Na
John Gagarini
WATANZANIA
wametkiwa kuunga na serikali ya awamu ya tano katika mapambano dhidi ya dawa za
kulevya na matumizi ya pombe za viroba kwa kutowajengea chuki wale wanaokabili
suala hilo.
Hayo
yalisemwa na Kuhani mkuu wa Kituo cha Maombi na Maombezi cha Gombo Gambusi Alista
Albano kilichopo Kibamba Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa vita hiyo ni ya
wananchi wote ili kuwanusuru Watanzania.
Albano
alisema kuwa dawa hizo na pombe hiyo imewafanya watumiaji kudhurika na
kushindwa kufanya kazi zao kikamilifu ambapo baadhi wamejikuta wakiwa wagonjwa
na wengine kufikia hatua ya kupoteza maisha.
“Tumuunge
mkono Rais wetu Dk John Magufuli katika vita hii ambayo imepewa nguvu na mkuu
wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda lakini kuna abaadhi ya watu wameonekana
kupingana na mapambano hayo jambo ambalo linashangaza,” alisema Albano.
Alisema
kuwa athari ya matumizi ya dawa na pombe hizo ni makubwa tofauti na watu
wanavyofikiria ambapo nguvu kazi kubwa imeathirika na kushindwa kuzalisha
kutokana na matumizi hayo.
“Sisi
kama kaanisa tunapaswa kuliombea Taifa ikiwa ni pamoja na viongozi wetu ambao
wanajaribu kuhakikisha wanatuletea maendeleo lakini kwanza wanaondoa vikwazo
vilivyokuwa vinazuia nchi ishindwe kupiga hatua ikiwemo dawa na pombe hizo,”
alisema Albano.
Aidha
alisema Magufuli ni moja ya viongozi ambao ni bora na wataleta mabadiliko
makubwa ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa nchi ambayo itazalisha na kutoa
misaada tofauti na ilivyo sasa imekuwa nchi ya kuomba wahisani.
“Hamasa
yake ya kuifanya Tanzinia kuwa nchi ya viwanda itafanya nchi kuwa na uzalishaji
wa bidhaa mbalimbali hivyo itasababisha uchumi kukua na kuwa moja ya nchi
zitakazokuwa zinatoa misaada kwa nchi nyingine,” alisema Albano.
Alibainisha
kuwa nchi kwa sasa inapita kwenye kipindi cha mpito lakini baadaye kila
mwananchi atafurahia maisha kwani anarejesha vile ambavyo viliporwa na watu
wachache ili viweze kutumiwa na watu wengi.
“Ninachowaomb
Watanzania wenzangu tuache kulalamika kwani tumebakia kulalamika badala ya
kufanya kazi kwani malamiko hayataweza kutusaidia badala yake yatatufanya
tusiwajibike,” alisema Albano.
Alisisitiza
kuwa Rais Magufuli ni mkombozi wa Taifa hili hivyo watu wamwombee katika
kuirekebisha nchi na kuiweka katika mazingira mazuri ya kutoa huduma nzuri kwa
wananchi wake.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment