MAPATO ya utalii yaongezeka maradufu kutokana na watalii kuongezeka nchini kutoka Dola za Marekani 1.310.34 (Sawa na Shilingi Trilioni 3.01) mwaka 2021 hadi Dola za Marekani,527.77 (sawa la Shilingi Trilioni 5.82) ukiwa ni matunda ya filamu ya The Royal Tour.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan Abbasi wakati akielezea mafanikio ya mwaka mmoja tangu Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alipozindua filamu hiyo Jijini Arusha.
Amesema filamu ya THE ROYAL TOUR imejenga hamasa kwa watalii na wawekezaji na hamasa hiyo imekuwa na manufaa katika sekta ya usafiri wa Anga hadi kuongeza Ruti na Miruko ikiwemo ndege ya kimataifa KIA imeongezeka kwa asilimia 28 kutoka miruko 6,115 April 2021 hadi 7,850 April, 2023.
Aidha amesema kuwa Novemba mwaka jana huko Dallas,Texas, USA, Taasisi ya Tuzo za Afrimma ilimtangaza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais Mwanamke wa kwanza Afrika na Kushinda Tuzo ya Mageuzi Katika Uongozi .
Pia amesema kuwa filamu ya The Royal Tour sio ya mwisho ni mwanzo wa kuitangaza nchi kimataifa zaidi hivyo Kamati ya mwaka mmoja sasa, imepokea na inaendelea kuchambua The royal Tours nyingine .