Na
John Gagarini, Kibaha
MKAZI
wa Mtaa wa Kwa Mfipa wilayani Kibaha Nuru Rashid amewashangaza wakazi wa mtaa
huo kwa kushindwa kumpeleka hospitali mwanae mwenye umri wa miaka miwili na
nusu baada ya kuungua na maji ya moto.
Akizungumza
na baba mzazi Ally Said alisema mwanae ambaye ni wa jinsi ya kiume ameungua kifuani
na kusababisha kidonda kikubwa hadi kwenye mkono wake wa kushoto hakumpatia
matibabu yoyote hadi siku iliyofuata.
Said
alisema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 27 mtaani hapo nyumbani kwa mama
yake mazazi ambaye walitengana naye zaidi ya mwaka mmoja uliopita ambapo
aliolewa na mume mwingine.
“Mimi
baada ya kupata habari juu ya mwanangu kuunguzwa na maji siku iliyofuata
nilikwenda nyumbani kwake kutaka kumchukua mwanangu ili nimpeleke hospitali
lakini alikataa na kusema hadi baba yake wa kambo aje jambo ambalo alilikataa
na kumchukua kwa nguvu,” alisema Said.
Alisema
kuwa mkewe amekuwa akimficha juu ya matatizo hasa pale anapoumwa na mbaya ni
pale alipomficha mwanae baada ya kuungua na kushangaa ni kwanini hataki
kumpeleka hospitalini.
Jitihada
za kumpata mama huyo yazikuweza kuzaa matunda licha ya mwandishi kufika
nyumbani kwake na kuambiwa kaenda dukani na hata aliposubiriwa hakuweza kutokea.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtaa huo Hai Hai alikiri kupata tukio hilo na kusema
kuwa ukweli halisi alikuwa nao mama huyo ambaye ndiye aliyekuwa akiishi na mtoto
huyo ambaye alikuwa akilia kutokana na maumivu makali aliyoyapata.
Hai
alisema kuwa hatua aliyoichukua ni kuandika barua ambayo ilibidi ipelekwe
polisi kwa ajili ya taratibu za kisheria na kupatiwa matibabu kwa mtoto huyo na
kusema hicho ni kitendo cha unyanyasaji na kuwanyima haki watoto wadogo.
Mwisho.
Mtoto aliyeunguzwa na maji ya moto akiwa amepumzika huku nyumbani kwao huko Kwa Mfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani (Picha na John Gagarini) |
No comments:
Post a Comment