Mwenyekiti wa Mtaa wa Kibwegere Edson Nyingi akiongea wakati wa kukabidhi vyoo vilivyokarabatiwa na shirika la Habitat for Humanit Tanzania |
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere kata ya Kibamba Halmashauri ya Ubungo wakishangilia baada ya kufanyika zoezi la kukabidhi vyoo vilivyokarabatiwa na shirika la Habitat for Humanity Tanzania |
Mwanafunzi wa darasa la nne shule ya Msingi KibwegereWitnes Hamaro akisoma risala ya shule wakati wa kukabidhiwa vyoo vilivyokarabatiwa na shirika la Habitat for Humanity Tanzania |
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibwegere |
Na
John Gagarini
JAMII
imetakiwa kutoitumia vibaya dhana ya elimu bure na kuacha uchangiaji kwenye
sekta ya elimu kwa kutotoa mchango wake kwa madai kuwa elimu inatolewa bure.
Hayo
yalisemwa na ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Manispaa ya Ubungo Hussein Masoud
wakati wa kupokea msaada wa ukarabati wa choo uliofanywa na Shirika lisilo la
Kiserikali la Habitat for Humanity Tanzania kwenye shule ya Msingi Kibwegere
kata ya Kibamba wilaya ya Ubungo.
Masoud
alisema kuwa katika kuwaondolea kero serikali iliondoa baadhi ya michango
iliyokuwa ikichangwa na wazazi ikiwemo ada lakini haijakataza wadau kuchangia
changamoto mbalimbali kwenye shule za msingi na sekonadri.
“Serikali
haijafunga milango kwa jamii kuchangia shule zetu kwani haiwezi ikafanya kila
kitu kutokana na uwezo wake bali inasaidiana na wadau wake kuchangia ili
kuzikabili changamoto mbalimbali zilizopo kwenye shule,” alisema Masoud.
Alisema
kuwa shule zina changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na upungufu wa madawati,
upungufu wa vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, vitabu na mambo mengine ya
kitaaluma.
“Tunaomba
wadau kama hawa waendelee kujitokeza na kuchangia pale wanapoona kuna hitaji
msaada ili watoto wetu waweze kusoma kwenye mazingira mazuri yatakayowafanya
wapate elimu bora,” alisema Masoud.
Naye
mkurugenzi wa Habitat For Humanity Tanzania Danny Mpogole alisema kuwa baada ya
kupokea changamoto hiyo wao kama wafanyakazi wa shirika hilo na wajumbe wa bodi
walijichangisha na kufanikisha ujenzi wa matundu matatu na sehemu ya kunawia na
kugharimu kiasi cha shilingi milioni 3.3.
Mpogole
alisema kuwa kufanikiwa ukarabati huo kutasaidia mazingira ya wanafunzi kufanya
vizuri na kuongeza ufaulu kwani itaongeza hamasa ya wanafunzi kusoma kwani
mazingira yao yatakuwa mazuri.
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Margareth Lukwekwe alilishukuru shirika
hilo na kusema kuwa limewapunguzia wanafunzi kero ya choo ambapo shule hiyo ina
wanafunzi 1,268.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment