Thursday, May 29, 2014

BILALI KUZINDUA MFUKO WA ELIMU KIBAHA MEI 31



Na John Gagarini, Kibaha
MFUKO wa elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani utazinduliwa Mei 31 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Gharib Bilali.
Kwenye uzinduzi huo ambao utafanyika mjini Kibaha mgeni rasmi ataongoza matembezi ya hisani kwa ajili ya kuhamasisha uchangiaji wa mfuko huo ambao una lengo la kupata kiasi cha shilingi milioni 300.
Akielezea juu ya tukio hilo mwenyekiti wa mfuko huo Anna Bayi alisema kuwa  katika uzinduzi huo kutatanguliwa na matembezi ya hisani yatakayoanzia maeneo ya Mkoani hadi viwanja vya Maili Moja ambapo ndipo halfa itafanyika.
Bayi alisema kuwa  hadi sasa tayari wameshapata kiasi cha shilingi milioni 180 zitakazosaidia kuiwezesha halmashauri hiyo kukabiliana na changamoto za sekta ya elimu hususan madawati na maabara.
"Mara zitakapopatikana fedha hizo tutaanzia kununulia madawati 1,500 yenye thamani ya shilingi milioni 90 na kujenga maabara tatu kwa shilingi Milion 210,” alisema Bayi.
Alisema uchangiaji huo utakuwa ni zoezi endelevu ili kuhakikisha wanapunguza ama kumaliza kabisa changamoto za kielimu katika halmashauri ya Mji wa Kibaha.
“Kila mwananchi anatakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 2,000 wakiwemo  ,wafanyabiashara, wamiliki wa makampuni na wadau wa elimu na hadi sasa mwamko unaonekana kwa wananchi hivyo kuwa na imani ya kuwa mfuko utafanikiwa,” alisema Bayi.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo, Jeniffer Omolo alisema mfuko huo umeundwa chini ya sheria namba 288 kifungu kidogo namba 80 katika tangazo la serikali namba 218 la tarehe 18 Juni 2010.
“Shule za msingi na sekondari za serikali bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinafanya lengo la utoaji elimu bora kushindwa kufikiwa kikamilifu,” alisema Omolo.
Alibainisha kuwa Shule za msingi zilizopo wilayani Kibaha Mji  zinakabiliwa na uhaba wa madawati 3,488 hali inayopelekea baadhi ya shule hizo wanafunzi kutumia kukaa zaidi ya watatu kwenye dawati moja.
Aidha alisema katika upande wa shule za sekondari kuna upungufu wa maabara 24 ambapo kwa sasa kuna maabara 9 pekee, Halmashauri ya mji wa Kibaha ina jumla ya shule za msingi 47 na shule za sekondari za serikali na binafsi 34 .
Mwisho.

HOUSE GIRL ATUPA KICHANGA ADAKWA



Na John Gagarini, Kibaha
MSICHANA Theresia Matai (19) ambaye ni mfanyakazi wa ndani mkazi wa Kwa Mathias wilayani Kibaha mkoani Pwani anashaikiliwa na Jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake aliyejifungua.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu majira ya saa 3 usiku.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Mwembe tayari nyuma ya nyumba ya Dalaida Samwel (54) ambaye ni bosi wake ambapo alikuwa akifanya kazi za ndani.
“Baada ya kufanya tukio hilo alirudi ndani na kulala na aliweza kufahamika baada ya wasiri kutoa taarifa kuwa mtuhumiwa alionekana kuwa na mimba na baada ya kujifungua alimwacha mtoto huyo nyuma ya nyumba hiyo,” alisema Kamanda Matei.
Alibainisha kuwa jirani yake na mwenye nyumba Filbert Sekeleno (31) alipata taarifa kutoka kwa jirani mwenzake aliyefahamika kwa jina la Mama Frank kuwa kuna sauti ya mtoto nyuma ya nyumba alipokutwa mtoto huyo.
“Majirani waliongozana hadi kwenye eneo la tukio na kumkuta mtoto mchanga wa kiume akiwa ametelekezwa na kutoa taarifa polisi ambao walianza uchunguzi juu ya tukio hilo,” alisema Kamanda Matei.  
Aidha alisema kuwa mtuhumiwa alipelekwa hospitali ya Tumbi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na daktari kujua chanzo kilichosababisha kufanya tukio hilo ambapo mtoto huyo anaendelea vizuri.
Mwisho.




