Na John Gagarini, Kibaha
MKAZI wa Kijiji cha Bupu kata ya Bupu Tarafa ya Mkamba wilaya
ya Mkuranga mkoani Pwani Forodesi Ntabegera (30) ameuwawa kwa kubakwa kisha
kunyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa kichakani.
Kwa mujibu wa taarifa ziliotolewa na kaimu kamanda wa polisi
mkoani Pwani Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi
(SSP) Athuman Mwambalaswa Marehemu kuwa marehemu alinyongwa na watu hao kwa
kutumia kitenge chake alichokuwa amekivaa.
Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea
Septemba 9 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana baada ya wakazi wa kijiji hicho
kufanya msako wa kumtafuta marehemu ambaye alipotea Septemba 8.
“Baada ya msako huo kufanyika mwili wa marehemu ulikutwa
kwenye kichaka umbali wa mita 30 kutoka barabarani ambapo mwili wake ulimwagiwa
unga sehemu za kichwani na mgongoni,” alisema Kamanda Mwambalaswa.
Alisema watu hao walitumia mfuko wa salfeti aliokuwa amebebea
unga aliotoka kuusaga mashine, kumvisha miguuni kisha mwili wake waliulaza
kifudifudi.
Aidha alisema kuwa taarifa za kupotea marehemu zilitolewa na
kituo cha polisi Kimazinchana na mwenyekiti wa Kijiji cha Bupu Kasimu Kambangwa
walioongozana na watoto wa marehemu ambao walidai mama yao alitoweka baada ya
kuaga kuwa anakwenda kusaga na hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa
kwenye eneo hilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment