Tuesday, January 13, 2026
BAGAMOYO SUGAR BINGWA PWANI
BINGWA
Bagamoyo Sugar wametwaa ubingwa kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya fainali ya kwanza kushinda kwa kupata ushindi wa goli 1-0.
Monday, January 12, 2026
BAGAMOYO SUGAR MABINGWA DARAJA LA TATU MKOA WA PWANI
Bagamoyo Sugar wametwaa ubingwa kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya fainali ya kwanza kushinda kwa kupata ushindi wa goli 1-0.
Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Mwendapole Wilaya ya Kibaha ulikuwa mkali na kuvutia mashabiki wengi wa Kibaha na Viunga vyake.
Kwa matokeo hayo timu ya Bagamoyo Sugar watawakilisha Mkoa wa Pwani kwenye mashindano ya mabingwa wa mikoa.
Akikabidhi kombe kwa washindi mgeni rasmi wa mchezo huo huo Fidha Helmud (Tyson) ambaye ni Rais wa timu ya Barberian inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza alizipongeza timu hizo kwa kuonyesha ufundi mkubwa wa kusakata kabumbu.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) Robert Munisi amesema kuwa kufuatia kuwa mabingwa wa Mkoa huo watahakikisha wanaiunga mkono kwenye mashindano yanayofuata.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mabingwa wapya wa Mkoa wa Pwani Bagamoyo Sugar amesema kuwa kwa kushirikiana na Chama Cha Soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA) Kelvin Mawata amesema kuwa lengo ni kuhakikisha timu hiyo inafika mbali kwa kufanya vizuri.
Mwenyekiti wa Kiduli Fc Ally Masimike amesema kuwa amekubaliana na matokeo hayo ambapo timu hiyo itarudi kambini kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali.
BAGAMOYO SUGAR YATWAA UBINGWA MKOA WA PWANI
BARBERIAN YAICHAPA TMA
Tuesday, January 6, 2026
KIDULI FC YAJIPANGA KUPINDUA MATOKEO ILI KUTWAA UBINGWA WA MKOA WA PWANI
Kiduli inatarajia kucheza mchezo wa marudiano Januari 12 kwenye uwanja wa Mwendapole na mshindi wa jumla ndiye atakayekuwa bingwa wa ligi daraja la Tatu mkoa wa Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa timu hiyo Ally Masimike amesema wamepoteza mchezo huo kwa bahati mbaya.
Masimike amesema kuwa watarudi kwenye uwanja wa mazoezi na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao wa kwanza.
"Lengo letu ni kupambana na kuhakikisha tunashinda ili kuwa mabingwa na kuuwakilisha Mkoa wetu kwenye michuano ya Mabingwa wa Mikoa,"amesema Masimike.
Bagamoyo Sugar iliifunga Kiduli Fc kwa goli 1-0 kwenye mchezo wa fainali ya kwanza kwenye uwanja wa Mwendapole Kibaha huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa kwenye uwanja huo huo ikiwa ni fainali ya pili ili kupata bingwa wa Mkoa.
Mbilinyi amewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kwenye fainali hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza.
Bingwa wa ligi hiyo atapata kombe na atawakilisha Mkoa wa Pwani kwenye mashindano ya ligi ya Mabingwa wa mikoa.







