Thursday, December 5, 2013

SITA WAFA PWANI

Na John Gagarini, Kibaha

WATU sita wamepoteza maisha katika matukio tofauti yaliyotokea Mkoani Pwani.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msiadizi Juma Yusufu Ally alithibitisha kutokea kwa matukio hayo na kueleza kuwa katika tukio la kwanza Bw Ramadhani Lubaya (35) mkulima na mkazi wa kijiji cha Kondo aliuwawa na watu wasiofahamika wakati akichunga mifugo ipatayo 90 porini ikiwa ni mchnganyiko wa ng’ombe na mbuzi mali ya Bw Malick Seif.

Tukio hilo lilitokea majira ya saa 9:00 alasiri Novemba  28 mwaka huu  katika Kijiji cha Kondo kata ya Zinga Wilaya ya Bagamoyo kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso.

Bw Ally alisema kuwa katika tukio la pili huko kijiji cha Gwata Kata ya Mzenga Tarafa ya Mzenga Wilaya ya Kisarawe mfanya biashara Bw Peter Gumbi (28) mkazi wa Ngerengere Mkoa wa Morogoro aliuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika kisha kuporwa Tsh. 1,300,000/= alizokuwa nazo kwa ajili ya kwenda kununulia ng’ombe majira ya saa 8:00 mchana Novemba tarehe mwaka huu.

Alisema kuwa marehemu alikutwa na mauti wakati akitoka kijiji cha Gwata kwenda Dololo kwenye mnada akiwa amepakiwa kwenye Pikipiki. Dereva wa pikipiki hiyo anshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.

Aidha katika tukio la tatu alisema mkazi wa Kitongoji cha Madafu Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Bw Hamadi Juma (46) fundi ujenzi aliuwawa na wananchi waliojichukulia sheria mikononi baada ya kumtuhumu kupora pikipiki ambayo mmiliki wake bado kufahamika majira ya saa 3:30 usiku Novemba 28

“Marehemu alifikwa na mauti baada ya kushambuliwa kwa mawe na vigongo sehemu mbalimbali za mwili, kutokana na tukio hilo Jeshi la Polisi linaendesha msako mkali ili kuweza kuwabaini wale waliohusika katika tukio hilo kwa kisingizio cha hasira kali,” alisema Kamanda Ally.

Alibainisha kuwa katika tukio lingine, mnamo Novemba 30 mwaka huu majira ya saa 08:30 usiku huko Kijiji cha Msata Kata ya Msata Wilaya ya Bagamoyo Bw Ally Abdallah Mlenga (56) mkulima na ambaye pia anajishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji alivamiwa nyumbani kwake na watu nane ambao walimshambulia kwa mapanga na kumuua na kisha kumjeruhi mtoto wake aitwaye Bw Abdallah Ally (25) kwa kumkata mapanga kichwani na kifuani.

“Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi walivamia nyumba hiyo na kuvunja mlango kwa kutumia kitu kizito na baada ya kutenda kosa hilo hawakuchukua kitu chochote,” alisema Kamanda Ally.

Aidha katika tukio linguine Bw Hassan Hamadi mkazi wa Kijiji cha Mbebetini  Kata ya Kibiti Wilaya ya Rufiji (25) aliuwawa na watu waliojichukulia sheria mkononi katika tukio lilitokea majira ya Desmba 1 mwaka huu majira ya saa 7:45 usiku baada ya kumtuhumu kuvunja duka la Bw Selapia Stephen (47).

Kamanda Ally, alithibitisha kupoteza maisha kwa Omary Milondomo (17) mkazi wa Kinguila baada ya kugongwa na gari katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Kilwa majira ya saa 2:30 usiku wa Novemba  30 mwaka huu huko katika Kijiji cha Mbembetini Kata ya Kibiti Wilaya ya Rufiji.

Alibainisha kuwa marehemu alifikwa na mauti baada ya kugongwa na gari ambayo haikufahamika namba ambayo haikusimama baada ya kutenda kosa hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Rufiji ukisubiri kufanyiwa uchunguzi wa daktari.

Mwisho.


