Na John Gagarini, Kibaha
WASWAHILI
wanasema ukistaajabu ya Musa basi utaona ya Firauni yaliyomkuta Bw Charles Malosha (44) mkulima wa Visiga Kati
wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani yanasikitisha kwani amekumbwa na masahibu ambayo
hataweza kuyasahau katika maisha yake yote na kila aliyesikia hakika anashikwa
na simanzi kutokana na kuondolewa sehemu zake za siri katika mazingira ya
kutatanisha.
Akizungumza
jana kwenye kituo cha afya cha Mlandizi Bw Malosha mwenye watoto sita alisema
kuwa alitokewa na tukio hilo la kikatili akiwa kwenye kituo cha polisi Visiga
lakini cha kushangaza watu walivumisha kuwa amengofoa sehemu zake za siri na
kuzitafuna jambo ambalo si la kweli.
Bw
Malosha alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 26 mwaka huu majira ya
mchana ambapo alichukuliwa na mgambo na kuambiwa kuwa anaitwa kituo cha polisi
ambapo alikwenda na ndipo alipoambiwa kuwa kuna watu kadhaa wanamdai fedha
ambazo walimpa kwa ajili ya kuwanunulia kwa ajili ya kujengea.
“Wakati
niko polisi kwenye selo walifika walalamikaji wakiwa na polisi mmoja ambapo
kati yao mmoja alikuwa na rungu ambalo alinipiga nalo kichwani na kupoteza
fahamu na nilipozinduka sehemu zangu za siri (Korodani) zilikatwa na nikajikuta
damu nyingi zinamwagika na ndipo nilipokimbizwa hospitali kupata matibabu,”
alisema Bw Malosha.
Alisema
kuwa kimsingi alikuwa akidaiwa milioni tatu na watu watatu ambao walimpa fedha
kwa ajili awauzie maeneo lakini alishindwa kuwapatia maeneo hayo kwa wakati
waliokuwa wakiyataka.
“Kweli
walikuwa wakinidai na mimi nilikuwa najipanga aidha kuwarudishia fedha zao au
kuwatafutia sehemu nyingine ambapo tangu tuanze kuwasiliana ni kama miezi minne
imepita sasa,” alisema Bw Malosha.
Kwa
upande wake mkewe Bi Martha Boni alisema kuwa siku ya tukio hilo alimwaga na
kumwambia hata mwona tena hivyo alee watoto wake jambo ambalo lilimshangaza
lakini hakuweza kumfafanulia kuwa alikuwa akimaanisha nini.
“Baada
ya muda nilipigiwa simu na kuambiwa kuwa mume wangu yuko hoi hospitali na
hawezi kuongea kwa kweli nilichanganyikiwa na kutaka kujua yaliyomsibu lakini
nilijulishwa kuwa ameondolewa sehemu zake za siri jambo ambalo lilizidi
kuniumiza na kushindwa kujua nini cha kufanya na kuanguka chini kasha kupoteza
fahamu,” alisema Bi Boni.
Bi
Boni alisema kuwa anashangaa kusikia watu hao wakisema kuwa wanamdai milioni 20
jambo ambalo si lakweli kwani wanamdai shilingi milioni sita tu na alichukua
milioni mbili kwa kila mmoja kwa watu watatu ambao wanatokea Jijini Dar es
Salaam.
Naye
mganga wa kituo hicho cha afya cha Mlandizi Dkt Nicetus Matem alisema kuwa
alimpokea mgonjwa huyo ambaye alifika hapo huku akiwa anatokwa na damu nyingi
na kumhudumia hadi damu ilipoacha kutoka.
“Ni
kweli sehemu zake hizo za kiwanda cha kuzalishia mbegu (Korodani) zimeondolewa
kabisa lakini hazikuondolewa na kitu chenye ncha kali bali kwani zilondolewa
kwa kitu kiischo na ncha kali na nilipomuuliza alisema kuwa amezinyofoa yeye
mwenyewe,” alisema Dkt Matem.
Dkt
Matem alisema kuwa alirudishia vizuri lakini cha kusikitisha ni kwamba Bw
Malosha hataweza kuzaa tena lakini hali ya sehemu yake kuu ya siri itakuwa
ikifanya kazi kama kawaida na hali yake inaendelea vizuri.
Naye
kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Ulrich
Matei alisema kuwa taarifa alilzozipata ni kuwa mtu huyo alijijeruhi mwenyewe
na alikuwa akidaiwa na milioni 11.5 na watu wanne tofauti.
“Aliachiwa
shamba na bibi mmoja ambapo alikuwa akikata maeneo na kuyauza na yule mmiliki
alipofika alisema kuwa maeneo aliyoyauza ni ya kwake kwani hakumruhusu kuyauza
hivyo atajuana na watu hao hivyo awalipe yeye mwenwe,” alisema Matei.
Kamanda
Matei alisema kuwa watu hao walianza
kumdai na kusema kuwa aliwadanganya kuwa eneo hilo ni lake hivyo arejeshe fedha
zao kutokana na kuchanganyikiwa alifikia hatua ya kutaka kujiua.
“Lengo
lake kujidhuru alitaka kujiua na hakufanyiwa kitendo hicho na mtu bali alifanya
yeye mwenye na kwamba alifanyiwa na mtu si kweli na kama kuna mtu kamfanyia na
kama kuna mtu anaficha ukweli nitafutailia kujua na akipata nafuu tutamhoji
kupata ukweli kwani hana nia ya kumlinda mtu yoyote kwani kila mtu ana haki zake
za msingi,” alisema Matei.
Aliongeza
kuwa mtu huyo aliamua kufanya hivyo baada ya kuona kuwa sasa hana njia na ana
deni na kuona njia ni kujiua na haiwezekani afanyiwe kitendo hicho kwenye kituo
cha polisi.
Mwisho