Na John Gagarini, Kibaha
KIJANA Victor Wilfred (29) mkazi wa Keko amekatisha uhai wake kwa kujinyonga kwa kutumia kanga aliyoifunga kwenye dirisha la chumba cha rafiki yake.
Marehemu kabla ya kujinyonga aliacha ujumbe usemao kuwa anaomba samahani ndugu zake kwa kufanya kitendo hicho cha kujitoa uhai hata hivyo hakuweza kuweka wazi kwamba aliamua kujiua kwa sababu gani.
Tukio hilo lilitokea Aprili 30 mwaka huu majira ya asubuhi eneo la Maili Moja Shuleni wilayani Kibaha mkoani Pwani ambapo umati wa watu ulikuwa umejazana kushuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Akithibitisha kutokea tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo ambalo lilitokea kwenye sebule ya chumba cha Emanuel Lawrance mkazi wa Keko Jijini Dar es Salaam ambaye amepangisha nyumba kwa Emanuel Msengi marehemu alikuwa mgeni kwenye nyumba hiyo na alifika kwa lengo la kutafuta kazi.
"Marehemu aliachwa na rafiki yake ambaye alikuwa amekwenda kazini na kwa kuwa rafiki yake alimuahidi kumtafutia kazi na aliporudi alikuta marehemu kajinyonga kwa kutumia kanga kwenye dirisha la chumba hicho," alisema Kamanda Matei
Hata hivyo marehemu aliacha ujumbe kwenye karatasi lililokutwa pembeni ya mwili wake kuwa kutokanana na kifo chake ana omba samahani na asisumbuliwe mtu yoyote kwani kaamua kujiua yeye mwenyewe.
mwisho.
No comments:
Post a Comment