Wednesday, December 4, 2013

MAHAFALI CBE MRS M MAUMBA

MRS M MAUMBA MARA BAADA YA KUPEWA MAUA
 AKIWA AMEPOZI NA MOJA YA NDUGU ZAKE
AKIWA AMNAVISHW ATAJI NA MOJA YA RAFIKI ZAKE
 AKIWA AMEPOZI NA MOJA YA NDUGU ZAKE
 KULIA NI MWANAE NA KUSHOTO NI MUHITIMU MWENZAKE
AKIWA NA WAHITIMU WENZAKE NA NDUGU YAKE KULIA
AKIWA NA MOJA YA WATU WALIOKWENDA KUMPONGEZA
AKIWA NA WENZAKE WAKIMSIKILIZA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA HAYUPO PICHANI

Tuesday, December 3, 2013

MAHAFALI MAMA FATUMA MAUMBA


MATUKIO MBALIMBALI YAKIMUONYESHA MAMA MZAZI WA MWANDISHI WA HABARI FATUMA MAUMBAJU, MARIAMU M MAUMBA ALIPOHITIMU DIPLOMA YA ACCOUNTANCY (PGDA) KWENYE MHAFALI( CBE)KWENYE  MAHAFALI YALIYOFANYIKA KWENYE KLABU YA SIGAR JIJINI DAR ES SALAAM AMBAPO MGENI RASMI ALIKUWA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA












 


Monday, November 25, 2013

WATU MILIONI MOJA NA NUSU HUFARIKI

Na John Gagarini, Kibaha

IMEELEZWA kuwa watu milioni moja na nusu hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani zinazotokea hapa nchini.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Mohamed Mpinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya kukumbuka watu waliokumbwa na majanga ya ajali za barabarani.

Kamanda Mpinga alisema kuwa mbali ya vifo hivyo pia jail hizo zinasababisha majeruhi zaidi ya 20,000 hadi 50,000 huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu.

“Ajali ni moja ya vyanzo vya vifo vya watu wengi hapa nchini ambapo zinashika nafasi ya nane kwa kusababisha vifo na ifikapo mwaka 2020 kitakuwa ni chanzo cha tano kwa vifo,” alisema Kamanda Mpinga.

Alisema kuwa hadi mwezi Oktoba mwaka huu jumla ya ajali zaidi ya 19,000 zimetokea na kusababisha vifo zaidi ya 3,000 ukiachilia jail za hivi karibuni iliyoua watu saba mkoani Morogoro na iliyotokea mkoani Dodoma na kuua watu watatu.

“Watu wanaokufa ni nguvu kazi ya Taifa ambapo wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka (18) hadi (35) hivyo Taifa kupoteza nguvu kazi kubwa ambayo ndiyo inayozalisha mali na kukuza uchumi wa nchi,” alisema Kamanda Mpinga.

Aidha alisema kuwa jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali kwa madereva wazembe ambao wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa ajili za barabarani na kuwataka abiria kutoa taarifa kwa madereva wanaoendesha mabasi kwa mwendo wa kasi.

Kwa upande wake mtendaji wa shirika la Global Helmet Vaccine Initiative Bw Alpherio Nchimbi alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka wahanga wote waliopata matatizo kutokana na ajali za barabarani duniani.

Alisema kuwa moja ya wahanga wa ajali ni wanafunzi ambao wamekuwa wakigongwa mara wanapokuwa wakivuka kwenda ama kurudi shuleni.

“Tunawashauri madereva na wale wanaotumia vyombo vya moto kuachana na tabia ya kutumia vilevi ambavyo vimeonekana kuwa ni chanzo kikuu cha ajali za barabarani,” alisema Nchimbi.

Mwisho.

MADEREVA BODABODA WAFA AJALINI

Na John Gagarini, Kibaha

JUMLA ya watu nane wamepoteza maisha katika matukio mawili tofauti yaliyotokea mkoani Pwani likiwemo la madereva bodaboda wa tano kupoteza maisha kwa kugongana na gari la mizigo aina ya Scania uso kwa uso.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Pwani Ulrich Matei alisema kuwa matukio hayo yalitokea Novemba 21 mwaka huu majira ya saa 2: usiku.

Kamanda Matei alisema kuwa kwenye tukio la kwanza waendesha pikipiki (bodaboda) walipoteza maisha baada ya kugonga uso kwa uso na gari lenye namba za usajili T.602 ACT katika kichwa na tela lenye namba T.493 ABP aina ya Scania  likiendeshwa na Bw Dastan Migunda (35), mkazi wa Kitunda Dar es Salaam majira ya saa 2.00 usiku huko eneo la Ruvu Darajani kata ya Vigwaza barabara ya Dar es Salaam – Morogoro Wilaya ya Bagamoyo.

