Na John Gagarini, Kibaha
IMEELEZWA kuwa utendaji kazi wa
mazoea umesababisha Taifa kushindwa kusonga mbele katika kuwaletea
maendeleo wananchi kutokana na utendaji wa mazoea wa baadhi ya viongozi
na wafanyakazi.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Alafayo Kidata naibu katibu mkuu Tawala
za Mikoa Serikali za Mitaa (TAMISEMI), alipokuwa akizungumza na viongozi
wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) baada ya ziara aliyoifanya
kulitembelea Shirika hilo la Umma.
Kidata alisema kuwa baadhi ya watendaji kazi hasa kwenye mashirika na
taasisi za serikali wamekuwa hawafanyi kazi ipasavyo na kufanya kazi kwa
mazoea hali ambayo imekuwa haileti tija kwa maendeleo ya nchi.
"Tunapaswa kubadilika kama kweli tunataka kuleta mabadiliko ndani ya
nchi yetu hatuwezi kufanya kazi kwa mazoea tu lazima kuwe na uwajibikaji
vinginevyo tutazidi kulididimiza Taifa," alisema Kidata.
Alisema kuwa kwa upande wa mashirika ya Umma uzalishaji wake umekuwa
ukishuka siku hadi siku kutokana na kutowajibika ipasavyo tofauti na
mashirika binafsi ambayo yako makini katika utendaji kazi wake.
"Mashirika na taasisi binafsi zimekuwa zikifanikiw akutokana na kuwa
makini katika utendaji kazi lakini kwa mashirika na taasisi za serikali
hali imekuwa kinyume hii yote ni kutokana na watu kutowajibika
ipasavyo," alisema Kidata.
Aidha alisema kwenye taasisi za Umma mfanyakazi anaweza kukaa mwezi
mzima hajafanya kazi lakini mshahara unaingia kupitia ATM lakini hakuna
mtu anayehoji je uwajibikaji hapo utakuwepo.
"Lazima wafanyakazi wa wajibike ipasavyo na kufanya kazi kama anavyoweza kuwajibika kwenye shughuli yake binafsi na uzalishaji wa kiwango kikubwa ndiyo utakaowaondoa kwenye matatizo mliyonayo hasa ya madeni," alisema Kidata.
Naye mkurugenzi wa KEC Dkt Cyprian Mpemba alisema kuwa changamoto kubw
ailiyopo kwenye shirika hilo ni ukosefu wa fedha na madeni makubwa ya
watumishi na watoa huduma katika shirika hilo ambalo lilianzishwa miaka
ya 70.
mwisho.
No comments:
Post a Comment