Na
John Gagarini, Chalinze
ADHA
ya akinamama wajawazito kujifungua mbele za wanaume kutokana na zahanati ya
Kijiji cha Pongwe Kiona wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kuwa na chumba kimoja
cha matibabu huenda ikaondoka baada ya kuchangiwa kiasi cha shilingi milioni
moja na mifuko 70 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wanawake na wanaume.
Kutokana
na zahanati hiyo kuwa na chumba kimoja imesababisha akinamama kujifungua huku
kukiwa na wanaume jambo ambalo limesababisha kutokuwa na usiri hivyo utu wa
mwanamke kutokuwepo.
Msaada
huo umetolewa na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ambapo fedha na Saruji vilikabidhiwa na Katibu wa Mbunge huyo Iddy
Swala kwa niaba ya Mbunge.
Akizungumzia
changamoto hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Rajab Mgaya alisema kuwa zahanati
hiyo ilijengwa mwaka 1964 na ina wodi moja tu.
“Tunamshukuru
Mbunge kwani hii ilikuwa changamoto kubwa kwa akinamama wanaojifungua huku
kukiwa na akinababa nao wanapata matibabu humo hivyo usiri kutokuwepo kutokana
na hali hiyo,” alisema Mgaya.
Kwa
upande wake Diwani wa Kata ya Kimange Husein Hadingoka alisema kuwa mbunge huyo
ameonyesha upendo wa hali ya juu kwa kutoa vitu hivyo ambavyo vitasaidia ujenzi
huo.
Hadingoka
alisema kuwa wananchi watafanya ujenzi huo ambapo yeye alitoa 100,000 kwa ajili
ya kufanikisha ujenzi huo na kusema atafurahi kuona uujenzi huo unakamilika
mapema.
Naye
moja ya wakazi wa Kijiji hicho ambaye ni mwanamama Sikudhani Ally alisema kuwa
kujifungua huku wanaume wakiwepo ni mtihani mkubwa lakini kwa mpango huo
utakuwa umeweka stara ya mwanamke.
Kwa
upande wake katibu wa Mbunge Swala alisema kuwa mbunge ametoa msaada huo baada
ya kutemebelea hivi karibuni akiwa kwenye ziara zake za kikazi na wananchi
kutoa kilio chao juu ya hali hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment