Na John Gagarini, Bagamoyo
KATA ya Talawanda wilayani Bagamoyo mkoani Pwani
imetenga hekta 13,000 kwa ajili ya matumizi bora ya ardhi kwa wakulima na
wafugaji ili kuondoa migogoro baina ya pande mbili hizo.
Hayo yalisema na diwani wa kata hiyo Bw Said Zikatimu
kwenye Kijiji cha Talawanda wakati wa mkutano wa hadhara ulioandaliwa na
Jumuiya ya Wazazi ya wilaya hiyo kujua kero zinazowakabili wakazi wa kata hiyo.
Bw Zikatimu alisema kuwa maeneo hayo yalitengwa na
halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kupunguza
vurugu zinazotokea mara kwa mara.
“Kati ya hekta hizo 13,000 wafugaji wametengewa hekta
5,800 huku wakulima wakitengewa hekta 9,200 kupitia mpango huo ambao utawafanya
makundi hayo kuishi kwa amani,” alisema Bw Zikatimu.
Alisema mpango huo uko kwenye vijiji vya Talawanda na
Magulumatali ambapo utaeneo kwenye vijiji vingine kadri suala la fedha
litakapokuwa liko sawa.
“Kutokana na mpango huu wafugaji wamepewa muda wa
miezi mitatu kuondoka na kwenda kwenye eneo lao lililotengwa na serikali na
endapo watashindwa kuondoka wataondolewa kwa nguvu,” alisema Bw Zikatimu.
Aidha alisema wafugaji walioingia kwenye kata hiyo kwa
ajili ya malisho kuondoka haraka ili kuondoa migogoro baina ya wakulima na
wafugaji.
Aliwataka wakulima na wafugaji kila moja akae kwenye
eneo lililopangwa kwa lengo la kuondoa mizozo isiyona na lazima.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment