WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameupigia debe uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha kutumiwa na Timu za Taifa zitakazokuwa zinajiaandaa na michuano ya CHAN na AFCON kwa ajili ya mazoezi.
Majaliwa aliyasema hayo alipotembelea kuukagua uwanja huo ambao utatumika kwenye usinduzi wa mbio za mwenge 2025.
Majaliwa alisema kuwa jana alifanya ukaguzi wa viwanja vitatu viyakavyotumika kwa ajili hiyo ambavyo ni vichache.
"Tanzania tumepata uenyeji wa mashindano hayo mawili ambayo ni makubwa hivyo lazima tuwe na viwanja vingi kwa ajili ya mazoezi na hichi kikiboreshwa kinaweza kutumika,"alisema Majaliwa.
Alisema kuwa wataangalia uwezekano wa uwanja huo kutumiwa kwa ajili ya mazoezi na tutaongea na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kama watakikubali itabidi kitumike.
"Kiwanja hichi kikiimarishwa vizuri kinaweza kutumika kwa ajili hata ya ligi kuu ni uwanja mzuri unahitaji maboresho kidogo tu kwani hata taa zipo kwa kweli hapa ni pazuri,"alisema Majaliwa.
Aidha alisema hayo ni matunda ya uwekezaji kwenye sekta ya michezo ambapo Rais Dk Samia Suluhu Hassan ameamua kuwekeza kwenye michezo.
"Kwa vijana wa Halaiki msiishie hapa endeleeni na mazoezi hii iwe ni sehemu ya kuanzia kwa wale watakaocheza mpira wa miguu, pete, riadha na michezo mingine ili muendeleze vipaji vyenu isiwe hapa ndiyo mwisho,"alisema Majaliwa.
No comments:
Post a Comment