Na John Gagarini, Kibaha
DEREVA wa Texi wa Maili Moja Richard Ponera (36) mkazi wa
Mwendapole wilayani Kibaha mkoani Pwani amepotea katika mazingira ya
kutatanisha baada ya kukodishwa na watu wasiofahamika.
Ponera alikodishwa na watu wawili ambao hawakufahamika Agosti 5 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku akiwa
anaendesha gari lenye usajili na T 905 BHT aina ya Corolla nyeupe.
Akizungumza na mjini Kibaha kuhusina na tukio hilo katibu wa
Umoja wa madereva Texi Kibaha Mjini (KITAGURO) Fadhil Kiroga alisema kuwa
dereva huyo tangu alipoondoka siku hiyo hadi leo hakurudi na hakuna taarifa
yoyote iliyopatikana juu yake.
Kiroga alisema kuwa siku ya tukio hilo Ponera alionekana
akipatana na watu hao kwa muda kidogo kama dakika 10 hivi kisha akaondoka na
watu hao ambao walikuwa wawili.
“Baada ya mapatano licha ya kuwa madereva wengine hawakuweza
kujua walichokuwa wakiongea na Ponera waliondoka na alipofika Mlandizi
aliwasiliana na mwenzetu ambaye ni Salum Mbawala na kumwambia kuwa kwa sasa
yuko Mlandizi,” alisema Kiroga.
Alisema kuwa baada ya hapo simu yake haikuweza kupatikana
tena kwani baada ya kuona harudi wenzake walijaribu kumpigia lakini simu yake
haikupatikana tena.
“Ponera hapa alikuwa hana muda mrefu tangu aanze kazi na
alipata gari hilo ambalo alikuwa amekabidhiwa kama wiki mbili zilizopita na
gari lenyewe halikuwa kwenye hali nzuri sana kusema labda ilikuwa ni kishawishi
cha watu labda kutaka kuliiba gari hilo, hatujui kilichomtokea mwenzetu,”
alisema Kiroga.
Aidha alisema kuwa wamefanya jitihada mbalimbali ambapo
walikwenda polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo na kupewa namba KMM/RB/847/2014
pia walitoa taarifa kwenye vituo vya Mlandizi na Tumbi kisha kutembelea maeneo
ya Yombo, Miswe na Mzenga bila ya mafanikio.
Kwa uapande wake mke wa dereva huyo Rosemary Urasa (31) alisema
kuwa siku ya tukio hilo alikuja naye hadi Maili Moja yeye akenda sokoni kununua
vitu vya nyumbani akamwacha stendi kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake kama
kawaida.
“Nakumbuka majira ya saa 5 asubuhi nilimpigia simu baada ya
gari linguine ambalo liko hapa nyumbani lilikuwa linapiga honi lenyewe
nikamwambia aje alizime lakini kwa bahati nzuri kuna mtu alifanikiwa kulizima
nikamjulisha alikuwa njiani kuja lakini akarudia eneo linaloitwa Picha ya
Ndege, toka hapo kila nikipiga simu simpati,” alisema Urasa.
Alibainisha kuwa mumewe ambaye wamezaa naye watoto wawili
walihamia Kibaha baada ya kufanikiwa kujenga na kuzaa watoto wawili ambao ni
Ruben (14) anayesoma kidato cha kwanza St Anne na Kontrada anayesoma darasa la
sita shule ya Msingi Jitegemee.
Aidha alisema kuwa wakati mwingine mumewe hufanya kazi na
kukesha hivyo siku hiyo usiku alijua kuwa atakesha lakini ilipofika asubuhi
alishangaa kutokumwona kwani endapo anakuwa amekesha asubuhi ni lazima arudi
lakini siku hiyo hakumwona ikambidi aje kwenye eneo analopaki lakini alipouliza
wakasema tangu alivyoondoka jana hajaonekana tena.
Naye mmiliki wa gari hilo Athuman Kimia alisema kuwa siku
hiyo ya tukio aliwasiliana na Ponera ambapo kulikuwa na tatizo la kulipia gari
linapokuwa barabarani na kumpa 170,000 kwa ajili ya kulipia.
Kimia alisema kuwa baada ya kama saa moja alimpigia na
kumwambia kila kitu kashalipia hivyo mambo mazuri na ndipo alipoendelea na
shughuli kama kawaida.
“Tumekubaliana kila baada ya wiki awe ananipa malipo ya kazi
lakini nilipigiwa simu kuambiwa kuwa Ponera aonekani na nilipojaribu kumpigia
simu yake haipatikani sijui kilichomtokea ninini kwani yeye huwa ananipigia
endapo kumetokea tatizo kwani sasa hivi ni wiki ya pili tangu nimkabidhi gari ,”
alisema Kimia.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment