NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ameshauri Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuvipatia fedha za mikopo za asilimia 10 vikundi vya ujasiriamali vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Tuesday, July 11, 2023
VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI VYA TASAF VIKOPESHWE ASILIMIA 10 ZA HALMASHAURI
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete ameshauri Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kuvipatia fedha za mikopo za asilimia 10 vikundi vya ujasiriamali vilivyopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
MHE.MASANJA : FILAMU YA "THE ROYAL TOUR" IMEFANIKIWA KWA KIWANGO KIKUBWA SANA
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema filamu ya “The Royal Tour” iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kwamba kwa sasa watalii wameongezeka.
Mhe. Masanja ameyasema hayo leo Julai 11,2023 alipotembelea Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea Jijini humo.
“Tunatambua kwamba ni nadra sana kumpata Kiongozi anayeamua kuongoza kwa vitendo kama alivyofanya Rais Samia, ametangaza kwa vitendo vivutio vyetu hivyo tunatakiwa kuvitembelea vivutio hivyo ili kumuunga mkono” Mhe. Masanja amesisitiza.
Mhe. Masanja ametumia nafasi hiyo kuwahimiza Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyoko nchini akitolea mfano wa maeneo ya Malikale, Misitu ya Asili, tamaduni za Kitanzania, historia za Tanzania za Waasisi wa Taifa na maeneo mengine ya utalii.
“Tutembelee vivutio vyetu, ukishakitembelea kile kivutio unakuwa umechangia pato la Taifa lakini hata wewe mwenyewe utakuwa umejifunza historia ya nchi ilivyo lakini pia utapunguza hata msongo wa mawazo” Mhe. Masanja amefafanua.
KAMPUNI YA GGML NA WIZARA YA MADINI KWA KUTOA ELIMU
WIZARA ya Madini imepongezwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kutoa elimu kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda la Wizara, taasisi zake na wadau wa Sekta ya Madini.
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 11, 2023 na Mwanasheria Mkuu wa kampuni ya GGML David Nzaligo alipotembelea banda la Wizara ya Madini (MADINI PAVILION) katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Nzaligo ameipongeza kampuni hiyo kwa kuleta Mkaa Mbadala wa Rafiki Briquettes ambao utasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira hapa nchini.
Akiwa katika banda la kampuni ya GGML ambalo lipo pia ndani ya banda la madini, Nzaligo amewapongeza wafanyakazi wa GGML na kampuni zingine ndani ya banda hilo kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kutoa elimu ya shughuli wanazozifanya ikiwemo uchimbaji madini na mnyororo wake.
"Nafahamu GGML wapo vizuri kwenye miradi mingi ya kijamii pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi. Nafurahi kwamba mafanikio hayo wanayaelezea vizuri kwa kila mwananchi anayetembelea banda la GGML," alisema.
MAOFISA UTUMISHI WAONYWA
Monday, July 10, 2023
HALMASHAURI YA MJI YAPONGEZWA KUPITIA TASAF
HALMASHAURI ya Mji Kibaha imepongezwa kwa kutekeleza kwa vitendo uhawalishaji wa fedha kwa kaya maskini kiasi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) cha shilingi bilioni 3.1 kwa kaya 2,583.
TASAF YATAKIWA KUANDAA TAARIFA ZINAZOAKISI MAFANIKIO YA TASAF
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete amewataka waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye wilaya nchini kuandaa taarifa zinazoakisi mafanikio au changamoto ya mfuko huo.
MHE.MASANJA AFANYA MKUTANO WA HADHARA SENGEREMA, AGUSA MAKUNDI MAALUM
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amekabidhi baiskeli tano zenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa wananchi wenye ulemavu wa miguu Wilayani Sengerema na kuahidi kuwalipia bima ya afya, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukutana na makundi maalum katika Jamii Mkoani Mwanza.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika eneo la Stendi ya zamani Mhe. Masanja amesema Serikali ya Awamu Sita inayoongozwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mikakati ya kutatua changamoto za makundi maalum yasiyojiweza katika jamii hivyo msaada huo ni utekelezaji wa ilani ya CCM.
Mhe. Masanja amewaelekeza Madiwani na viongozi wengine wa Serikali kuibua wananchi wenye changamoto mbalimbali za ulemavu ili Serikali iwafikie na kuwasaidia.
"Kama kuna wananchi huko hawawezi kutembea wengine mmewaficha ndani, na kama kuna watoto wadogo hawawezi kwenda shule waleteni Serikali itawahudumia" Mhe. Masanja amesisitiza.
Aidha, Mhe. Masanja amewataka wananchi kuhakikisha wanaiunga mkono Serikali na kuipigia kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu unaokuja.
Katika mkutano huo, Mhe. Masanja amesikiliza changamoto za baadhi ya wananchi kuhusu kero ya watumishi wa maliasili kukamata baiskeli na pikipiki za wananchi, kero za maji, kero ya uhaba wa vifaa vya kujifungulia katika vituo vya afya,ardhi, uhaba wa walimu kero za wafanyabiashara ndogondogo.
Mhe. Masanja ameahidi kuziwasilisha kero hizo katika Sekta husika na kufanyia kazi kero zinazohusu Sekta ya Maliasili na Utalii.