Monday, August 4, 2014

WASOMI WATUMIE TAALUMA ZAO KULETA MAENDELEO

Na John Gagarini, Chalinze
WASOMI kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wametakiwa kutumia elimu yao kukabiliana na changamoto za kimaendeleo zilizopo jimboni humo.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze iliyojengwa na na kampuni ya kutengeneza saruji ya Tanga Simenti huku taasisi ya Read International ikiwa imetoa msaada wa vitabu.
Ridhiwani alisema kuwa jimbo hilo lina changamoto nyingi ambazo nyingine zitatatuliwa na wasomi wanaotoka eneo hilo na wengine kwa lengo la kuleta maendeleo.
“Elimu mnayosoma iwe chachu na ya maana kwa kuleta maendeleo ya jimbo hili kwani wazazi wenu wanajitolea kuwasomesha ili baadaye na nyie muweze kuwa msaada kwa jamii na  elimu ya sasa inaendana na vitendo ambavyo ndiyo tafsiri  kwa vile wanavyokuwa wamejifunza wanafunzi na si kuwa wasomi jina ambao hawana msaada kwa jamii inayowazunguka,” alisema Ridhiwani.
Alibainisha kuwa maktaba ambayo tumeizindua leo iwe chanzo cha nyie kujifunza kwa bidii kwa kujisomea baada ya walimu kuwafundisha kwani Watanzania kwa sasa bila ya elimu ni kazi bure na hataweza kufanya jambo lololote la kimaendeleo.
Kwa upande wake kaimu meneja biashra wa kampuni ya Tanga Simenti Yasin Hussein alisema kuwa wamejenga jengo hilo kwa lengo la kuhakikisha shule hiyo inakabiliana na tatizo la ukosefu wa maktaba ambapo hutoa asilimia moja ya faida ya mapato wanayopata kwa kurudisha kwa jamii kwa kusaidia masuala mbalimbali yakiwemo ya mazingira, elimu na afya.
“Tumetumia kiasi cha shilingi milioni 47 kwa ajili ya ujenzi huu ambapo mpango ni kujenga maktaba kwenye shule za Mingoyo Lindi na Kinyerezi Jijini Dar es Salaam na watatumia zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa maabara na maktaba kwenye mikoa mbalimbali nchini,” alisema Hussein.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo Emanuel Kahabi alisema kuwa ufunguzi wa maktaba hiyo utasaidia kukabiliana na changamoto ya maktaba ailiyokuwa inakabili shule yao ambayo ina wanafunzi 879.
Mwisho.

Picha no 1397 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani akiongea wakati wa ufunguzi wa makataba ya shule ya sekondari ya Chalinze kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya shule Mbwana Madeni na kulia ni mkuu wa polisi wilaya ya Chalinze Janeth Magori.

picha no 1389 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka alama kwenye ukuta kama alama ya kumbukumbu baada ya kuizindua makta ya shule ya sekondari ya Chalinze.

picha no 1369 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa Chalinze Riidhiwani Kikwete maara baada ya kuzindua maktaba ya shule hiyo.

picha no 1391 Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya Chalinze kushoto Mbwana Madeni akiongea katikakati ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na katikati mkuu wa polisi kanda maalumu wilaya ya Chalinze Janeth Magori.

picha no 1371 wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa maktaba ya shule.

 

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani akiongea wakati wa ufunguzi wa makataba ya shule ya sekondari ya Chalinze kushoto ni mwenyekiti wa bodi ya shule Mbwana Madeni na kulia ni mkuu wa polisi wilaya ya Chalinze Janeth Magori.
 


Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiweka alama kwenye ukuta kama alama ya kumbukumbu baada ya kuizindua makta ya shule ya sekondari ya Chalinze.
 

 

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa Chalinze Riidhiwani Kikwete maara baada ya kuzindua maktaba ya shule hiyo.



Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari ya Chalinze kushoto Mbwana Madeni akiongea katikakati ni Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete na katikati mkuu wa polisi kanda maalumu wilaya ya Chalinze Janeth Magori.
 

 

picha no 1371 wanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Ridhiwani Kikwete wakati wa uzinduzi wa maktaba ya shule.

No comments:

Post a Comment