Na John Gagarini, Kibaha
WAFANYABIASHARA wa
maduka ambayo yaliungua moto eneo la Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani
wamepewa msaada wa mifuko 30 ya saruji yenye thamani ya shilingi 480,000 kwa
ajili ya kujenga maduka yao.
Msaada huo
ulitolewa na mdau huyo ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk David
Nicas na kusema kuwa ameamua kujitolea ili kuwafariji wahanga hao ambao
wamepata hasara kubwa.
Dk Nicas alisema
kuwa wafanyabiashara hao walikuwa na mataratijio makubwa ya kuboresha biashara
na maisha yao lakini ndoto zao zimekwenda kinyume.
“Janga la moto au
lolote halina hodi wa taarifa linatokea wakati wowote bila ya kutegemea na
linaleta umaskini kwani hawa waliamka na fedha lakini sasa hawana fedha tena na
sisi ndiyo wa kuwasaidia ili kuwapa moyo, alisema Dk Nicas.
Aidha alisema kuwa
moto huo umesababisha hasara ambayo haiwezi kulipika zaidi ya kuwasaidia na
kuwafariji wafanyabiashara hao ambao bidhaa zao pamoja na fedha viliteketea kwa
moto.
“Tunaimba serikali
ya mkoa kuhakikisha inakuwa na gari lake la zimamoto badala ya kutegemea kutoka
Jijini Dar es Salaam, licha ya kuwa wanalipa fedha kwa ajili ya huduma za
zimamoto,” alisema Dk Nicas
Kwa upande wake
mwakilishi wa wafanyabiashara hao Ally Gonzi alishukuru msaada huo na kusema
kuwa umekuja wakati mwafaka na utawasaidia kukabiliana na gharama za ujenzi
mpya wa maduka yao.
“Tunashukuru kwa
msaada huu na tunawaomba wadau wengine nao wajitokeze kutusaidia ili angalau
tuweze kurejesha biashara zetu kama ilivyokawaida,” alisema Gonzi.
Alisema kuwa
gharama za hasara waliyoipata inakadiriwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 700
ambapo katika tukio hilo mfanyabiashara mmoja alijeruhiwa na moto.
Mwisho.
Na John Gagarini,
Kibaha
MKE wa Mbunge wa
Jimbo la Kibaha Mjini mkoani Pwani Selina Koka ametoa hundi ya shilingi milioni
moja kwa Chama Cha Msalaba Mwekundu tawi la Maili Moja ili wanunulie vifaa vya
kutolea msaada wakati wa majanga.
Akizungumza mjini
Kibaha wakati wa mkutano wa Chama na kusema kuwa amejitolea fedha hizo kwa
ajili ya kuboresha utoaji huduma kwa chama hicho kwenye jamii.
Koka alisema kuwa
chama hicho ni muhimu ndani ya jamii kwani kimekuwa kikisaidia mara yanapotokea
maafa mbalimbali katika jamii kama vile moto, ajali, mafuriko, kimbunga na
majanga mengine.
“Nimesikia kwenye
risala yenu kuwa mnaazima vifaa kwa ajili ya kutolea huduma naomba niwapatie
fedha ili mnunue vifaa vyenu ili mfanye kazi zenu kwa uhakika bila ya
kubahatisha,” alisema Koka.
Aidha alisema kuwa
chama hicho ni muhimu sana kwa jamii kwani kinajitolea kusaidia watu wenye
matatizo mbalimbali na dhana kuu ya chama ni kujitolea.
“Hawa wanajitolea
kwenye shughuli mbalimbali hivyo tunaomba wadau wajitokeze kuwasaidia hawa ili
waisaidie jamii yenye matatizo,” alisema Koka.
Naye mwenyekiti wa
chama hicho tawi la Maili Moja Lazaro Kwiligwa alisema kuwa wanamshukuru mke wa
Mbunge kwani vifaa ilikuwa ni changamoto kubwa kwao.
“Tulikuwa tunaazima
vifaa jambo ambalo linatusababisha tushindwe kutoa huduma ipasavyo lakini sasa tutafanya kazi zetu kwa uhuru,”
alisema Kwiligwa.
Lazaro alisema kuwa
tawi hilo lilianza mwaka 2013 na lina wanachama 280 huku hai wakiwa 168 ambapo
aliwataka wanachama wote walipe ada zao ili wawe hai.
Mwisho.
Picha 3831 Mke wa
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Selina Koka kushoto akimkabidhi jora la
kushonea sare, mwenyekiti wa tawi la Maili Moja la chama cha msalaba mwekundu
Lazaro Kwiligwa.
Picha 3830 Mke wa
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Selina Koka kushoto akimkabidhi kizibao mwenyekiti
wa chama cha msalaba mwekundu tawi la Maili Moja Lazaro Kwiligwa.
Picha 3829 Mke wa
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Selina Koka akionyesha moja ya vizibao ambavyo
alivitoa kwa chama cha msalaba mwekundu tawi la maili Moja, kulia mwenyekiti wa
tawi hilo Lazaro Kwiligwa na katikati ni msaidizi wa Mbunge Method Mselewa.
Picha 3784 Mdau wa
Maendeleo wa maili Moja wilayani Kibaha Dk David Nicas kushoto akimkabidhi
mfuko wa sementi moja ya wafanyabiashara ambao maduka yao yaliteketea kwa moto
Ally Gonzi kulia
Picha Na John
Gagarini