Tuesday, August 6, 2024

TEAC IMELENGA KUSAIDIA MKULIMA NA MFUGAJI.

Na Wellu Mtaki, Dodoma.

Mkuu wa Kanda ya kati ya Tume ya Nguvu za Atom Tanzania ( TEAC ) Machibya Anthony Matulanya amesema kuwa Tume imelenga  kusaidia wakulima na wafugaji kupata mavuno makubwa ambayo yataongeza pato la uchumi wa nchi na mtu mmoja mmoja.

Hayo ameyasema Leo Tarehe 5 Agost 2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari Katika Banda la Tume ya Nguvu za Atom Tanzania Katika viwanja vya nanenane Zuguni jijini Dodoma huku akiwasihi wananchi kutembelea Banda ilo Ili kujifunza mambo mbalimbali yatakayokuza na kuboresha kilimo na ufugaji.

Adha amesema kuwa Tume inajishughulisha na swala la uhamasishaji wa Matumizi ya Nuclear nchini ambayo inalenga kuhakikisha teknolojia ya nuclear inakunza uchumi wa nchi.

"Tume ya nguvu za Atom Tanzania zinajishughulisha na swala la uhamasishaji ya matumizi Nuclear nchini lakini kwa usalama  ambapo wanalenga kuhakikisha kwamba teknologia ya Nuclear nchini  inatumika vizuri na inakuza uchumi wa nchi." Amesema Matulanya.

Pia meeleza kuwa teknologia ya nuclear imeweza kutumika kuangamiza  wadudu aina ya Mbung'o ambao wanang'ata Mifugo na  kusababusha Hali ya upungufu wa Maziwa kwa ng'ombe pamoja na kukosa nyama iliyo Bora.

"Kwa upande wamifugoTeknologia ya Nuclear imetumika imeangamiza wadudu aina ya Mbung'o , Mb'ung'o ni wadudu atali ambao wanang'ata Mifugo 

Hawa wadudu waking'ata kwa mfano Ng'ombe wanamsababishia Hali ya upungufu wa Maziwa na pia uwezi kupata nyama nzuri" amesema Matulanya.

Mayulanya amesema kuwa zipo mbegu Bora za Mpunga ambazo zinatumika Tanzania bara na nzazibar ambazo zinauwezo Mkubwa wa kuimili ukame na ahitaji maji Mengi katika kuzalisha na unafanya mmea usivunjike .

"Pia kwa upande wa kilimo teknologia ya Nuclear imetumiaka huko nzazibar na bara, mbegu ya mpunga aina ya   super DC  ambayo inatumika Mbegu hizi ambazo zimeboreshwa  uwezo Mkubwa wa kuimili ukame ambayo mbegu hiyo ukiilima aitaji maji Mengi Katika kutoa matunda yake" Amesema Matulanya 

"Baada ya kuboreshwa mbengu hiyo imekuwa na stimilivu na yenye kutoa faida kubwa kwa mkulima pamoja na mmea kustaimili usivunjike na huo mpunga baada ya kuuvuna na kuukoboa unakuwa mtamu" Amesema Matulanya 

Ikumbukwe kuwa  Tume ya Atom Tanzania  inajishughulisha na swala la uhamasishaji ya matumizi Nuclear nchini lakini kwa usalama.

Monday, August 5, 2024

BRELA KUANZA KUSAJILI WAKULIMA

Na Wellu Mtaki, Dodoma

OFISA Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Gabriel Gilangay amesema wakala huo umejipanga kuanza kuwasajili  Wakulima kwa kuwapa nembo ambayo itawatambulisha kibiashara. 

Gilangay amesema hayo Jijini Dodoma kwenye maonesho ya Wakulima Nanenane wakati akizungumza na Waandishi wa habari na kueleza kuwa Wakala huo unashughulikia mambo mengi  kwa wakulima nchini ikiwemo usajili wa Biashara. 

Mbali na hayo amesema  BRELA hutoa huduma hizo ili kuhakikisha  biashara za kilimo zinakubalika kisheria ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za ushauri kuhusu jinsi ya kufuata taratibu za kisheria katika biashara ya kilimo, ikiwa ni pamoja na kanuni za usajili, sheria za biashara, na masharti ya leseni.

Kwa upande mwingine Wakala huo hushughulikia Kampuni za Umma,Kampuni zinazoshiriki soko la hisa,Kampuni za Kibinafsi na Kampuni zinazomilikiwa na watu wachache.

TIMU ZA UMISSETA NA UMITASHUMTA MKOA WA PWANI ZAKABIDHI VIKOMBE






TIMU za Umoja wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) na Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) za Mkoa wa Pwani zimekabidhi makombe ilivyoshinda kwenye mashindano ambayo yaliyomalizika Mkoani Tabora hivi karibuni.

Mchatta akipokea vikombe na tuzo na kuwapongeza wachezaji hao ofisini kwake Mjini Kibaha ambapo timu za riadha zilifanya vizuri kwenye michezo ya riadha na kutupa mkuki kwenye michezo hiyo.

Amesema kuwa wachezaji hao wameuletea sifa mkoa wa Pwani na hiyo imetokana na kutumia vyema vipaji vyao na kuwa na nidhamu na kuzingatia yale waliyofundishwa na walimu wao.

"Nimeambiwa wachezaji tisa watashiriki mashindano ya sekondari kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayofanyika hivi karibuni nchini Uganda nawasihi mlinde viwango vyenu,"amesema Mchatta.

Aidha amesema kuwa wanariadha hao waige mfano wa mchezaji wa riadha Steven Akwari ambaye licha ya kuumia lakini alikimbia na kumaliza mbio licha ya maumivu makali.

Naye Mkurugenzi wa Filbert Bayi Elizabeth Mjema amesema kuwa shule inaomba kusaidiwa baadhi ya mahitaji ikiwa ni pamoja na lishe, maji na matunda.

Mjema amesema kuwa inawagharamia baadhi ya wanafunzi wenye vipaji ambao wazazi wao hawana uwezo ambapo lengo la Filbert Bayi ni kutaka wanariadha kufanya makubwa kwenye mchezo huo.

 Kwa upande wake mwalimu wa riadha wa timu za Filbert Bayi Ally Nyonyi amesema kuwa timu hiyo inafanya vizuri kutokana na kuwa na maandalizi mazuri na nidhamu.

Nyonyi amesema kuwa wao ni mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo kwenye mashindano ya Umisseta na Umitashumta Taifa hiyo inatokana na kuwa na mazingira rafiki ya kufanyia michezo ambapo wanakuwa na muda mwingi wa kufanya mazoezi baada ya masomo.

Wakielezea jinsi walivyojiandaa na mashindano hayo huko Uganda wachezaji hao wamesema kuwa wamejiandaa vya kutosha na wanaamini watailetea nchi ushindi.

Sunday, August 4, 2024

YPC YAWATAKA VIJANA KUJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI

VIJANA wa kike na kiume wametakiwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa mwakani.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Vijana (YPC) ya Kibaha Israel Ilunde alipokuwa akizungumza na Habarileo ofisini kwake.

Ilunde alisema kuwa wameanzisha mradi uitwao (K-Vote) unaohamasisha ushiriki wa vijana kwenye masuala ya umma, elimu ya mpiga kura, uraia, kuwasaidia na kuwaelimisha vijana wanaotaka kuwania nafasi za uongozi kwenye chaguzi hizo.

"Tume Huru ya Uchaguzi inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya vijana milioni tano na wale ambao hawakuwahi kupiga kura miaka ya nyuma tunawasihi wajitikeze kuhakiki taarifa zao itakapofika muda wa kufanya hivyo ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi,"alisema Ilunde.

Alisema vijana wanapaswa kushiriki zoezi hilo ambalo ni muhimu sana kwani wasipojiandikisha au kuboresha taarifa zao watakuwa watazamaji na hawataruhusiwa kupiga kura.

"Idadi ya vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi serikali za mitaa mwaka 2004 na uchaguzi mkuu mwaka 2005 ilikuwa ni asilimia 8 tu na mwaka 2015 iliongezeka na kufikia asilimia 50 na mwaka huu na mwakani itaongezeka,"alisema Ilunde.

Aidha alisema kuwa baadhi ya vijana hao walichaguliwa kwenye nafasi za uongozi ikiwa ni pamoja na ubunge, udiwani, wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa.

"Tuna mfano wa Dk Zainab Katimba ni Naibu Waziri na mbunge Salome Makamba walifanya vizuri na pia kuachana na dhana kuwa uchaguzi mtaji ni fedha bali ni watu, nidhamu, uchapakazi, kujali watu,"alisema Ilunde.

Aliwataka vijana kutonunua kura kwani zinavunja heshima na zinaaibisha Taifa na uongozi unakuwa wa kulipa madeni pia wafanye siasa za heshima bali ziwe za hoja na kuweka utu mbele na kutofanya vurugu wanaposhindwa na waijali jamii.


Thursday, August 1, 2024

DK BITEKO AMWAKILISHA RAIS MKUTANO MKUU (TLS)

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko leo Agosti 1, 2024 amemwakilisha Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Miaka 70 wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) unaofanyika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma. 

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Pindi Chana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dkt. Eliezer Feleshi, pamoja na Wanachama wa Chama cha Wanasheria Tanganyika. 

Itakumbukwa kuwa TLS ilianzishwa mnamo mwaka 1954 ikiwa na mawakili takribani 141 wakiwa ni wakoloni hadi ilipofika mnamo Oktoba 31,1961 ilipopata wakili wa kwanza Mtanganyika.

Hadi sasa TLS ina jumla ya mawakili takribani 12,471 wanaofanya kazi za usaidizi wa kisheria katika taasisi mbalimbali za kisheria nchini.

MH.RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA TRENI YA KISASA (SGR)



Mhe.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua Rasmi Huduma za Usafiri wa Treni ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam – Morogoro hadi Dodoma, katika eneo la Stesheni Jijini Dar es Salaam, leo 1 Agosti, 2024.

WAZIRI MKUU AFUNGUA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 01, 2024 afungua maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yanafanyika  kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma,

Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.