Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Husna Iddi (16) mkazi wa
Tarafa ya Vikindu kata ya Kisemvule wilaya ya mkuranga mkoani Pwani ka
tuhuma za kusababisha mauaji ya mumewe baada ya kudaiwa kumvuta sehemu
zake za siri.
Inadaiwa kuwa wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa kimapenzi hali
iliyosababisha ugomvi kati yao hali iliyosababisha kutokea kwa tukio
hilo la kusikitisha.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa
tukio hilo na alimtaja marehemu kuwa ni Jumanne Mwarami (21).
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 24 mwaka huu
majira ya saa 2:00 usiku ambapo wakiwa nyumbani na mke wake
kulijitokeza ugomvi kati yao kwa marehemu kumtuhumu mke wake huyo kuwa
siyo mwaminifu katika ndoa yao na ana mahusiano na wanaume wengine
nje.
"Baada ya kutokuwepo kwa maelewano kati yao na ugomvi huo kuwa mkubwa
ndipo mke wake huyo alimshambulia na kumvuta mume wake sehemu zake za
siri hali iliyopelekea kupoteza maisha wakati akipatiwa matibabu
kwenye Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga," alisema Kamanda Matei.
Katika hatua nyingine,Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa
kosa la kukutwa na bangi nusu kilo huko kitongoji cha Mwandege Wilaya
ya Mkuranga.
Watuhumiwa hao ni Seleman Sahdi Ngota (35), KasimuOmari Mlumbita (25)
na Salumu Yusufu Athumani ambao watafikishwa mahakamani mara upelelezi
utakapokamilika.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment