Na John Gagarini, Kibaha
WACHEZAJI wa michezo ya Umoja wa
Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) mkoa wa Pwani
wametakiwa kushindana na si kushiriki kwenye michuano hiyo ngazi ya Kanda ili
mkoa utoe wachezaji wengi.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na ofisa
elimu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Benjamini Majoya wakati wa ufungaji wa
michezo hiyo ngazi ya mkoa kwenye viwanja vya Filbert Bayi na kusema kuwa
ushindani ndiyo unaotakiwa na si ushiriki.
Majoya alisema kuwa mashindano ya
Kanda ambayo yatafanyika mkoani Morogoro mwezi ujao ili kupata timu itakayounda
kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro kwa ajili ya timu
itakayokwenda mkoani Mwanza kwenye mashindano ya Taifa.
“Michezo ni sehemu ya kuendeleza
taaluma hivyo lazima mcheze ip[asavyo na si muende kwa ajili ya kushiriki tu
lazima mpambane na kuonyesha vipaji vyenu ili muwakilishe vyema mkoa na kutoa
wachezaji wengi kuwakilisha kanda ya Mashariki,” alisema Majoya.
Aidha aliwataka wanamichezo hao
kuonyesha nidhamu wakati wanacheza michezo kwani nidhamu ndiyo mafanikio ya
michezo kwani bila ya kuwa na nidhamu itakuwa vigumu kufanikiwa.
Kwa upande wake ofisa michezo wa mkoa
wa Pwani Grace Bureta alisema kuwa michezo hiyo ilihusisha wilaya sita za mkoa
huo ambapo jumla ya wachezaji 136 wa michezo mbalimbali walichaguliwa kwa ajili
ya kuunda timu ya mkoa.
Bureta alisema kuwa timu hiyo
itaingia kambini kwa muda wa siku nne hadi Mei 31 ambapo Juni Mosi wataelekea
mkoani Morogoro kwa ajili ya mashindano ya kanda ya Mashariki.
Alisema kuwa wachezaji waliochaguliwa
ni wazuri na anategemea watafanya vizuri kwa kutoa wachezaji wengi kuunda timu
ya Kanda na kufanikiwa kutetea ubingwa wa jumla wa mashindano hayo kitaifa
mjini Mwanza.
Mwisho.Na John Gagarini, Kibaha
MKOA wa Pwani umechagua jumla ya
wanamichezo 136 wa michezo mbalimbali kwa ajili ya kuunda timu ya mkoa ya Umoja
wa Michezo na Sanaa kwa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa ajili ya
kushiriki michezo ya Kanda ya Mashariki.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Ofisa
Michezo wa mkoa wa Pwani Grace Bureta wakati wa ufungaji wa michezo hiyo ngazi
ya wilaya iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Filbert Bayi.
Bureta alisema kuwa mashindano hayo
ambayo yaliwahusisha wachezaji toka kwenye shule za sekondari za wilaya sita za
mkoa huo ambazo ni Mafia, Rufiji, Kibaha Mjini na Vijijini, Kisarawe, Mkuranga
na Bagamoyo walifanikiwa kupata wachezaji ambao walifanya vizuri.
“Mara baada ya michezo kukamilika na
kuchaguliwa wachezaji hao timu itaingia kambini kwa muda wa siku nne hadi Mei
31 ambapo Juni Mosi wataelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya mashindano ya kanda
ya Mashariki,” alisema Bureta.
Alisema kuwa wachezaji waliochaguliwa
ni wazuri na anategemea watafanya vizuri kwa kutoa wachezaji wengi kuunda timu
ya Kanda na kufanikiwa kutetea ubingwa wa jumla wa mashindano hayo kitaifa
mjini Mwanza.
Benjamini Majoya aliwataka
wanamichezo wa mkoa huo kushindana na si kushiriki kwenye michuano hiyo ngazi
ya Kanda ili mkoa utoe wachezaji wengi watakaounda kanada hiyo.
Majoya alisema kuwa mashindano ya
Kanda ambayo yatafanyika mkoani Morogoro mwezi ujao ili kupata timu itakayounda
kanda ya Mashariki inayoundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro kwa ajili ya timu
itakayokwenda mkoani Mwanza kwenye mashindano ya Taifa.
“Michezo ni sehemu ya kuendeleza
taaluma hivyo lazima mcheze ip[asavyo na si muende kwa ajili ya kushiriki tu
lazima mpambane na kuonyesha vipaji vyenu ili muwakilishe vyema mkoa na kutoa
wachezaji wengi kuwakilisha kanda ya Mashariki,” alisema Majoya.
Aidha aliwataka wanamichezo hao kuonyesha
nidhamu wakati wanacheza michezo kwani nidhamu ndiyo mafanikio ya michezo kwani
bila ya kuwa na nidhamu itakuwa vigumu kufanikiwa, michezo iliyoshindaniwa ni
pamoja na soka, pete, wavu, kikapu, riadha na bao.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment