Na John Gagarini, Kibaha
MWANAFUNZI wa Chuo cha Eden Hill (EDHICO) kilichopo mtaa wa KwaMfipa
wilayani Kibaha mkoani Pwani Attu Gabriel anayekadiriwa kuwa na umri
kati ya miaka (18) na (19) amekutwa amekufa kwenye nyumba ya mpenzi
wake kwa kile kinachodaiwa kutaka kutoa mimba.
Awali mwanafunzi huyo aliomba ruhusa kwenye uongozi wa chuo hicho
Jumanne ya wiki hii kuwa anakwenda kumuuguza ndugu yake ambaye alikuwa
amelazwa kwenye hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kwamfipa, Emanuel Kilasa
alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira kati ya saa 9 au 10
alfajiri nyumbani kwa mpenzi wake Hafidh Mohamed (22) ambaye alikimbia
mara baada ya tukio hilo.
Kilasa alisema kuwa marehemu alikutwa na mauti ambapo tangu alipoomba
ruhusa hiyo alikuwa kwa mpenzi wake jirani na chuo hicho na kujaribu
kutoa mimba lakini hakufanikiwa.
"Tulipoingia kwenye chumba cha mpenzi wake tulikuta kuna vitu kadhaa
zikiwemo vidonge, chipsi, sukari na inasadikiwa kuwa alikuwa akijaribu
kutoa mimba," alisema Kilasa.
Alisema kuwa mpenzi wa marehemu siku ya tukio alikwenda kwa mama yake
mzazi aitwaye Zaina Said na kumwambia kuwa alilala na mpenzi wake
lakini haamki.
"Mama yake alipofika alimwambia kuwa marehemu ameshakufa hivyo aende
akamwambie mwenyekiti wa serikali ya mtaa ndipo alipokimbia kutokana
na tukio hilo," alisema Kilasa.
Aidha alisem akuwa baada ya tukio hilo walitoa taarifa polisi ambapo
walifika na kuuchukua mwili wa marehemu ambaye alikuwa akiishi hosteli
nyumbani kwao ikiwa ni Makambako mkoani Iringa.
Naye baba mdogo wa kijana ambaye ni mpenzi wa marehemu Lukanda Omary
alisema kuwa yeye alipata taarifa majira ya saa 3 asubuhi lakini awali
kijana huyo alisemekana kabla ya kifo hicho alisikika akiongea na
daktari ambaye bado hajafahamika akimwambia ampe marehemu chai.
"Inasemekana marehemu alikuwa akijaribu kutoa mimba lakini hali ikawa
mbaya na kujaribu kuwasiliana na daktari juu ya nini cha kufanya hivyo
inavyoonekana binti huyo alikuwa kwenye zoezi la utoaji mimba,"
alisema Omary.
Kwa upande wake Kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi wa
Polisi (SACP) Ulrich Matei alithibitisha kutokea tukio hilo na kusema
kuwa bado yuko hospitali ili kufanya uchunguzi kujua chanzo cha kifo
chake.
mwisho.
No comments:
Post a Comment