Friday, September 12, 2014

MSHINDI WA TABORA MARATHON AOMBA UFADHILI KUPIGA KAMBI NCHINI KENYA

Mwanariadha John Mwandu akihojiwa na vyombo vya habari baada ya kushinda mbio za Tabora Marathon kwenye mashindano yaliyofanyika mkoani Tabora mwaka 2013


John Mwandu akimaliza mbio za mita 1,500 kwenye mashindano ya Taifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam mwezi Julai mwaka 2014.

Mwanariadha John Mwandu akifanya mazoezi kabla ya kuingia kwenye mashindano ya Taifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro mwaka 2013

Mwanariadha John Mwandu watatu kutoka kulia kwenda kushoto akianza kukimbia mbio za mita 800, mwaka 2013 huko uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

Mwanariadha John Mwandu watatu kutoka kushoto akiwa ameshika medali na kombe baada ya kushinda mashindano ya Tabora Marathon akiwa na washindi wengine,  wapili kulia aliyevaa suti nyeusi ni mkuu wa Wilaya ya Tabora Mjini Kumchaya. Mashindano hayo yalifanyika mkoani Tabora mwaka 2013

Mwanariadha John Mwandu akiwa na washindi wngine na baadhi ya viongozi wa serikali mara baada ya kuibuka mshindi wa mashindano ya Tabora Marathon yaliyofanyika mwaka  2013,nyuma juu ni picha mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwanariadha John Mwandu akiwa na washindi wengine baada ya kushinda mbio za Tabora Marathon mashindano yaliyofanyika mkoani Tabora mwaka 2013

Mwanariadha John Mwandu akivalishwa medali na mkuu wa wilaya ya Tabora Mjini Kumchaya baada ya kushinda mashindano ya Tabora Marathon yaliyofanyika mwaka 2013

Hii ni barua ambayo inayoonyesha kukubaliwa kwa mwanariadha John Mwandu kwenda kwenye kambi ya riadha ya Mara Runners Club ya nchini Kenya ambapo Mwandu anatarajia kwenda Desemba mwaka huu hivyo anaomba wafadhili mbalilmbali kujitokeza kumsaidia ambapo barua hiyo imesainiwa mwalimu wa kituo hicho Samwel Koech (IAAF, Toecs/coach Lev. 2)

No comments:

Post a Comment