Na John Gagarini, Pwani
JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini
mkoa wa Pwani inatarajia kukopesha wananchi pikipiki kupitia yao (Family Bank)
kwa ajili ya kuboresha kipato cha wakazi wa wilaya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kaimu katibu
wa jumuiaya hiyo Bw David Mramba alisema kuwa kwa sasa wanaendelea na
maandalizi ya kuanzishwa benki hiyo.
Bw Mramba alisema kuwa tayari benki kama hiyo kupitia Jumuiya
ya Wazazi Taifa tayari imeshazinduliwa na imeanza kutoa huduma Jijini Dar es
Salaam.
“Baada ya makao makuu kuzindua benki hiyo ya Jumiya ya Wazazi
na sisi tunatarajia kuifungua wakati wowote kuanzia sasa ambapo kwa sasa tunaandaa
semina kwa Makati wa kata ili nao wakawafundishe wananchi kwenye mitaa,”
alisema Bw Mramba.
Alisema pikpiki hizo zitakopeshwa kwa wananchi bila ya kujali
itikadi ya chama ambao watafuata masharti yatakayokuwa wyamewekwa ikiwa ni
pamoja na kuwa na mradi ambao unaingiza kipato si chini ya shilingi 7,500.
“Mafunzo tutakayoyatoa kwa viongozi wa kata ili kuelewa
madhumuni ya kuanzishwa kwake ili wawaelimishe walengwa ambao ni familia ili
ziweze kuongeza kipato ambapo watatoa kiasi cha shilingi 20,000 na mara
taratibu zikikamilika atatoa 500,000 na kukopeshwa pikipiki hizo na kuendelea
kurejesha kidogokidogo,” alisema Bw Mramba.
Aidha alisema kuwa mafunzo hayo kwa viongozi yatatolewa na
mkurugenzi wa benki hiyo Bw Dauda Salmin
na itafunguliwa na Bw mwenyekiti wa Wazazi mkoa wa Pwani Bw Jackson
Katunka.
Pia alimpongeza mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Bw Abdala
Bulembo kwa jitihada zake kuimarisha na kuiletea heshima na kuiboresha Jumuiya
hiyo pamoja na kurejesha mahusiano mazuri na chama.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment