Ndugu Omary Abdul Punzi Afisa Mahusino wa Mradi wa Mazingira wa RAMATA (Rafiki wa Mazingira Tanzania) kutoka GBCF nchini Tanzania Tarehe 1.6.2024 awafunda wakina mama wa UWT tawi la Ndumbwi Mbezi Juu Kata ya Mbezi juu Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Ndugu Omary Punzi aliwaelekeza kuwa Taifa hili limejengwa katika Misingi ya Kizalendo na walioitengeneza hii nchi ni wakina mama mfano Mwenyekiti wa kwanza Taifa wa Uwt Sofia Kawawa na Mwanasiasa Mashuhuri Bibi Titi Mohammed aliyejitoa kuchangia Mchango wake katika nchi hii.
Aliwaomba wanawake wamuunge mkono Mhe Dr Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta ya kutunza Mazingira na sekta nyingine za Kiuchumi.
Kwa kuzifuata hizi Falsa za TA TE TI TO TU
TA = Tangaza nchi yako bila uoga
TE= Tetea nchi yako bila uoga tusikubali idhalilike
TI= Timiza wajibu wako kwa kila hali
TO= Toa Ushauri kwa hali na Mali
TU= Tubu pale unapokosea
Pia aliwakumbisha sifa kuu ya kiongozi ni Kulalamikiwa na kuwa na Kiherehere chenye Manufaa kwa nchi yake
Naye Wakili msomi Godfrey Kizito Chambi alitoa mada ya Umuhimu wa wanawake katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mtaa wa mwaka 2024 na wasisite kwenda kujiandikisha katika Daftari la kudumu la kupiga kula zoezi hilo la kupata kitambulisho kwa ajili ya uchaguzi litakalo anza tarehe 1.7.2024 alisisitiza kuwa wasijitokeze kupokea au kutoa rushwa katika mchakato wa Uchaguzi utarudisha nyuma na kuwapata wagombea siyo sahihi na aliendelea kuwakumbusha wanawake hao juu ya Umuhimu wa kutunza Mazingira kwa kutumia rasilimali rafiki ili mazingira yetu yawe rafiki alisema shughuli za binadamu zinaongoza kuchochea kuharibu Mazingira.
Kwa upande Rehema Muya Mwenyekiti wa UWT Kata ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Mkutano huo alimwaga sifa kwa Mwenyekiti na katibu wa tawi la ndumbwi kwa kufanya jambo kubwa la kuandaa mada hizo na kuwakusanya Wanawake wa UWT hii inaonesha kuwa sasa CCM inakwenda kupata Ushindi wa Kishindo kwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika uchaguzi wa 2024 na 2025
Naye Mhe Anna lukindo Diwani wa kata ya Mbezi Juu alisema kuwa Serikali Mhe Dk Samia Suluhu Hassani imewasaidia wananchi wa Mbezi Juu kujenga Daraja Mito Miwili lengo kutatua kero ya muda mrefu ya kupita hapo Daraja hilo likikamilika litakuwa chachu ya Maendeleo kutokana na Kasi inayofanywa na Mhe Josephat Gwajima na Timu nzima ya Viongozi wa Kinondoni sambamba na hilo alivutiwa na Mada za mkutano huo.
Katibu wa Tawi la Ndumbwi ndugu Witnes Ngowi alisema kuwa UWT katika Tawi hilo wamejipanga na kuhakikisha kuwa watashinda kwa kishindo katika Uchaguzi wa 2024 na 2025.
Kwa upande wa Catherine Mpangala Mwenyekiti wa Tawi la Ndumbwi alisema wameanda Mkutano huo kwa lengo la kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuwakumbusha watanzania kuwa mwaka 2024 kutakuwa na Uchaguzi wa serikali ya Mitaa hivyo wasisite kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha katia Daftari la Kupiga kula litakalo anza Julai Mosi.
Aliwashukuru Bank ya NMB kuja kutoa Elimu ya Mikopo kwa wakina mama na na watoa mada ya Ujasiliamali kutoka kwa Estar Muhanga ,Mada Itifaki na Uzalendo iliyotolewa na ndugu Omary Punzi na ile mada ya Utunzaji wa Mazingira na Umuhimu wa kushiriki Uchaguzi wa serikali za mita iliyotolewa na wakili Msomi Geoffrey Kizito
Ndugu Catherine aliwawapongeza wanachama wa UWT kufika kwa wingi Sambamba na viongozi wa Chama kutoka Wilaya na kata kuja kushiriki Mkutano huo.
No comments:
Post a Comment