Na John Gagarini, Kibaha
MATUKIO ya uvunjifu wa maadili
kwenye shule mbalimbali hap nchini yameendelea kuharibika baada ya wanafunzi
wanne wa shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kubaka
mwanafunzi wa darasa la pili (9) na kumsababishia maumivu yalipelekea kulazwa
hospitali ya Tumbi kwa matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi jana babu wa mtoto huyo (jina tunalo), Jacob Mrope alisema tukio
hilo lilitokea Septemba 2 majira ya saa 6 mchana, ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima, alikuwa
akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike walikimbizwa na watuhumiwa
hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuuumia mguu na kujikuta akikumbana
na dhahma hiyo.
Mrope alisema kuwa wanafunzi
wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba
mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata
msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.
“Wenzake waliokuwa nao walitoa
taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta
akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka na
kumchukua na kumpeleka shuleni na kutoa taarifa,” alisema Mrope.
Kwa upande wake dada yake Lwiza
alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao walikuwa nao
wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa
ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu na kumkokota mwenzao hadi
nyumba iliyojirani na kumjulisha.
“Alikuwa kwenye hali mbaya kwani
alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na
mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na
wenzake watatu,” alisema Lwiza.
Lwiza alisema kuwa baada ya kuona
hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za
kisheria ambapo walikwenda serikali ya mtaa kasha kwenda polisi na baadaye
hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa
bado kalazwa na hali yake inasemekena kuwa ni mbaya.
Naye mwalimu mkuu wa shule hiyo
ya Lulanzi Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema
lolote kwani sula hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na
watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.
“Ni kweli tukio hili limetokea
lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule
na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi
nyumbani mara baada ya masomo kwisha,” alisema Bilali.
Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa
mtaa wa Lulanzi Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushnagazwa
na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule
hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi
wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio
hilo kamanda wa polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa
wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na
tukio hilo.
“Wanafunzi hao wanatuhumiwa
kumbaka mwenzao wakati akitoka shule ambapo walimkamata na kumkimbiza kwenye
kichaka na kumziba mdomo ili asiweze kupiga kelele kisha walimshika miguu na
mikono na kumbaka kwa zamu na
kumsababishia maumivu makali ambapo amelazwa hospitali ya Tumbi kwa matibabu
zaidi na hali yake bado haijawa nzuri,” alisema Matei.
Matei alisema kuwa watuhumiwa hao
wanne wanahojiwa juu ya tukio hilo ambapo watafikishwa mahakamani mara
upelelezi utakapokamilika ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa daktari kuhusina na
tukio hilo lakusikitisha.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment