JUMUIYA ya Wazazi Mkoa wa Pwani imeadhimisha miaka 49 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kufanya matendo ya huruma kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Yahaya Mtonda amesema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuisaidia jamii kwani ni moja ya majukumu ya Jumuiya hiyo wakati wa maadhimisho hayo Kimkoa ambayo yamefanyika kwenye Kata ya Tangini.
Kwenye tukio la kwanza Jumuiya hiyo imetoa vifaa mbalimbali kwa wagonjwa kwenye ya Tangini ambayo hata hivyo iko kwenye hatua za mwisho kukamilika ambapo vifaa hivyo vitapelekwa kwenye Hospitali zilizopo kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.
Tukio la pili ni la upandaji wa Miti kwenye Shule mpya ya Msingi Tangini ambapo shule hiyo ni mpya ambayo imeanzishwa mwaka huu ikiwa na wanafunzi 650.
Katika tukio la tatu ilitoa fedha kiasi cha shilingi 80,000 kwa familia ya Catherine Januari ina mtoto mwenye ulemavu Catherine John (12) ambaye hawezi kukaa wala kutembea au kufanya chochote zaidi ya kulala tu.
Tukio la tatu ilitoa fedha kiasi cha shilingi 80,000 kwa Mzee Burhan Rehani ambaye ni mlemavu wa miguu wote ni wa kwenye Mtaa wa Tangini Kata ya Tangini.
Mtonda amesema kuwa aliguswa alipotembelea Kata hiyo na kuahidi kusaidia pale atakapoguswa ambapo alitoa 150,000 na mdau mwingine akaongezea 30,000 ili kusaidia familia hizo zenye uhitaji.
"Tumeamua kufanya hivi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 49 ya CCM ambapo Kimkoa yamefanyika kwenye Kata ya Tangini ambapo ni sehemu ya maadhinisho hayo,"amesema Mtonda.
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Yusufu Masombola amesema kuwa matukio hayo yanaonyesha jinsi gani chama kinavyoshirikiana na jamii.
Masombola amesema kuwa matukio hayo ni sehemu ya maadhimisho ya chama kutimiza miaka 49 tangu kuanzishwa kwake ambapo matukio mbalimbali yamefanyika.
Amesema kuwa Jumuiya hiyo ihakikishe inafundisha maadili mema kwa watoto na vijana ili wawe na maadili mazuri na kuachana na tabia mbaya zisizofaa.
Naye Mwenyekiti wa CCM na Diwani wa Kata ya Tangini Antony Milao amesema kuwa anaishukuru serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia miradi ya maendeleo ndani ya Kata hiyo.
Milao amesema kuwa miradi hiyo muhimu ikiwa ni pamoja na Zahanati Shule ya Msingi na Sekondari itakabili changamoto ya wakazi wa Kata hiyo kupata huduma mbali.

No comments:
Post a Comment