“Waliopoteza maisha katika tukio hilo ni, Bw Saidi Dosa (17), Bw Severine Luoga (19),  Bw Philemon Job (20), Bw Nassoro Mzalamila (18) na Bw Sadam Mapunda (21)  huku majeruhi wa ajali hiyo ni Bw Peter Maswaga (25) wote hawa ni wakazi wa Picha ya Ndege Wilaya ya Kibaha,” alisema Kamanda Matei.
.
Alisema kuwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni mwendo kasi wa waendesha pikipiki watatu pikipiki zao zenye namba T.164 CHF, T.953 CQB na T.426 CJZ zote zikiwa ni aina ya Sanlg ambapo walikuwa wanatokea Picha ya Ndege kwenda Kijiji cha Buyuni kumfuatilia Bw Ramadhani Rajabu (16) dereva wa bodaboda kwa Mathias aliyetuhumiwa kwa wizi wa Pikipiki yenye namba.T.216 CNC aina ya Sanlg.

“Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Tumbi Kibaha ikisubiri kufanyiwa uchunguzi wa Daktari na Majeruhi anaendelea na matibabu Hospitali ya Tumbi Kibaha,” alisema Matei.

Katika tukio la Pili, Kamanda Matei alithibitisha watu watatu kupoteza maisha huko Kitongoji cha Kibong’wa Kijiji cha Kisarawe Kata ya Kisarawe Tarafa ya Sungwi Wilaya ya Kisarawe  Mkoa wa Pwani majira ya saa 8.50 mchana.

Alisema kuwa watu hao walifikwa na mauti wakati walikuwa wanachimba kokoto kwenye shimo ambao ni Bi Mwazani Salehe (18), Ally Twaha (2), pamoja na Hasnatha Semin mwenye miezi (5) wote wakazi wa Kibong’wa.

Kamanda Matei aliongeza kuwa watu hao walifariki dunia baada ya kuangukiwa na udongo ulioporomoka na kuwafukia wote kwenye machimbo ya kokoto wakiwa wamejipumzisha chini ya shimo.

Aidha alisema tukio hilo mtu mmoja alinusurika kifo ambaye ni Bi Amina Emil (28), mkulima mkazi wa Kibong’wa ambaye alijeruhiwa na amelazwa Hospitali ya Wilaya Kisarawe akiendelea na matibabu, miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa nduguzao kwa mazishi.
Mwisho.

STORY

Na John Gagarini, Bagamoyo

KUFUATIA Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo
MkoaniPwani,kuridhia kupitisha

rasmi kuanza kwa mchakato wa jimbo la Chalinze kuwa Wilaya baadhi ya
wakazi wa mji huo wameunga

mkono hatua hiyo.

Azimio hilo la Chalinze kuwa wilaya liliafikiwa baada ya Mwenyekiti wa
baraza hilo, Bw Shukuru
Mbato kuwataka madiwani hao kupiga kura za ndio ama hapana,katika
kikao cha baraza hilo,ambapo

wote kwa kauli moja walipiga kura ya ndio na hivyo kubariki maamuzi hayo.

Kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema kuwa maamuzi hayo
yametolewa katika muda muafaka

na itasaidia Jimbo hilo kuendelea kukua kwa haraka hatimaye kuongeza
ajira na uchumi wake.

Mmoja wa wananchi hao ,Bi Kibena Mtoro alisema kwa kuanza kwa mchakato
huo ni faraja kwa wakazi

wa Chalinze na Bagamoyo kwajumla.

"Unajua mchakato huu umekuja muda muafaka kwakuwa umeenda sambamba na
ugawaji wa

vijiji,vitongoji vipya na kata mpya,hivyo kutaondoa tatizo la viongozi
kutawala maeneo makubwa

ambayo hushindwa kufikia wananchi kirahisi na utekelezaji kuwa
hafifu," alisema Bi Mtoro.

Kwa upande wake Bw Alex Matonange alisema kuwa mara mji huo
utakapokuwa wilaya itasaidia

kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiutendaji ambazo kwa sasa
wanazipata mbali huko wilayani

Bagamoyo

Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Bw Samuel
Salianga alisema kuwa ushirikiano

baina ya madiwani hao na viongozi mbalimbali watawezesha kufanikisha
jambo hilo.

Bw Salianga aliongeza kwamba mchakato huo wa jimbo la Chalinze kuwa
wilaya unahitaji uharaka

kabla ya kikao cha baraza la maendeleo la wilaya hiyo (DCC) na cha Mkoa (RCC).

Na John Gagarini, Kibaha

KATIKA kuhakikisha mji wa Kibaha unaongeza fursa za uwekezaji
Halmashauri ya Mji huo Mkoani

Pwani,imetenga hekari zaidi ya 3,000 kwa ajili ya viwanda ili kukuza
uchumi wa mji huo sambamba

na kuongeza ajira kwa vijana.

Akizungumzia na waandishi wa habari jinsi mji wa kibaha unavyokua na
changamoto zake,Mwenyekiti

wa Halmashauri ya mji wa kibaha, Bw Addhudad Mkomambo alisema katika
awamu ya kwanza katika eneo

la Zogowale kwenye shamba la zegereni  walipima viwanja 10 ambavyo
vimeshachukuliwa viwanja sita

na vimebaki vinne.

Bw Mkomambo alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya fursa hiyo , ni
eneo la Zogowale lenye

hekari 1,048 kwenye shamba la Zegereni ambalo lilikuwa likimilikiwa na
Serikali na Kitovu  cha

mji huo.

"Maeneo mengine ni Mitamba ambapo wizara ya mifugo imeikabidhi
halmashauri hiyo hekari zaidi ya

2,000 na Miyomboni katika kata ya Misugusugu ambapo pametengwa kwa
ajili ya kuendeleza viwanda

vidogovidogo," alisema Bw Mkomambo.

Alisema kuwa kati ya viwanja vilivyochukuliwa tayari ni kiwanda cha
nondo ambacho kimeshaanza

kazi, kiwanda cha jipsam,kiwanda cha kuchuja mafuta machafu,pamoja na
ujenzi wa kiwanda cha

kiwanda cha biskuti.

"Kwasasa tumetangaza viwanja 20 katika eneo hilo hilo ambapo watu
wameshachukua fomu za viwanja

vyote na bado tutaendelea kutenga maeneo zaidi ili kuhakikisha mji wa
Kibaha unakuwa na viwanda

vingi ili kupanua wigo wa ajira," alisema Bw Mkomambo.

Aliongeza kuwa hata hivyo alibainisha kuwa wanakabiliana na changamoto
ya madalali wanaomiliki

maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza kwa muda mrefu hatimaye kuwa pori
lengo likiwa kuyauza kwa

gharama kubwa miaka ya usoni .

"Watu wengine wanashangaza ,wanachukua maeneo makubwa hekari 500 hadi
1,000,pasipo kuyatumia eti

wanayaacha kwa ajili ya kuyauza kwa gharama kubwa baadae,watu wa namna
hiyo hatuwahitaji katika

mji wa kibaha,"alisema Mkomambo.


Mwenyekiti huyo wa halmashauri alisema Kufuatia hali hiyo ,wamejipanga
kupambana na  watu
hao kwa kuhakikisha wanawafuatilia kwa muda uliopangwa na
atakayebainika kuwa ni mbambaishaji

atavunjiwa mkataba wake.

Aliwataka wawekezaji nchini kuwekeza viwanda Kibaha kwani mji wa Dar
es salaam umejaa hivyo

kwasasa wilaya ya kibaha inatoa vipaumbele kwa kuendelea kutenga
maeneo mengi ya viwanda ili

kukuza mji huo na kuongeza ajira.

mwisho.

Na John Gagarini, Kibaha

KATIKA kuhakikisha wanafunzi waishio mazingira magumu taasisi isiyo ya
kiserikali ya Mbonde

Foundation inayoshughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu
na yatima imetoa vifaa

vya shule kwa wanafunzi zaidi ya 40 wa shule ya msingi Boko
Timiza,wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha Bw Wilson Ezekiel
alisema msaada huo kwa

wanafunzi ambao ni viatu, madaftari na Kalamu ni mwanzo wa usaidizi
kwa watoto hao mpaka

watakapofikia elimu ya sekondari.

Bw Ezekiel alisema watoto hao ambao kila mmoja amepatiwa namba maalum
ya utambulisho na tayari

wameshatengewa bajeti ya mwaka mzima kwa ajili ya mahitaji yao muhimu ya shule.

Mmoja wa wanafunzi ambao wamefaidika na msaada huo Said Ally wa darasa
la tatu ameishukuru

taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo ambao utawasaidia kufanya vizuri
katika masomo yao na

halikadhalika wamewasaidia wazazi wao kwa kiasi Fulani katika
kuwapunguzia majukumu.

Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao Bw Ally Mohamed ameishukuru taasisi
hiyo na kusema kuwa

wameonyesha kuwajali wanafunzi na wamepunguza mzigo kwa wazazi ambao
wengi wana majukumu mengi

huku hali ya maisha ikiwa ngumu.

Bw Mohamed aliwataka kuendelea na usaidizi wao kwa watoto wenye
uhitaji ili kuweza kuongeza kasi

ya mafanikio katika sekta ya elimu ili kuunga mkono hatua ya serikali
kuwataka wadau kujitokeza

kuisaidia.

mwisho.

Na John Gagarini, Kibaha

WAZAZI na wananchi wa wilaya ya Kibaha wametakiwa kuwasaidia wanafunzi
wa shule mbalimbali

mkoani Pwani ili kuwanusuru na ajali za barabarani kwani kati ya
wahanga ni kundi hilo ambalo wanahitaji kusaidiwa.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani nchini Mohamed Mpinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kukumbuka watu waliokumbwa na majanga ya ajali za barabarani.

Kamanda Mpinga alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamepoteza maisha
kutokana na ajali mbalimbali hususani wanapokuwa wakivuka barabara
waendapo shule au wanaporudi nyumbani hivyo lazima wapewe msaada
kuwanusuru na ajali.

Katika hatua nyingine alisema mbali ya vifo hivyo vya wanafunzi pia
ajali hizo zinasababisha majeruhi zaidi ya 20,000 hadi 50,000 huku
wengine wakipata ulemavu wa kudumu.

“Ajali ni moja ya vyanzo vya vifo vya watu wengi hapa nchini ambapo
zinashika nafasi ya nane kwa kusababisha vifo na ifikapo mwaka 2020
kitakuwa ni chanzo cha tano kwa vifo,” alisema Kamanda Mpinga.

Alisema kuwa hadi mwezi Oktoba mwaka huu jumla ya ajali zaidi ya
19,000 zimetokea na kusababisha vifo zaidi ya 3,000 ukiachilia jail za
hivi karibuni iliyoua watu saba mkoani Morogoro na iliyotokea mkoani
Dodoma na kuua watu watatu.

“Watu wanaokufa ni nguvu kazi ya Taifa ambapo wengi wao ni vijana
wenye umri kati ya miaka (18) hadi (35) hivyo Taifa kupoteza nguvu
kazi kubwa ambayo ndiyo inayozalisha mali na kukuza uchumi wa nchi,”
alisema Kamanda Mpinga.

Aidha alisema kuwa jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali kwa
madereva wazembe ambao wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kutokea
kwa ajili za barabarani na kuwataka abiria kutoa taarifa kwa madereva
wanaoendesha mabasi kwa mwendo wa kasi.

Kwa upande wake mtendaji wa shirika la Global Helmet Vaccine
Initiative Bw Alpherio Nchimbi alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo
ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka wahanga wote waliopata
matatizo kutokana na ajali za barabarani duniani.

Alisema kuwa moja ya wahanga wa ajali ni wanafunzi ambao wamekuwa
wakigongwa mara wanapokuwa wakivuka kwenda ama kurudi shuleni.

“Tunawashauri madereva na wale wanaotumia vyombo vya moto kuachana na
tabia ya kutumia vilevi ambavyo vimeonekana kuwa ni chanzo kikuu cha
ajali za barabarani,” alisema Nchimbi.

Mwisho.

VIZIWI WAHITAJI MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

Na John Gagarini, Kibaha

TIMU ya Viziwi mkoani Pwani (PDSC) inatarajia kuingia kambini Desemba
20 mwaka huu kwenye uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha kujiandaa na
mashindano ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha katibu
wa timu hiyo Daudi Kulangwa alisema kuwa timu hiyo kwa sasa inaendelea
na mazoezi yake kwenye uwanja wa Kongowe wilayani Kibaha.

Kulangwa alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika Januari 7 hadi 11
mwaka 2014 ambapo wao na Dar es Salaam wamealikwa watachuana na timu
wenyeji ambao ni Unguja na Pemba.

“Tunaendelea na mazoezi lakini changamoto yetu kubwa ni ukosefu wa
vifaa kama vile jezi ambapo tunacheza vifua wazi, hatuna viatu na
kujikuta wakicheza pekupeku na mipira,” alisema Kulangwa.

Alisema kuwa wanawaomba watu mbalimbali wakiwemo wabunge wa mkoa wa
Pwani wajitokeze kuwasaidia ili waweze kufanya vema.

“Maombi yetu tayari tumeyapeleka ofisi ya Mfuko wa Maendeleo ya
Wanawake (WAMA) pamoja na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani ambao
wameonyesha nia ya kutusaidia,” alisema Kulangwa.

Alibainisha kuwa mbali ya changamoto hizo wanaendelea na mazoezi chini
ya walimu wao Zuberi Boka na Philbert Mbwette na kuwataka watu
waitembelee timu yao na kuiunga mkono ili iweze kufanya vizuri kwenye
mashindano hayo.

Mwisho.