Hali hiyo inatokana na mfumo dume ambao unamkandamiza mwanamke asiweze kupaza sauti kupitia kwenye nafasi ya uongozi hata hivyo hali hiyo ya mfumo dume kadiri miaka inavyokwenda mbele changamoto hiyo inapungua licha ya kwamba bado haijaisha ndani ya jamii.
Licha ya kuwa mjane na kukumbana na changamoto za kunyanyaswa kijinisa na baadhi ya wagombea na wapiga kura lakini haikumkatisha tamaa, licha ya kwamba maneno aliyokuwa akikashifiwa nayo yalimuumiza sana lakini alivumilia.Huyo siyo mwingine bali ni mwenyekiti wa mtaa wa Bamba Halmashauri ya Mji Kibaha Mkoani Pwani Mboni Mkomwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye alishinda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2024 ambapo alishinda akiwa ni mgombea pekee kwani hakukuwa na mgombea kutoka vyama vya upinzani.
Mboni alisema kuwa alipata kashfa sana wakati wanaendelea na kampeni ndani ya chama ilifika wakati alitaka hata kujitoa kwenye uchaguzi sababu hakuwahi kupata kashfa kama hizo kwa kama mtu hana moyo anaweza kujitoa ili aepukanane na kashfa kwa kweli uchaguzi una mambo mengi sana ya kukatisha tamaa kuwa mwanamke hawezi kuongoza na mtaa haujawahi kuongozwa na mwanamke hivyo awaachie wanaume.
“Nilishangaa kuona hata baadhi ya wagombea wenzangu wanaume walikuwa wakinitolea maneno ya kashfa lakini nashukuru wananchi hawakujali kashfa hizo lakini walinipa kura za kutosha na kuwashinda wanaumewawili na sisi wanawake tulikuwa wawili ambao tulikuwa tunashindana nao,”alisema Mkomwa.
Kwenye uchaguzi huo wa ndani ya chama Mkomwa alipata kura 269 aliyemfuatia alikuwa mwanaume aliyepata kura 171 huku mwanamke mwenzake akipata kura 93 na kumfanya apate nafasi ya kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi wa serikali ya mtaa huo na yeye kuwa mshindi.
“Suala la rushwa ikiwemo ya ngonio kipindi cha uchaguzi ipo lakini mimi nilifanya kampeni bila ya kutoa fedha niliwaambia wanichague niwaletee maendeleo lakini fedha za kuwapa sina nashukuru walinielewa na kunipa nafasi hiyo na kuwanyima wanaume ambao walijivunia jinsi yao,”alisema Mkomwa.
Alisema kuwa wakati akiomba kura aliweka vipaumbele ambavyo atavifanyia kazi wakati wa uongozi wake ni pamoja na ujezi wa vyoo vya shule ya sekondari Bamba inakamilika ili mwaka huu 2025 ifunguliwe na kupokea wanafunzi zaidi ya 100 wa mtaa huo ambao wanasoma shule za sekondari za mbali ambapo hutembea umbali wa kilometa sita kwenda na kurudi shuleni.
Alisema kuwa wanaishukuru serikali ambayo ilitoa kiasi cha shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi huo pia wananchi nao walichangia kila kaya 2,000 na kufanikisha ujenzi huo kufikia hapo na kubaki hatua ndogo ili ianze ikiwa ni ukosefu wa matundu nane.
“Tuliomba tena fedha Halmashauri milioni 12 kwa matundu sita ila walituambia kuwa tusubiri na wanafunzi waendelee kusoma huko lakini mara fedha zitakapoingia wanafunzia hao watahamishiwa shuleni hapo ndiyo tunasubiri tunataka wanafunzi wanaotoka kwenye mtaa wetu waanze kusoma hapo pia itasaidia maeneo ya mitaa jirani ambao nao watanufaika,”alisema Mkomwa.
Alisema kuwa changamoto nyingine ambayo iko kwenye mipango yake katika kuitatua ni baadhi ya wakazi wa mtaa wake wapatao 23 hawana huduma ya maji kabisa hali ambayo inawasababisha kupata shida ya kupata maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya kawaida.
Alisema kuwa jambo lingine ni kuwa na stendi ya mabasi kwani sasa hakuna sehemu nzuri ya mabasi kugeuzia ambapo Kongowe ni mwisho wa ruti za baadhi ya mabasi huwa yanageuzia hapo hivyo wanaongea na Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads kuwapatia eneo la hifadhi ya barabara kwenye kituo cha mafuta cha Tawaqal kuwa na stendi hapo na ndoto yake pia ni kujenga zahanati kwenye mtaa huo ndiyo ndoto yake kabla hajamaliza uongozi wake.
“Hivi ni baadhi ya vipaumbele ambavyo nilijiwekea na haya yametokana nay ale wananchi waliyokuwa wakiayuliza kipindi cha kampeni ndiyo nimeanza nayo lakini uongozi wangu utakuwa shirikishi kwani wananchi wao ndiyo watakaokubaliana tuende na jambo gani la kimaendeleo,”alisema Mkomwa.
Alisema kuwa yeye alikuwa mjumbe wa serikali ya mtaa huo kwa kipindi cha miaka mitano na alikuwa pia Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) tawi la Bamba na alikuwa akitumiwa akimwakilisha mwenyekiti aliyepita ambaye ni marahemu Majid Kavuta ndiyo aliyemhamasisha kuwa kiongozi na hata watu walikuwa wakimwambia agombee nafasi hiyo.
“Pia Rais Dk Samia Suluhu Hassan alinihamasisha sana kuwa kiongozi kutokana na jinsi anavyoongoza nchi na Spika wa Bunge Tulia Akson naye ni moja ya watu waliokuwa kioo kwangu na moja ya vitu vilivyonifanya nichaguliwe ni jinsi nilivyokuwa nawasaidia wananchi na ilinibidi niingie kwenye siasa baada ya mume wangu kufariki dunia nikasema sasa nitajiliwaza wapi ndiyo kuingia japo ndugu zangu hawakupenda mimi kuingia kwenye siasa,”alisema Mkomwa.
Alibainisha akiwa mjumbe wa serikali ya mtaa na kiongozi wa UWT alisaidia sana wanawake na vijana na watu wenye ulemavu kupata mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 na moyo wa kuwasaidia pindi wajapo ofisini na alikuwa akisaidia vijana ikiwa ni pamoja na kwenye msuala ya michezo na vijana walimwambia wanataka awe mlezi wa mtaa huo ili awasidie.
“Nawasihi wanawake wasiwe na hofu ya kuwania nafasi ya uongozi wapambanie ndoto zao ili kufikia malengo waliyojiwekea na waachane na maneno ya kukatoisha tamaa kwani uongozi hauangalii jinsi bali ni utekelezaji wa majukumu na kufuata miongozo taratibu sheria na kanuni za uongozi zilizowekwa,”alisema Mkomwa.
Akizungumzia juu ya mwenyekiti huyo Simon Mbelwa alisema kuwa mtaa huo umepata kiongozi mzuri na alikuwa karibu na wananchi hivyo wamepata kiozi sahihi kwani ni msikivu na mpenda maendeleo anaamini kuwa ataufiukisha mbali mtaa huo.
Mbelwa alisema kuwa kiongozi huyo ana uzoefu mkubwa kwani kabla ya ksuhika nafasi hiyo alikuwa mjumbe hivyo anajua changamoto za wananchi na jinsi gani atazitatua kwa kupitia mipango na ushirikishaji wananchi kupitia vikao vya mtaa.
Kwa upande wake Swaiba Kazi alisema kuwa wanawake ni viongozi wenye uwezo mkubwa na dhana kuwa mwanamke hana uwezo si ya kweli na haipaswi kuungwa mkono na wanaweke wameonyesha gani kiongozi anatakiwa afanye.Kazi alisema kuwa wanwake wana uwezo mzuri wa kuongoza na ndiyo sababu wameaminika na kupewa nafasi hizo za juu kuanzia ngazi za chini hadi Uras hivyo wanapaswa kuungwa mkono na siyo kuwavunja moyo na mtaa huo una jumla ya wananchi 7,546 ana watoto watatu na ni mjasiriamali. Mwisho.
No comments:
Post a Comment