Wednesday, May 28, 2014

HOUSE GIRL ATUPA KICHANGA AKAMATWA NA POLISI



Na John Gagarini, Kibaha
MSICHANA Theresia Matai (19) ambaye ni mfanyakazi wa ndani mkazi wa Kwa Mathias wilayani Kibaha mkoani Pwani anashaikiliwa na Jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumtupa mtoto wake aliyejifungua.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu majira ya saa 3 usiku.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Mwembe tayari nyuma ya nyumba ya Dalaida Samwel (54) ambaye ni bosi wake ambapo alikuwa akifanya kazi za ndani.
“Baada ya kufanya tukio hilo alirudi ndani na kulala na aliweza kufahamika baada ya wasiri kutoa taarifa kuwa mtuhumiwa alionekana kuwa na mimba na baada ya kujifungua alimwacha mtoto huyo nyuma ya nyumba hiyo,” alisema Kamanda Matei.
Alibainisha kuwa jirani yake na mwenye nyumba Filbert Sekeleno (31) alipata taarifa kutoka kwa jirani mwenzake aliyefahamika kwa jina la Mama Frank kuwa kuna sauti ya mtoto nyuma ya nyumba alipokutwa mtoto huyo.
“Majirani waliongozana hadi kwenye eneo la tukio na kumkuta mtoto mchanga wa kiume akiwa ametelekezwa na kutoa taarifa polisi ambao walianza uchunguzi juu ya tukio hilo,” alisema Kamanda Matei.  
Aidha alisema kuwa mtuhumiwa alipelekwa hospitali ya Tumbi kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi na daktari kujua chanzo kilichosababisha kufanya tukio hilo ambapo mtoto huyo anaendelea vizuri.
Mwisho.






Monday, May 26, 2014

MATUKIO PWANI





  










 Na John Gagarini, Kibaha

WATU wawili wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana huko eneo la Bwawani kata ya Ubena Tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 25 mwaka huu majira ya saa 10:30 jioni katika barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro.

Kamanda Matei alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha gari T 752 ADE aina ya Toyota Landcruiser likiendeshwa na Anthony Paul (47) raia wa Uingereza ambaye ni mkazi wa Rock Garden mkoani Morogoro akitokea Dar es Salaam kwenda Morogoro aligongana uso kwa uso na gari namba T 404 CSN aina Forester lililokuwa likiendeshwa na Hizza Semkubo na kusababisha vifo hivyo.

Aliwataja waliokufa kuwa  dereva Semkubo na abiria aitwaye Odino Haule (45) na majeruhi wanne amao ni Happy Michael (21), Jamila Jaffary (21) ambao ni wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Dar es Salaam.

Aidha aliwataja majeruhi wengine kuwa ni Joseph Mapunda (30) mkazi wa Iringa ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam kutokana na hali yake kuwa mbaya.

Kamanda Matei alisema kuwa dereva Paul na majeruhi wengine wawili walikimbizwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu, Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari namba T 404 CSN kuyapita magari mengine bila ya kuchukua tahadhari na miili ya maerehemu imehifadhiwa katika hospitali Teule ya Tumbi.

Mwisho.
Na John Gagarini, Kibaha

WATU 10 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu wakiwemo wanawake watatu waliopatikana na bangi kilogramu 2 ikiwa kwenye mfuko wa plastiki maarufu kama Rambo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kamanda wa polisi mkoani humo Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei amesema kuwa watuhumniwa hao walikamatwa Mei 19 mwaka huu 19 majira ya saa 09:00 alasiri huko Mkuranga Kata/Tarafa ya Mkuranga Wilaya ya Mkuranga.

Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa na  askari waliokuwa doria,  watuhumiwa hao ni Ummy  Mkwachu (32) mkazi wa Mbagala Charambe, Amina Said (23), mkazi wa Mbagala Kiburugwa na Sarah Daud (19), mkazi wa Mbagala Charambe wakiwa na Bhangi yenye uzito wa kg 2 ikiwa imefungwa kwenye mfuko wa nailoni (Rambo), wakisafirisha katika gari lenye namba za usajili T117 BKN aina ya Toyota Hiace wakitokea Dar es Salaam kwenda Kisiju wilayani Rufiji.


Kamanda Matei alisema kuwa kwenye tukio lingine Salum Rashid (43) mkazi wa Ubena Zomozi anashikiliwa kwa tuhuma ya kupatikana na silaha aina ya Gobore bila ya Kibali.

Alibainisha kuwa tukio hilo lilitokea Mei 23 mwaka huu majira ya saa 05:41 asubuhi huko Kijiji cha Ubena kata ya Ubena Tarafa ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo, ambapo askari wakiwa doria walimkamata mtuhumiwa huku sila hiyo ikiwa na risasi moja.

 Katika tukio lingine watu watatu wanshikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kupatikana na Madawa ya kulevya aina ya Mirungi bunda 33 wakiwa ndani ya Basi la kampuni ya Tawfiq lenye namba za usajili T 248 KBT likitoka Tanga Kwenda Jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Mei 24mwaka huu majira ya saa 08:15 mchana huko kijiji cha Msoga kata/Tarafa ya Msoga Wilaya ya Bagamoyo.

Watuhumiwa hao walikamatwa na askari waliokuwa doria, ambapo waliwakamata walimkamata Hafidh Siraji, ( 22), mkazi wa Tanga, akiwa na Mirungi bunda 33 sawa na kg 33 ndani ya gari lenye namba za usajili T 248 KBT aina ya Isuzu Bus.

Katika hatua nyingen jeshi hilo linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuvua samaki kwa njia haramu ya nyavu ambazo zimepigwa marufuku na serikali.

Alisema kuwa tukio hilo limetokea Mei 25 mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi huko maeneo ya Bondeni Pwani Kata ya Kilindoni Tarafa ya kusini Wilaya ya mafia

Alifafanua kuwa askari wakiwa doria waliwakamata Ussi Juma, (50), mkazi wa Msufini, Ahmad Saleh,(22), mkazi wa Msufini na Ahmad Bakari,(27), mkazi wa Kichangachui wakivua samaki kwa kutumia nyavu haramu.


MWISHO.