment