Manara alitoa ahadi hiyo kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mtongani Mlandizi Kibaha wakati akizindua michuano hiyo ambayo itashirikisha timu 104 kutoka kwenye Kata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha yakiwa na lengo la kuhamasisha wananchi wakiwemo vijana kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Alisema kuwa amevutiwa na vijana kuandaa mashindano kama hayo ambayo yanaunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuchangia kwenye michezo kwani ni sehemu ya kuleta maendeleo nchini.
“Kutokana na kitu kizuri mlichokiandaa nitaunga mkono na nitawapatia kiasi cha shilingi milioni 1 ili mfanikishe mashindano haya yafanyike kwa ufanisi mkubwa na kufikisha vizuri ujumbe wa vijana kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura litakalofanyika Februari na kushiriki uchaguzi mkuu,”alisema Manara.
Kwa upande wake katibu wa hamasa wa UVCCM Godfrey Mwafulilwa alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa watu kuboresha taarifa zao.
Kwa kila kata watacheza hatua na kupata timu na kuingia hatua ya 16 bora ngazi Wilaya zawadi ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya guta la matairi matatu, mshindi wa pili atajinyakulia pikipiki na mshindi wa tatu atapata kiasi cha shilingi milioni 1.
Mwafulilwa alisema kuwa kwenye mashindano hayo hakutakuwa na kiingilio na kila timu itapatiwa jezi na mipira miwili huku zawadi nyingine ni mchezaji bora kipa mfungaji kila mmoja atapata ngao na shilingi 50,000 na timu yenye nidhamu shilingi 100,000.
Naye mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Pwani COREFA Robert Munis alisema kuwa malengo yao ni kuhakikisha mpira Pwani unachezwa kwa kuzingatia taratibu na watashirikiana na wadau wanaoandaa mashindano mbalimbali lengo likiwa ni kuhakikisha vijana wanakuza vipaji vyao kwani soka ni ajira.
Munis alisema kuwa anawapongeza wadau hao kwa kuandaa mashindano hayo ambayo ni makubwa kwenye mkoa huo ambapo makubwa zidi ni yale yaliyoandaliwa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ambaye pia Mbunge wa Mafia.
Baadhi ya viongozi wa timu hizo waliwashukuru waandaaji wa mashindano hayo timu za Kujiandikisha na timu oresha taarifa zilitoka sare ya bao 1-1.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment