Na John Gagarini, Bagamoyo
KUFUATIA Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo
MkoaniPwani,kuridhia kupitisha
rasmi kuanza kwa mchakato wa jimbo la Chalinze kuwa Wilaya baadhi ya
wakazi wa mji huo wameunga
mkono hatua hiyo.
Azimio hilo la Chalinze kuwa wilaya liliafikiwa baada ya Mwenyekiti wa
baraza hilo, Bw Shukuru
Mbato kuwataka madiwani hao kupiga kura za ndio ama hapana,katika
kikao cha baraza hilo,ambapo
wote kwa kauli moja walipiga kura ya ndio na hivyo kubariki maamuzi hayo.
Kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi walisema kuwa maamuzi hayo
yametolewa katika muda muafaka
na itasaidia Jimbo hilo kuendelea kukua kwa haraka hatimaye kuongeza
ajira na uchumi wake.
Mmoja wa wananchi hao ,Bi Kibena Mtoro alisema kwa kuanza kwa mchakato
huo ni faraja kwa wakazi
wa Chalinze na Bagamoyo kwajumla.
"Unajua mchakato huu umekuja muda muafaka kwakuwa umeenda sambamba na
ugawaji wa
vijiji,vitongoji vipya na kata mpya,hivyo kutaondoa tatizo la viongozi
kutawala maeneo makubwa
ambayo hushindwa kufikia wananchi kirahisi na utekelezaji kuwa
hafifu," alisema Bi Mtoro.
Kwa upande wake Bw Alex Matonange alisema kuwa mara mji huo
utakapokuwa wilaya itasaidia
kurahisisha upatikanaji wa huduma za kiutendaji ambazo kwa sasa
wanazipata mbali huko wilayani
Bagamoyo
Naye mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Bw Samuel
Salianga alisema kuwa ushirikiano
baina ya madiwani hao na viongozi mbalimbali watawezesha kufanikisha
jambo hilo.
Bw Salianga aliongeza kwamba mchakato huo wa jimbo la Chalinze kuwa
wilaya unahitaji uharaka
kabla ya kikao cha baraza la maendeleo la wilaya hiyo (DCC) na cha Mkoa (RCC).
Na John Gagarini, Kibaha
KATIKA kuhakikisha mji wa Kibaha unaongeza fursa za uwekezaji
Halmashauri ya Mji huo Mkoani
Pwani,imetenga hekari zaidi ya 3,000 kwa ajili ya viwanda ili kukuza
uchumi wa mji huo sambamba
na kuongeza ajira kwa vijana.
Akizungumzia na waandishi wa habari jinsi mji wa kibaha unavyokua na
changamoto zake,Mwenyekiti
wa Halmashauri ya mji wa kibaha, Bw Addhudad Mkomambo alisema katika
awamu ya kwanza katika eneo
la Zogowale kwenye shamba la zegereni walipima viwanja 10 ambavyo
vimeshachukuliwa viwanja sita
na vimebaki vinne.
Bw Mkomambo alisema maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya fursa hiyo , ni
eneo la Zogowale lenye
hekari 1,048 kwenye shamba la Zegereni ambalo lilikuwa likimilikiwa na
Serikali na Kitovu cha
mji huo.
"Maeneo mengine ni Mitamba ambapo wizara ya mifugo imeikabidhi
halmashauri hiyo hekari zaidi ya
2,000 na Miyomboni katika kata ya Misugusugu ambapo pametengwa kwa
ajili ya kuendeleza viwanda
vidogovidogo," alisema Bw Mkomambo.
Alisema kuwa kati ya viwanja vilivyochukuliwa tayari ni kiwanda cha
nondo ambacho kimeshaanza
kazi, kiwanda cha jipsam,kiwanda cha kuchuja mafuta machafu,pamoja na
ujenzi wa kiwanda cha
kiwanda cha biskuti.
"Kwasasa tumetangaza viwanja 20 katika eneo hilo hilo ambapo watu
wameshachukua fomu za viwanja
vyote na bado tutaendelea kutenga maeneo zaidi ili kuhakikisha mji wa
Kibaha unakuwa na viwanda
vingi ili kupanua wigo wa ajira," alisema Bw Mkomambo.
Aliongeza kuwa hata hivyo alibainisha kuwa wanakabiliana na changamoto
ya madalali wanaomiliki
maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza kwa muda mrefu hatimaye kuwa pori
lengo likiwa kuyauza kwa
gharama kubwa miaka ya usoni .
"Watu wengine wanashangaza ,wanachukua maeneo makubwa hekari 500 hadi
1,000,pasipo kuyatumia eti
wanayaacha kwa ajili ya kuyauza kwa gharama kubwa baadae,watu wa namna
hiyo hatuwahitaji katika
mji wa kibaha,"alisema Mkomambo.
Mwenyekiti huyo wa halmashauri alisema Kufuatia hali hiyo ,wamejipanga
kupambana na watu
hao kwa kuhakikisha wanawafuatilia kwa muda uliopangwa na
atakayebainika kuwa ni mbambaishaji
atavunjiwa mkataba wake.
Aliwataka wawekezaji nchini kuwekeza viwanda Kibaha kwani mji wa Dar
es salaam umejaa hivyo
kwasasa wilaya ya kibaha inatoa vipaumbele kwa kuendelea kutenga
maeneo mengi ya viwanda ili
kukuza mji huo na kuongeza ajira.
mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
KATIKA kuhakikisha wanafunzi waishio mazingira magumu taasisi isiyo ya
kiserikali ya Mbonde
Foundation inayoshughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu
na yatima imetoa vifaa
vya shule kwa wanafunzi zaidi ya 40 wa shule ya msingi Boko
Timiza,wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha Bw Wilson Ezekiel
alisema msaada huo kwa
wanafunzi ambao ni viatu, madaftari na Kalamu ni mwanzo wa usaidizi
kwa watoto hao mpaka
watakapofikia elimu ya sekondari.
Bw Ezekiel alisema watoto hao ambao kila mmoja amepatiwa namba maalum
ya utambulisho na tayari
wameshatengewa bajeti ya mwaka mzima kwa ajili ya mahitaji yao muhimu ya shule.
Mmoja wa wanafunzi ambao wamefaidika na msaada huo Said Ally wa darasa
la tatu ameishukuru
taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo ambao utawasaidia kufanya vizuri
katika masomo yao na
halikadhalika wamewasaidia wazazi wao kwa kiasi Fulani katika
kuwapunguzia majukumu.
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao Bw Ally Mohamed ameishukuru taasisi
hiyo na kusema kuwa
wameonyesha kuwajali wanafunzi na wamepunguza mzigo kwa wazazi ambao
wengi wana majukumu mengi
huku hali ya maisha ikiwa ngumu.
Bw Mohamed aliwataka kuendelea na usaidizi wao kwa watoto wenye
uhitaji ili kuweza kuongeza kasi
ya mafanikio katika sekta ya elimu ili kuunga mkono hatua ya serikali
kuwataka wadau kujitokeza
kuisaidia.
mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha
WAZAZI na wananchi wa wilaya ya Kibaha wametakiwa kuwasaidia wanafunzi
wa shule mbalimbali
mkoani Pwani ili kuwanusuru na ajali za barabarani kwani kati ya
wahanga ni kundi hilo ambalo wanahitaji kusaidiwa.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na kamanda wa kikosi cha usalama
barabarani nchini Mohamed Mpinga, wakati wa maadhimisho ya siku ya
kukumbuka watu waliokumbwa na majanga ya ajali za barabarani.
Kamanda Mpinga alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamepoteza maisha
kutokana na ajali mbalimbali hususani wanapokuwa wakivuka barabara
waendapo shule au wanaporudi nyumbani hivyo lazima wapewe msaada
kuwanusuru na ajali.
Katika hatua nyingine alisema mbali ya vifo hivyo vya wanafunzi pia
ajali hizo zinasababisha majeruhi zaidi ya 20,000 hadi 50,000 huku
wengine wakipata ulemavu wa kudumu.
“Ajali ni moja ya vyanzo vya vifo vya watu wengi hapa nchini ambapo
zinashika nafasi ya nane kwa kusababisha vifo na ifikapo mwaka 2020
kitakuwa ni chanzo cha tano kwa vifo,” alisema Kamanda Mpinga.
Alisema kuwa hadi mwezi Oktoba mwaka huu jumla ya ajali zaidi ya
19,000 zimetokea na kusababisha vifo zaidi ya 3,000 ukiachilia jail za
hivi karibuni iliyoua watu saba mkoani Morogoro na iliyotokea mkoani
Dodoma na kuua watu watatu.
“Watu wanaokufa ni nguvu kazi ya Taifa ambapo wengi wao ni vijana
wenye umri kati ya miaka (18) hadi (35) hivyo Taifa kupoteza nguvu
kazi kubwa ambayo ndiyo inayozalisha mali na kukuza uchumi wa nchi,”
alisema Kamanda Mpinga.
Aidha alisema kuwa jeshi la polisi litaendelea kuchukua hatua kali kwa
madereva wazembe ambao wamekuwa wakichangia kwa kiasi kikubwa kutokea
kwa ajili za barabarani na kuwataka abiria kutoa taarifa kwa madereva
wanaoendesha mabasi kwa mwendo wa kasi.
Kwa upande wake mtendaji wa shirika la Global Helmet Vaccine
Initiative Bw Alpherio Nchimbi alisema kuwa lengo la maadhimisho hayo
ambayo hufanyika kila mwaka ni kuwakumbuka wahanga wote waliopata
matatizo kutokana na ajali za barabarani duniani.
Alisema kuwa moja ya wahanga wa ajali ni wanafunzi ambao wamekuwa
wakigongwa mara wanapokuwa wakivuka kwenda ama kurudi shuleni.
“Tunawashauri madereva na wale wanaotumia vyombo vya moto kuachana na
tabia ya kutumia vilevi ambavyo vimeonekana kuwa ni chanzo kikuu cha
ajali za barabarani,” alisema Nchimbi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment