SERIKALI imezitaka Halmashauri nchini kutenga bajeti kwa ajili ya kununua mafuta kinga ya kujipaka watu wenye ualbino ili kuepukana na mionzi ya jua ambayo inawasababishia kansa ya ngozi.
Hayo yalisemwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Deogratius Ndejembi ambapo hotuba yake ilisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya kuongeza uelewa juu ya Ualbino Duniani (IAAD) ambapo kitaifa ilifanyika Kibaha.Ndejembi alisema kuwa serikali inafanya jitihada kubwa kuhakikisha watu wenye ulemavu wakiwemo watu wenye ualbino wanawekewa mazingira mazuri ili kupata huduma muhimu zikiwemo za kiafya."Tunaziagiza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili ya kununulia mafuta hayo (sun screen lotion) ili ziweze kuwasaidia kukabiliana na mionzi ya jua ambayo imekuwa ikiwasababishia kansa ya ngozi,"alisema Ndejembi.Alisema kuwa huduma za afya ni sehemu ya jukumu la serikali kama inavyotoa huduma nyingine na hiyo ni huduma mojawapo kwa wananchi."Pia ni vema kuwapatia vifaa zaidi kuliko fedha pale wanapokuwa wanahitaji vifaa kama vile vyerehani ili waweze kushonea kofia ambazo zinawasaidia kukabiliana na mwanga mkali na jua,"alisema Ndejembi.Aidha alisema kuwa serikali iko makini katika kuangalia ustawi wa watu wenye ulemavu ambapo inawndelea na utaratibu wa kuboresha sheria ya watu wenye ulemavu na inalaani matukio ya kuwafanyia vitendo vya ujatili watu wenye ualbino."Jamii inapaswa kuthamini utu wa mtu na ni jukumu la kila mwananchi na kamati za usalama za mikoa zihakikishe vitendo hivyo vinakomeshwa na wao kwa wao waache migongano na washiriki uchaguzi kwa kuchagua na kuchaguliwa kwani ni haki yao,"alisema Ndejembi.Aliwataka maofisa watendaji kuhakikisha wanafanya utambuzi wa watu wenye ualbino na kuhusu asilimia mbili ya mikopo ya Halmashauri kwa watu wenye ukemavu kwa mtu mmoja mmoja badala ya kukopa kwa vikundi serikali inalifanyia kazi suala hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi, SACP Ralph Meela alisema kuwa wataendelea kusimamia ulinzi na usalama hivyo watu wenye ualbino wasiwe na wasiwasi.Meela alisema kuwa wanafanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa na wakaguzi wa polisi ngazi ya kata zaidi ya 3,000 nchini na kuna makamishna wa polisi jamii kwenye mikoa hivyo kutakuwa na usalama wa kutosha.Kwa upande waka katibu wa Chama Cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) Batha Totei amesema kuwa wanaomba ruzuku kwa vyama vya watu wenye ulemavu na kuondoa gharama za matibabu ya kansa kwa watu wenye ualbino na kuwa na mpango wa bima ya afya.Totei alisema kuwa serikali iweke mpango wa kuwa na kliniki kwenye hospitali za wilaya na kliniki tembezi na kuwashirikisha kwenye mikutano ya kampeni ili waweze kutoa elimu ya kupinga vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino.
No comments:
Post a Comment